Ijumaa, 7 Julai 2017

ROHO MTAKATIFU NI ROHO WA KRISTO.

Ingawa ROHO MTAKATIFU ni nafsi na Mwana, ameunganika na Mwana wala hawezi kutengwa naye, kama vile Mwana na Baba walivyounganika ROHO naye hawezi kutenganika.


Yohana 5

43 Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, wala ninyi hamnipokei; mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea huyo.

Pia


Yohana 14

26 Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia..


ROHO MTAKATIFU ni Roho wa YESU Kristo. Ana tabia ya Kristo kama vile YESU alivyokuwa na tabia ya Baba (Mdo 16:6-7, Warumi 8:8; Gal 4:6; Flp 1:19; 1Pet 1:11: pia Ebr1:3)


Kwa njia ya ROHO MTAKATIFU, YESU anaendelea kuwa pamoja na Wanafunzi wake, ingawa kimwili hayupo ulimwenguni tena 

(Yoh 14:18  Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu.

 Gal 2:20 Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.

Kol 1:27 ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika Mataifa, nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu


Katika ROHO MTAKATIFU tunaunganishwa kwa YESU NA KWA MUNGU katika wakati mmoja ambapo auanganishwaye katika hali hiyo huwa yuko katika ulimwengu wa ROHO na si vinginevyo.

Vile vile fikra zake zote haziwi nje ya kuwaza Matendo makuu ya MUNGU katika hali yake. Ndivyo ilivyo katika hali hiyo huwa tabia ya Mwamini inakuwa zaidi na viwango vya kumtafuta MUNGU huwa vya hali ya juu 


ROHO anaitwa Mshauri au Msaidizi kwa sababu anawapa wafuasi wa YESU ushauri na msaada kama vile YESU alivyowapa alipokuwa nao kimwili. Katika njia ya ROHO MTAKATIFU, kuwepo kwa YESU ambako katika karne ya kwanza kulikuwa na kikomo katika Palestina tu, kwa kweli huwa pasipo wakati wa duniani kote (Yn 14:16,18,26; 15:26; 16:7)

Kwa hiyo haiwezekani Kabisakuwa na ROHO MTAKATIFU pasipo kuwa na YESU Kristo. Hali kadhalika haiwezekani kuwa na uhusiano na MUNGU kwa njia ya ROHO, lakini siyo kwa njia ya Kristo (mdo 2:48; Rum 8:9-11). ROHO hajitukuzi mwenyewe juu ya Kristo, kwa sababu kazi YA ROHO ni kuwaongoza watu waje kwa Kristo (Yoh 15:26; 1Kor 12:3)


Hakuna mashindano kati ya ROHO na Kristo, kwa sababu ROHO ni Roho wa Kristo. Kuishi ndani ya Kristo ni kuishi ndani ya ROHO , na kuishi ndani ya ROHO ni kuishi ndani ya Kristo (Rum 8:1,9: 2Kor 3:14-18). Kama vile YESU Kristo alivyopokea mamlaka yake kutoka kwa Baba, alivyomtukutuza Baba, vivyo hivyo ROHO hupokea mamlaka yake kutoka kwa Kristo, humtukuza Kristo na huwafundisha watu mambo ya Kristo (linganisha Yoh 8:  28 Basi Yesu akawaambia, Mtakapokuwa mmekwisha kumwinua Mwana wa Adamu, ndipo mtakapofahamu ya kuwa mimi ndiye; na ya kuwa sifanyi neno kwa nafsi yangu, ila kama Baba alivyonifundisha ndivyo ninenavyo.

  na 

16:13 Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.


pia 


Yoh 17:4 Mimi nimekutukuza duniani, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye.

na 16:14 Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari.


pia


 Yoh 17:8 Kwa kuwa maneno uliyonipa nimewapa wao; nao wakayapokea, wakajua hakika ya kuwa nalitoka kwako, wakasadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.

 na Yoh 14:26 Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.

16:15 Na yote aliyo nayo Baba ni yangu; kwa hiyo nalisema ya kwamba atatwaa katika yaliyo yangu, na kuwapasheni habari.






MUNGU AWABARIKI


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni