Alhamisi, 13 Julai 2017

Ijumaa, 7 Julai 2017

ROHO MTAKATIFU NI ROHO WA KRISTO.

Ingawa ROHO MTAKATIFU ni nafsi na Mwana, ameunganika na Mwana wala hawezi kutengwa naye, kama vile Mwana na Baba walivyounganika ROHO naye hawezi kutenganika.


Yohana 5

43 Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, wala ninyi hamnipokei; mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea huyo.

Pia


Yohana 14

26 Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia..


ROHO MTAKATIFU ni Roho wa YESU Kristo. Ana tabia ya Kristo kama vile YESU alivyokuwa na tabia ya Baba (Mdo 16:6-7, Warumi 8:8; Gal 4:6; Flp 1:19; 1Pet 1:11: pia Ebr1:3)


Kwa njia ya ROHO MTAKATIFU, YESU anaendelea kuwa pamoja na Wanafunzi wake, ingawa kimwili hayupo ulimwenguni tena 

(Yoh 14:18  Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu.

 Gal 2:20 Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.

Kol 1:27 ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika Mataifa, nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu


Katika ROHO MTAKATIFU tunaunganishwa kwa YESU NA KWA MUNGU katika wakati mmoja ambapo auanganishwaye katika hali hiyo huwa yuko katika ulimwengu wa ROHO na si vinginevyo.

Vile vile fikra zake zote haziwi nje ya kuwaza Matendo makuu ya MUNGU katika hali yake. Ndivyo ilivyo katika hali hiyo huwa tabia ya Mwamini inakuwa zaidi na viwango vya kumtafuta MUNGU huwa vya hali ya juu 


ROHO anaitwa Mshauri au Msaidizi kwa sababu anawapa wafuasi wa YESU ushauri na msaada kama vile YESU alivyowapa alipokuwa nao kimwili. Katika njia ya ROHO MTAKATIFU, kuwepo kwa YESU ambako katika karne ya kwanza kulikuwa na kikomo katika Palestina tu, kwa kweli huwa pasipo wakati wa duniani kote (Yn 14:16,18,26; 15:26; 16:7)

Kwa hiyo haiwezekani Kabisakuwa na ROHO MTAKATIFU pasipo kuwa na YESU Kristo. Hali kadhalika haiwezekani kuwa na uhusiano na MUNGU kwa njia ya ROHO, lakini siyo kwa njia ya Kristo (mdo 2:48; Rum 8:9-11). ROHO hajitukuzi mwenyewe juu ya Kristo, kwa sababu kazi YA ROHO ni kuwaongoza watu waje kwa Kristo (Yoh 15:26; 1Kor 12:3)


Hakuna mashindano kati ya ROHO na Kristo, kwa sababu ROHO ni Roho wa Kristo. Kuishi ndani ya Kristo ni kuishi ndani ya ROHO , na kuishi ndani ya ROHO ni kuishi ndani ya Kristo (Rum 8:1,9: 2Kor 3:14-18). Kama vile YESU Kristo alivyopokea mamlaka yake kutoka kwa Baba, alivyomtukutuza Baba, vivyo hivyo ROHO hupokea mamlaka yake kutoka kwa Kristo, humtukuza Kristo na huwafundisha watu mambo ya Kristo (linganisha Yoh 8:  28 Basi Yesu akawaambia, Mtakapokuwa mmekwisha kumwinua Mwana wa Adamu, ndipo mtakapofahamu ya kuwa mimi ndiye; na ya kuwa sifanyi neno kwa nafsi yangu, ila kama Baba alivyonifundisha ndivyo ninenavyo.

  na 

16:13 Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.


pia 


Yoh 17:4 Mimi nimekutukuza duniani, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye.

na 16:14 Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari.


pia


 Yoh 17:8 Kwa kuwa maneno uliyonipa nimewapa wao; nao wakayapokea, wakajua hakika ya kuwa nalitoka kwako, wakasadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.

 na Yoh 14:26 Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.

16:15 Na yote aliyo nayo Baba ni yangu; kwa hiyo nalisema ya kwamba atatwaa katika yaliyo yangu, na kuwapasheni habari.






MUNGU AWABARIKI


Jumatatu, 26 Juni 2017

BIBLIA INAVYOSEMA JUU YA KUINUKA KWA UISLAM.

BIBLIA INAVYOSEMA JUU YA KUINUKA KWA UISLAM:

1 Malaika wa tano akapiga baragumu, nikaona nyota iliyotoka mbinguni, imeanguka juu ya nchi; naye akapewa ufunguo wa shimo la kuzimu.

2 Akalifungua shimo la kuzimu; moshi ukapanda kutoka mle shimoni kama moshi wa tanuru kubwa; jua na anga vikatiwa giza kwa sababu ya ule moshi wa shimoni.

3 Nzige wakatoka katika ule moshi, wakaenda juu ya nchi, wakapewa nguvu kama nguvu waliyo nayo nge wa nchi.

4 Wakaambiwa wasiyadhuru majani ya nchi, wala kitu cho chote kilicho kibichi, wala mti wo wote, ila wale watu wasio na muhuri ya Mungu katika vipaji vya nyuso zao.

Ufunuo wa Yohana 9:1-4

Hapa dini mpya inaoneshwa, ikiwa na baadhi ya mafundisho mazuri, NI NYOTA ILIYOANGUKA KUTOKA MBINGUNI, lakini ilikuwa imechanganyikana na MAFUNDISHO MACHAFU, moshi kutoka lile, "SHIMO LA KUZIMU"

Uislam ulianza kwa kulaani uovu wa ibada ya sanamu iliyokuwa inaendeshwa na kanisa la Roman Catholic, (NA HAPA ULIKUWA SAWA).

Kwa hakika kuna Mungu mmoja, na hakuna astahiliye kuabudiwa isipokuwa yeye. Lakini mafundisho ya Uislam yaliyokuwa yanahitajika kwa kanisa asi, YALILETA "MOSHI" KATIKA ULIMWENGU.

"SHIMO LA KUZIMU" katika kiyunani lina maana ya JANGWA au NYIKA yoyote iliyo ukiwa, na hivyo linafaa kabisa KUWAKILISHA JANGWA LA ARABUNI walikotokea wavamizi Waislam wa Kiarabu, KATIKA WINGI UNAOFANANA NA NZIGE.

Abyssos ni neno la Kiyunani linalomaanisha, "SHIMO LA KUZIMU"
na hilo ndilo linalotupatia neno la sasa la kiingereza, linalomaanisha KUZIMU. Waandishi wa kisasa wa Kiislam wanalitumia neno hilo kuielezea jamii ya Kiarabu alikotokea Muhammad: ARABIA@SHIMO LA GIZA.

Katika enzi hizo za ujinga uliokithiri, kulikuwa na eneo ambalo giza zito tena totoro lilikuwa limetuwama... ARABIA... Nalo lilikuwa pweke likiwa limetengwa na bahari kubwa sana ya mchanga. Wafanya biashara wa Kiarabu walikuwa wanasafiri mwendo mrefu kwa kujikokota wala hawakupata punje yoyote ya maarifa katika safari zao. Katika nchi yao hawakuwa na taasisi yoyote ya elimu wala maktaba. Hakuna aliyekuwa anaonekana kuwa na shauku ya kukuza ama kuendeleza elimu... Fikra zao zilikuwa zimejaa miiko, akili na jadi yao ilikuwa ni unyama na ukatili mkubwa, maadili na ufahamu wao vilikuwa vya kishenzi na visivyo staha.

"...Hakukuwa na sheria isipokuwa ile ya ukatili. Uporaji, mashambulizi na mauaji ya watu dhaifu wasio na hatia ilikuwa ndio kawaida... Tukio lolote dogo lilikuwa linaweza kusababisha vita kulipuka kwa hasira za kikatili...
Dhana yoyote waliyokuwa nayo juu ya maadili, utamaduni, na ustaarabu vilikuwa vinaonekana vya kizamani na ushenzi... Walikuwa wakiabudu mawe, miti, sanamu, nyota na mizimu, na kiufupi walikuwa wanaabudu chochote walichokuwa wanakifikria isipokuwa MUNGU.
(Rejea ABDUL A'LAMAUDUDI TOWARDS UNDERSTANDING ISLAM, UK. 41, 42, NAIROBI: THE ISLAMIC FOUNDATION, QUR'AN HOUSE 1973)

Siku moja mfalme Chosroes II wa Uajemi alipokea barua kutoka kwa raia mmoja wa Maka asiyefahamika, ikimtaka amtambue Muhammad kuwa ni nabii wa Mungu. Mfalme aliichana ile barua kwa dharau na akakataa madai ya nabii. Yeye hakujua kuwa, mapema, yeye mwenyewe ataangamia kabisa na ufalme wake pia kuangamizwa, NA KWAMBA NABII HUYU WA AJABU KUTOKA MAKA ANGETAWALA ULIMWENGU. Kuanguka kwa mfalme Chosroes kunafikriwa na wengine kuwa kulikuwa ndio, "UFUNGUO WA SHIMO LA KUZIMU", kwa sababu Muhammad asingeweza kuinuka katika kutawala isipokuwa kwa kuuangusha kwanza ufalme wa Waajemi.

NDIPO WAISLAM WA ZAMANI (SARACENS) KUTOKA UARABUNI, "WAKAPEWA NGUVU", NA KUONGEZEKA SANA MPAKA WAKAWA WENGI MNO KAMA NZIGE.

Bila ya kuwa na dhana ya kitabu cha Ufunuo akilini mwake, mwandishi mmoja alisema hivi juu ya hawa wafuasi wa Muhammad kuwa, " Wa-Osmanlis walisongamana kama NZIGE pande zote, na hakuna kijiji ambacho hakikuwafahamu, mpaka hata kuta za Constantinople". Kama vile nge anavyogonga, ndivyo walivyolipiza kisasi kwa ukatili katika vita.

Muhammad alipokufa, alirithiwa na Abubakari katika mwaka wa 632 B.K, ambaye aliwakusanya makabila ya kiarabu ili kufanya vita. Aliwaamuru wafuasi wake kuheshimu imani za watu wale waliokuwa wanazishika kwa uaminifu amri za Mungu. Ilikuwa inawapasa watu wake kuwaadhibu wale tu waliokuwa wanaabudu sanamu.

Akiwaamuru askari wake: "MSIUCHAFUE USHINDI WENU KWA DAMU ZA WANAWAKE NA AU WATOTO. MSIHARIBU MITENDE, WALA KUCHOMA MASHAMBA YO YOTE YA NAFAKA. MSIKATE MITI YO YOTE YA MATUNDA, WALA KUFANYA UHARIBIFU JUU YA MIFUGO, ISIPOKUWA WALE MTAKAOWAUA KWA CHAKULA.

Kadiri mtakavyoendelea mtawakuta baadhi ya watawa ambao wamejitenga na kuishi katika nyumba za watawa, wakiazimia wenyewe kumtumikia Mungu hivyo, MSIWASUMBUE NA WALA MSIWAUE WALA KUANGAMIZA MAKAZI YAO, na mtakuta aina ya watu wengine walio wa sinagogi la shetani, walionyoa utosi wao, hakikisheni mnapasua vichwa vyao, na msiwape nafasi mpaka ama wamegeuka kuwa Waislam au walipe " ushuru".

Ni watu gani waliokuwa na muhuri ya Mungu katika vipaji vya nyuso zao ambao askari wa Abubakari waliamuriwa kuwaacha?

Katika historia yote kumekuwa na waaminifu waliokuwa wanatunza Sabato ya kweli ya Bwana, ambayo ndiyo, "MUHURI YA MUNGU"

Katika siku za Muhammad na Abubakari kulikuwa na waaminifu kama hao. Inaonekana kuwa mwenye mamlaka kuu kuliko Muhammad watu wake waaminifu walindwe!
Waarabu walitumia mno Farasi katika vita vyao. Na "TAJI" inaweza kuwa kilemba, ambacho kwa muda mrefu kilikuwa ni kilemba cha taifa la Waarabu.
Askari walikuwa na nywele ndefu.

Mafungu 5-11

5 Wakapewa amri kwamba wasiwaue, bali wateswe miezi mitano. Na maumivu yao yalikuwa kama kuumwa na nge, aumapo mwanadamu.

6 Na siku zile wanadamu watatafuta mauti, wala hawataiona kamwe. Nao watatamani kufa, nayo mauti itawakimbia.

7 Na maumbo ya hao nzige yalikuwa kama farasi waliowekwa tayari kwa vita, na juu ya vichwa vyao kama taji, mfano wa dhahabu, na nyuso zao zilikuwa kama nyuso za wanadamu.

8 Nao walikuwa na nywele kama nywele za wanawake. Na meno yao yalikuwa kama meno ya simba.

9 Nao walikuwa na dirii kifuani kama dirii za chuma. Na sauti ya mabawa yao ilikuwa kama sauti ya magari, ya farasi wengi waendao kasi vitani.

10 Nao wana mikia kama ya nge, na miiba; na nguvu yao ya kuwadhuru wanadamu miezi mitano ilikuwa katika mikia yao.

11 Na juu yao wanaye mfalme, naye ni malaika wa kuzimu, jina lake kwa Kiebrania ni Abadoni, na kwa Kiyunani analo jina lake Apolioni.

Ufunuo wa Yohana 9 :5-11

Hapa tunalo jaribio juu ya usahihi wa unabii na kutimilika kwake kihistoria.

KATIKA UNABII WA BIBLIA SIKU MOJA NI MFANO WA MWAKA MMOJA, (Tazama maelezo ya sura 2:10). Kuna siku 30 katika mwezi wa unabii wa Biblia (linganisha mwanzo 7:11, 8:4 na 7:24 na pia linganisha miezi 42 ya Ufunuo 11:2 na siku 1260 za 11:3 na 12:6). Hivyo "MIEZI MITANO" ya kipindi cha unabii ni sawasawa na miaka 150.

Waislam hawa wa zamani, (SARACENS) "WALIPEWA AMRI", kuutesa " UTAWALA WA KIRUMI WA MASHARIKI KWA MIAKA HII 150, lakini siyo "KUWAUA", yaani siyo KUWASHINDA. Miaka 150 inapasa kuanzia wakati ule, " WATAKAPOKUWA NA MFALME WAO".

Kitabu cha Mithali kinasema, "NZIGE HAWANA MFALME, LAKINI HUENDA WOTE PAMOJA VIKOSI VIKOSI"
Mithali 30:27

Lakini, "NZIGE" wa Waislam, wavamizi walipangwa vizuri sana katika kazi ya kuangamiza, maana walikuwa na mtawala waliyekuwa wanafuata amri zake. Kwa mamia ya miaka baada ya kifo cha Muhammad, wafuasi wake waligawanyika katika makundi mbalimbali hasimu bila ya utawala wowote au mfalme. Lakini karibu na mwisho wa karne ya 13, Othman alianzisha na kuimarisha serikali iliyokuwa inajulikana kama ufalme wa Ottoman (Ufalme wa Kituruki).

"MALAIKA WA SHIMO LA KUZIMU" anaitwa "MALAIKA" katika fasili ya neno la kiyunani ambalo pia linamaanisha "MJUMBE" au "MHUDUMU". Sultani akawa mkuu wa dini ya Kiislam. Jina kwa Kiebrania "ABADONI", na kwa Kiyunani "APOLIONI" lina maana ya "YEYE AANGAMIZAYE". Hivyo ndivyo ilivyokuwa tabia ya watawala wa Kituruki (Ottoman).

Tunajiuliza ni lini Othman, kama mfalme wa kwanza wa Waislam alipofanya mashambulizi yake ya kwanza, "KUUTESA" ulimwengu wa kiistarabu wa Ufalme wa Mashariki?

Edward Gibbon, mtu ambaye aliandika historia lakini hakuamini katika Biblia, ametuachia tarehe ya usahihi zaidi kuwa Julai 27, 1299, ndiyo Othman alifanya mashambulizi yake ya kwanza juu ya Nicomedia.

Gibbon anasema kuwa, "USAHIHI" wa ajabu unaonekana kudhihirisha njozi fulani ya mbio na ukuzi wa uharibifu wa ubwana (Ufalme wa Kituruki).

Tunauliza tena. Je Waturuki "walitesa" ufalme wa Rumi wa Mashariki kwa miaka 150?  Ndiyo, historia inatuambia kuwa waliendeleza vita kuusumbua na kuutes ufalme huo tangu mwaka 1299 mpaka 1449 kwa miaka 150 kamili bila kuuteka kabisa. Halafu badiliko kuu lilitokea. Wafalme wa Rumi ya Mashariki waliendelea kudhoofika na kuwa wapotovu zaidi mpaka ikawa dhahiri kwa kila mtu kwamba muda kitambo wangepoteza uhuru wao.

Wakati mfalme Yohana alipofariki taehe 31 Oktoba, 1448, ndugu zake kwa unyenyekevu, ndugu zake waliomba idhini kwa Sultani wa Uturuki, Murad II, ili kumchagua ndugu yao mkubwa kutawazwa kama mfalme mpya katika mwezi Januari, 1449. Hivyo kwa kumnyenyekea Sultani wa Uturuki, walikiri kuwa uhuru wao ulikuwa umefikia mwisho. Kumbuka kuwa maelezo haya ni ya maana na yaliyo wazi kabisa.

Mafungu 12-15

12 Ole wa kwanza umekwisha pita. Tazama, bado ziko ole mbili, zinakuja baadaye.

13 Malaika wa sita akapiga baragumu, nikasikia sauti moja iliyotoka katika zile pembe za madhabahu ya dhahabu iliyo mbele za Mungu,

14 ikimwambia yule malaika wa sita aliyekuwa na baragumu, Wafungue nao malaika wanne waliofungwa kwenye mto mkubwa Frati.

15 Wale malaika wanne wakafunguliwa, waliokuwa wamewekwa tayari kwa ile saa na siku na mwezi na mwaka, ili kwamba waue theluthi ya wanadamu.

Ufunuo wa Yohana 9 :12-15

Ule "OLE WA KWANZA" ilikuwa ni kuinuka kwa nguvu ya Uislam. Baadaye ilikuwa ufuate "OLE WA PILI", na kuwa taabu kuu katika Ulaya. (Sura 11:14). Na "OLE WA TATU" ulikuwa uwe hasira ya kuogofya ya mataifa, pamoja na ghadhabu ya hukumu ya Mungu, itayoleta mwisho wa historia ya ulimwengu wetu (sura ya 11:18).

Katika mwaka 1449, "MALAIKA WA SITA" alifungulia kizuizi kilichokuwa kimewazuia Waislam kuuteka ufalme wa mashariki uliokuwa wenye utajiri na nguvu. Wale "MALAIKA WANNE WALIOFUNGWA KWENYE MTO MKUBWA FRATI" NI KIELELEZO KINACHOTAJA MAJIMBO MANNE TOFAUTI YA WAISLAMU YA ALEPPO, IKONIO, DAMESKI, NA BAGHDAD.

Na hivyo njia ilifunguliwa kwa Sultani ili baadaye aendeshe vita vya ushindi dhidi ya Ulaya. Mji wa Constantinople (sasa Istanbul) ulitekwa na majeshi ya Uturuki katika mwaka 1453.

Lakini zingatia hili: Miaka 150 ilipotimia katika mwaka 1449, uhuru wa mfalme wa Ulaya ulipotezwa siyo kwa mapigano, bali kwa mfalme kuusalimisha kwa hiari uhuru wao mikononi mwa Waturuki. Maana yake alisema. "SIWEZI KUTAWALA MPAKA KWANZA MRUHUSU". Kumbuka kwamba, kadiri tunavyosonga mbele, karibu utaona jambo muhimu mno.

Je ni kwa muda gani ufalme wa Waturuki Waislam ungeendelea kutawala kwa uhuru?

"Mwaka" mmoja wa siku 360 ni miaka halisi 360

Mwezi mmoja wa siku 30 ni miaka 30

Siku moja ya saa 24 ni mwaka 1

Saa 1/24 ya mwaka X 360 ni sawa na siku halisi 15

Jumla tutapata miaka 391 na siku 15

Ni lini hiki kipindi cha miaka 391 na siku 15 kilipoanza?

Ni dhahiri kuwa ni baada ya mwisho wa miaka 150 Waislam walipokoma "KUTESA" ufalme wa Mashariki maana waliutwaa. Baada ya kuongeza hiyo miaka 150 katika tarehe yetu ya kuanzia ya Julai 27, 1299, ni wazi kuwa tutafikia julai 27, 1499. Halafu ikiwa tutaongeza miaka 391 katika julai 27, 1499 tunafikia julai 27, 1840  Kisha ni lazima tuongeze siku nyingine 15.

Tunapata nini kama jibu kamili na la mwisho? Julai 27 ukiongeza siku 15 inapatikana Agost 11, 1840.

Je, Sultani wa Uturuki alipoteza Uhuru wake katika siku hiyo hasa kwa kujisalimisha kwa unyenyekevu na kwa hiari yake kwa watawala wa Ulaya kwa namna ile ile mfalme wa Rumi Mashariki alivyopoteza uhuru wake kwa Sultani mwaka 1449? Tutaona baadaye.

Ikiwa historia itasema ndiyo kwa swali hilo, tutakuwa na ushahidi wa hakika na kustaajabisha kwa mambo mawili:
Kwanza, kwamba utaratibu wa mwaka kwa siku wa kufasili unabii wa Biblia ni sahihi kabisa, na pili, kwamba kidole cha kuogofya cha Mungu kinaelekeza kwa jambo fulani pana na lenye maana kuliko kujifunza juu ya kuinuka na kuanguka kwa falme:

Kitabu cha Ufunuo ndio ufunguo Mungu aliotupatia kufungulia siri ya hukumu yake juu ya ulimwengu wetu wa siku hizi ulio mkaidi.

Pale msomaji asiyejali anapokuwa haoni kitu bali tu jangwa lisilofaa, katika kitabu cha Ufunuo sisi tunapata utajiri uliofichwa na wenye maana kubwa mno kwa watu wa Mungu. Kitambo kidogo tutaona ni nini historia inasema kilichotokea siku ya Agosti 11, 1840.

Kwanza, hebu na tuangalie kwa muda tu vipi Yohana anaelezea namna majeshi ya Kiislamu ya Uturuki yalivyowahi kutia hofu mataifa ya Ulaya kwa karne nyingi:

*Linganisha Maandiko Matakatifu yanavyouhesabu wakati katika UFUNUO 13:5, 12:6,14. Ni dhahiri kuwa "mwaka" wa Biblia ni siku 360 na "mwezi" wa Biblia ni siku 30.

Mafungu 16-19

16 Na hesabu ya majeshi ya wapanda farasi ilikuwa elfu ishirini mara elfu kumi; nilisikia hesabu yao.

17 Hiyo ndivyo nilivyowaona hao farasi katika maono yangu, nao waliokaa juu yao, wana dirii kifuani, kama za moto, na za samawi, na za kiberiti; na vichwa vya farasi hao ni kama vichwa vya simba, na katika vinywa vyao hutoka moto na moshi na kiberiti.

18 Theluthi ya wanadamu wakauawa kwa mapigo matatu hayo, kwa moto huo na moshi huo na kiberiti hicho, yaliyotoka katika vinywa vyao.

19 Kwa maana nguvu za hao farasi ni katika vinywa vyao, na katika mikia yao; maana mikia yao ni mfano wa nyoka, ina vichwa, nao wanadhuru kwa hivyo.

Ufunuo wa Yohana 9:16-19

HAPA KUNATAJWA MATUMIZI YA BARUTI KWA MARA YA KWANZA KATIKA HISTORIA YA MWANADAMU.

Kwa Yohana, ambaye kwa kweli hakuwahi kuona bunduki au baruti, mashujaa wa Kiislam wakiwa wamepanda farasi wakipiga bunduki zao wataonekana katika upeo wa macho yake kana kwamba, "KATIKA VINYWA VYAO HUTOKA MOTO NA MOSHI NA KIBERITI"

Mpaka mwaka 1453 B.K. kuta za mji wa Constantinople zilikuwa zimestahimili mashambulizi ya majeshi mengi, na hivyo ufalme ulikuwa umeokoka na hatari. Lakini sasa Waturuki wa Ottoman wakatumia kwa mara ya kwanza mizinga mipya na mikubwa pamoja na baruti katika kubomoa zile kuta zilizokuwa hapo awali haziingiliki. Kutumiwa kwa baruti na mizinga kulimaliza ulinzi wa mwisho wa jeuri ya ufalme wa zamani wa Warumi. Ubinafsi na ubadhirifu ulikuwa umeangamiza ustaarabu wa zamani.

Lakini sasa katika mwaka 1840, ubinafsi na ubadhirifu ulikuwa umepoozesha jeuri ya utawala wa Kiislam katika mwaka 1838, vita vikali vililipuka kati ya masultani wa Uturuki na Misri, Misri ikiwa mshindi.

Katika mwaka 1840, mataifa yenye nguvu manne ya Ulaya yaliingilia kati kwa kuhofia kwamba Misri ingeweza kwa muda mfupi kuchukua kiti cha enzi cha Sultani wa Uturuki katika kuhangaika kwake. Sultani ambaye alikuwa amedhoofishwa kwa hiari ALISALIMISHA UHURU WAKE MIKONONI MWA HAYA MATAIFA MANNE YA ULAYA, akiwaachia kumwendeshea mambo yake. Alimtuma mjumbe wake kwenda kwa mtawala wa Misri kutoa ujumbe kutoka kwa Mataifa manne ya Ulaya, ujumbe ulioweka mikononi mwao mambo yake.

Ilikuwa ni Agosti 11, 1840, ndiyo huyo mjumbe alipowasili Alexandria, na siku hiyo alikabidhi ujumbe mikononi mwa mtawala wa Misri.

Katika siku hiyo, uhuru wa Sultani ulikuwa wapi? ULIKUWA UMETOWEKA! Na "tangu siku hiyo. Uturuki ya Kiislamu imebakia tu kwa ruhusa na kutegemea kuungwa mkono na mataifa ya Ulaya".

Jambo hili lilipofahamika kwa umati wa wapenda Biblia walisadiki usahihi wa kanuni ya mwaka kwa siku ya kufasili unabii wa Biblia. Kilichoonekana kuwa si jambo la muhimu kihistoria kilitoa kwa dhati ushahidi wa kuridhisha kuwa vitabu vya Danieli na Ufunuo viliandikwa kwa uongozi wa Mungu, na vinatoa ujumbe muhimu sana kwa wakazi wa dunia ya sasa.

Wanazuoni na watafiti wa leo wanaweza kutofautiana katika kuhesabu wakati kipindi hiki cha miaka 391 kilipoanza na kumalizika. Jambo la kushangaza ni kwamba matukio makuu ya historia ndefu ya himaya ya Ottoman yanasimuliwa kwa usahihi kabla hayajatukia katika unabii. Kama tulivyoona katika Danieli mwitikio wa historia ni kama jiwe lililovunjwa linaloweza kurudishwa lilivyokuwa. Wapagani wengi waliongoka miaka ya 1840 kwa kushuhudia kutimizwa kwa unabii unaofuata kanuni ya MWAKA-SIKU na imani watu mamilioni wasiojulikana wamekuwa wakitiwa nguvu na unabii huu. Kwa hakika ndiye BWANA aliyekuwa ameutoa.

Mafungu 20, 21

20 Na wanadamu waliosalia, wasiouawa kwa mapigo hayo, hawakuzitubia zile kazi za mikono yao, hata wasiwasujudie mashetani, na sanamu za dhahabu na za fedha na za shaba na za mawe na za miti, zisizoweza kuona wala kusikia wala kuenenda.

21 Wala hawakuutubia uuaji wao, wala uchawi wao, wala uasherati wao, wala wivi wao.

Ufunuo wa Yohana 9:20-21

Ingawa makundi ya Waislamu yaliachwa huru juu ya ulimwengu wa Kikristo ulioasi, watu walikataa kujifunza somo la toba. Kwa hiyo tunaona kuwa Mungu huwa anaruhusu, "OLE" kuujia ulimwengu ili kuwafanya wenye dhambi kuzinduka, na kuwaongoza kuiendea toba. Ole baada ya ole zilifuatana, lakini bado wanadamu walikuwa wanazipenda dhambi zao. Je, "OLE WA TATU" utawaongoza kwenye toba? Wakati ule utakapofika, watakuwa wamechelewa mno!

Mpendwa unayesoma, Je, utajitoa moyo wako kwa toba leo?

*MSOMAJI AMBAYE ANGEPENDA KUONA DONDOO KUTOKA KWA MAGAZETI YA AGOSTI NA SEPTEMBA, 1840, YAKITOA MAELEZO KAMILI JUU YA MATUKIO YA AGOSTI 11, 1840, ANAWEZA KUANGALIA KATIKA KITABU CHA, "DANIEL AND THE REVELATION", KILICHOANDIKWA NA URIAH SMITH, KURASA 513-516.

MUNGU AWABARIKI

Jumatano, 10 Mei 2017

MOYO WA MTU HUAMBATANA NA MUNGU AU MALI.

MOYO WAKO UMEAMBATANA NA MUNGU AU MALI

HALELUYA

Mathayo 19;16~24

16 Na tazama mtu mmoja akamwendea akamwambia, Mwalimu nitende jambo gani jema ili nipate uzima wa milele?
17 Kwani kuniuliza habari ya wema? Alieye mwema ni mmoja. Lakini ukitaka kuingia katika uzima zishike amri
18 Akamwambia zipi? Yesu akasema, Ni hizi usiue,usizini,usiibe,usishuhudie uongo,
19 Waheshimu baba yako na mama yako na mpende jirani yako kama nafsi yako.
20 Yule kijana akamwambia, haya yote nimeyashika nimepungukiwa na nini tena?
21 Yesu akamwambia ukitaka kuwa mkamilifu enenda ukauze ulivyo navyo uwape masikini nawe utakuwa na hazina mbinguni kisha njoo unifuate
22 Yule kijana alipo sikia neno lile akaenda zake kwa huzuni kwa sababu alikuwa na mali nyingi.
23 Yesu akawaambia wanafunzi wake amini nawaambieni ya kwamba itakuwa shida tajili kuingia katika ufalme wa Mbinguni
24 *Nawaambia tena ni rahisi zaidi ngamia kupenya tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu*

Bwana Yesu apewe sifa sana

Tumesoma habari ya yule kijana tajiri anamuuliza Yesu kwamba afanye nn aulithi ufalme wa mbinguni. Kijana alipenda kwenda mbinguni na ndio maana anamuuliza Yesu kwamba afanye nn ili aingie mbinguni Yesu anamuuliza kama anazijua amri kijana alimjibu kuwa yote ameyashika na anayafanya sasa kwa kuwa alikuwa na shauku ya kutaka kuingia mbinguni anamuuliza nimepungukiwa nn tena kama ni amri anazijua na anayafanya ingekuwa ni mtu mwingine ingewezekana kwa kuwa Yesu amemwambia amri na anazijua angeishia hapo kuuliza angesha jua mbingu yangu lkn kijana akawa na shauku ili ajua labda kama amepungukiwa kitu kisimfanye aende mbinguni na Yesu ndipo anamjibu na Yesu aliijua shauku ya kijana na aliona kabisa huyu anapenda kwenda mbinguni na alijua pamoja na kijana kutaka kwenda mbinguni yulr kijana moyo wake ulikuwa haujashikamana na nae ila umeshikamana na mali ndipo anamwambia kauze vyote ulivyo navyo ukawape maskin kisha unifuate. Kijana aliondoka kwa huzuni sababu moyo wake ulikuwa kwenye mali na sio Mungu na ndio maana jibu la Yesu lilimfadhaisha sana. Ni kweli kijana alitaka kwenda mbingun lkn moyo haukuwa na Mungu bali mali
Yesu alipo kuwa anamwambia kijana akauze mali zake hakuwa na maana amfilisi ila alitaka kujua kama kweli moyo wake umeshikamana naye

Mpendwa Mungu anapo tuambia tumtolee sadaka si kwamba amataka pesa zetu sababu vyote ni mali yake anataka kupima mioyo yetu kama kweli tunampenda Mungu na kujitoa hata kwa mali kwa ajili yake. Na ndio maana anasema tutoe kwa hiyari yaan mioyo ya kupenda lkn pia maandiko yanasema hazina na mtu ilipo na moyo wake ulipo inamaana ww ukitoa kasehemu kadogo ka mali zako ndio kaupendo kako kalivyo kwa Mungu

Hebu tusome mf huu kwa baba yetu Ibrahimu tuone jinsi sadaka ilivyo na nguvu na Mungu jinsi anavyo tupima

Mwanzo 22;1~12
Hapa tunasoma habari za Ibrahimu. Mungu alimjaribu akamwambia amtoe sadaka mwanae wa pekee si kwamba Mungu alikuwa akimtaka Isaka na si kwamba Mungu alikuwa hajui kama Ibraimu hamchi yeye ila alimjaribu kuupima moyo wake kama kweli Ibrahimu anampenda Mungu kwa moyo wake na Mungu alithibitisha hilo kwamba kweli.Ibrahimu anampenda kwa maana hakumzuilia mwanae wa pekee alitaka kumchinja soma mstr wa 12

Hivyo mpendwa Mungu akikusemesha kwa habar ya kutoa hata kiwe kitu muhimu vip kwako toa sababu Mungu haitaji hicho anahitaji ule utayari wako wa kujitoa kwa moyo kwa ajili yako.

Je moyo wako.umeshikamana na nani Mungu au mali au kazi kama ni Mungu jipime unavyo jitoa kwa ajili ya Mungu ile kwa mali au muda hicho ndicho kitakacho kuthibitishia unampenda Mungu hebu muangalie mama mjane alitoa senti mbili lkn Yesu alimuona ametoa kuliko wote sababu hakutoa sehemu ya mali bali alitoa kwa moyo tena chote alicho nacho Mungu.anaangalia moyo wako unavyo jitoa angalii kiasi unachotoa na moyo ndio kipimo cha ww unampenda Mungu

kijana alishindwa kuendelea na Yesu sababu alikuwa na mali nyingi sana na moyo wake ulikuwa kwenye mali alizo nazo sio kwa Yesu

Je ww moyo wako uko wapi?
Je unampenda Mungu kweli?
Je unajitoa kiasi gani kwa ajili ya Mungu

Ibrahimu Mungu alipo uona moyo wake kwamba anamcha Mungu akumzuilia mwana wake wa pekee Mungu alimbariki Ibrahimu alitengeneza agano nae mpaka leo watu tujajibarikia katika uzao wake taifa la Israeli

SADAKA YAKO IAMBATANE NA MOYO WAKO NA MOYO WAKO UAMBATANE NA BWANA SI MALI.

Amosi 3;3 je! watu wawili waweza kutembea pamoja wasipokuwa wamepatana?
Hauwezi kutembea na mtu pasipo kupatana naye. Namaanisha Huwezi kutembea na Mungu au kuwa karibu na Mungu wakati moyo wako upo mbali nae na moyo wako kuwa karibu nae ni vile unavyo jitoa kwa ajili yake(MUNGU)  na kutembea katika sheria zake.

ROHO MTAKATIFU aendelee kukufundisha.

Barikiwa .

Jumanne, 2 Mei 2017

JE, YESU KRISTO NA MUHAMMAD WALITUMWA NA MUNGU MMOJA?

Kumekuwa na hoja moja ambayo inasumbua vichwa vya watu wengi.
Je, YESU NA MUHAMMADCWALITUMWA NA MUNGU MMOJA?
Leo nakata utepe kwa kutumia BIBLIA na Quran. Tunapaswa kuangalia hoja moja ya msingi, je kauli zao zinafanana? au zinapingana? Kama hazifanani yakupasa ujiulize mara mbili mbili, kati ya Moja na Mbili ipi iliabza kujitambulisha na ipi ilikanusha utambulisho.
Muhammad alizaliwa mwaka 570 bk,
Wakati anazaliwa aliikuta kauli hii
Mathayo : Mlango 3
17 na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.
Pia andiko hili alilikuta, ambalo ni KAULI YA MALAIKA
Luka : Mlango 1
32 Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake.
Hoja ya msingi ni kwamba, Je Malaika aliyetumwa na Mungu kusema kauli hii, ndiye aliyetumwa tena kupinga kauli tangulizi?
Lazima tujiulize kuhusu hili.
Tazama Quran 2:116
116.
Na ati wanasema: Mwenyezi Mungu ana mwana. Subhanahu! Ametakasika na hayo. Bali vyote viliomo mbinguni na duniani ni vyake. Vyote vinamt'ii Yeye.
Hii kauli ilikuja kupinga kauli inayopatikana kwenye LUKA 1:30-37
Ambayo inasema

Luka 1:
30. Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu.
31 Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu.
32 Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake.
33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho.
34 Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili, maana sijui mume?
35 Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.
36 Tena, tazama, jamaa yako Elisabeti naye amechukua mimba ya mtoto mwanamume katika uzee wake; na mwezi huu ni wa sita kwake yeye aliyeitwa tasa;
37 kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu.



Watu wote Wanajua kuwa MUNGU hawezi kujipinga atamkapo.

Hapo tu unapata picha kuwa, Wawili hawa walitoa ujumbe sehemu mbili tofauti.

Ukisoma Biblia iliyotangulia kuleta huu ujumbe juu ya YESU KUITWA MWANA WA MUNGU miaka 600 kabla ya kushuka aya zilizo kanusha ujumbe wa mwanzo.


Hapa yatupasa kuwa makini.


Tazama Quran 4:171


171.
Enyi Watu wa Kitabu! Msipite kiasi katika dini yenu, wala msimseme Mwenyezi Mungu ila kwa lilio kweli. Hakika Masihi Isa mwana wa Maryamu ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na neno lake tu alilo mpelekea Maryamu, na ni roho iliyo toka kwake. Basi Muaminini Mwenyezi Mungu na Mitume wake. Wala msiseme: Utatu. Komeni! Itakuwa kheri kwenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja tu. Ametukuka Yeye na kuwa na mwana. Ni vyake Yeye vyote viliomo katika mbingu na katika ardhi. Na Mwenyezi Mungu ni Mtegemewa wa kutosha.

Hii aya inapinga Maneno ya YESU yanayopatikana katika 

 YOHANA 9:35-37 inasema hivi


35 Yesu akasikia kwamba wamemtoa nje; naye alipomwona alisema, Wewe wamwamini Mwana wa Mungu?
36 Naye akajibu akasema, Ni nani, Bwana, nipate kumwamini?
37 Yesu akamwambia, Umemwona, naye anayesema nawe ndiye.
38 Akasema, Naamini, Bwana. Akamsujudia.
39 Yesu akasema, Mimi nimekuja ulimwenguni humu kwa hukumu, ili wao wasioona waone, nao wanaoona wawe vipofu.


Hapa kuna habari kuhusu vipofu wa kiroho, ambapo YESU anathibitisha kuwa ANAPASWA KUAMINIWA KUWA NDIYE MWANA WA MUNGU.

Kumbuka aya zinasema kuwa YESU HAKUFANYA DHAMBI HATA SIKU MOJA, 

Hivyo  kitendo cha Muhammad kusema kuwa YESU SI MWANA WA MUNGU NI Kumaanishi kuwa YESU ni mwongo baada ya kujiita MWANA WA MUNGU.



Na kama 
ni hivyo inamjumlisha na MALAIKA aliyrtumwa na MUNGU, pia MUNGU aliyemtuma MALAIKA + YESU WOTE NI WAONGO, HILI HALIKUBARIKI. Maana Aya zinasema YESU hakutenda dhambi na ujumbe wake hauwezi kuwa wa UONGO bali KWELI YAKE INABAKI KUWA KWELI MILELE YOTE.




Kwa mujibu wa Quran inaonyesha kuwa mwongo kwa kujiita MWANA WA MUNGU.
Hapa unapata jibu kuwa YESU na Muhammad walitumw na Miungu tofauti kulingana na maneno yao.


YESU ALIKIRI KWA KINYWA CHAKA PALE ALISEMA


YESU alisema anapaa kwenda kwa Baba yake, ambaye ni Mungu wake pia ni Baba yetu, pia Mungu wetu.



HUYU MUNGU ALIYE MTUMA YESU YEYE NI BABA WA WOTE,


Ila huyu aliyemtuma Muhammad hakubaliani na jambo hili na anadai kuwa inakaribia mbingu na ardhi kutatuka kisa Kuitwa Baba, yaana ukisema kuwa YESU ni Mwana wa Allah umeleta mtafaruku mkubwa.

Kwa ushahidi soma aya hii kutoka kwenye Quran 👇👇

Quran 19:

88.
Na wao ati husema kuwa Arrahmani Mwingi wa Rehema ana mwana!
89.
Hakika mmeleta jambo la kuchusha mno!
90.
Zinakaribia mbingu kutatuka kwa hilo, na ardhi kupasuka, na milima kuanguka vipande vipande.
91.
Kwa kudai kwao kuwa Arrahmani Mwingi wa Rehema ana mwana.
92.
Wala hahitajii Arrahmani Mwingi wa Rehema kuwa na mwana


.
Quran 6 : 101 Yeye ndiye Muumba wa mbingu na ardhi. Inamkinikaje Awe na mwana, hali Hana mke. Naye ndiye aliyeumba kila kitu (siyo baadhi yake kavizaa). Naye ni mjuzi wa kila kitu.

Inakuwa mjuzi wa kila kitu au muweza wa vyote ASHINDWE NA KITU KIMOJA TU!!! YAANA KUTO KUWA NA MWA A eti mpaka awe na mke?


Hapa unapata picha kuwa walitumwa na Miungu tofauti. Huhitaji kuvaa miwani ili ulione vizuri au ulielewe vyema.

👇👇👇👇
Quran 18:4-5


4. Na kiwaonye wale wanaosema Mwenyezi Mungu amejifanyia mtoto.

5. Wao hawana ilimu juu ya (jambo) hili wala baba zao ( hawana ujuzi juu ya jambo hili ilawanajisemea tu). Ni neno kubwa hilolitokalo katika vinywa vyao. Hawasemi ila uwongo tu.


Hapo ndio tupate kujua mbivu na mbichi.

Inamaana kuwa YESU ALIPOJIITA MWANA WA MUNG, alikosea na quran imekuja kupitia Muhammad imekuja kumuonya mtu ambaye hana kosa wala hakuwahi kutenda dhambi.


Kwa kauli ya Allah ya Muhammad mtume wake tunapata jibu kuwa YESU ni mwenye dhambi?

Haitokuwa hata siku kupata kosa la Yesu ila kujilisha upepo tu kewa Muhammad na mungu wake Allah.


Sasa twende kwenye utata huu ni kweli aliyejiita MWANA WA MUNGU ( ikaonekana ni kosa )  baadae aitwe MWENYE HEAHIMA MBINGUNI NA DUNIANI?

Quran 3:39

39. Mara Malaika akamlingania, hali amesima akisali chumbani, kwamba Mwenyezi Mungu anakupa khabari njema za (kuwa utazaa mtoto; umwite Yahya, atakaye kuwa mwenye kumsadikisha (Mtume atakayezaliwa)  kwa Nenolitokalo kwa Mwenyezi Mungu (Naye ni Nabii Isa) na  atakayekuwa Bwana kabisa na mtawa na nabii anayetokana na watu wema. (Naye ni nyinyi)


Aya hii inahusu kuzaliwa kwa YOHANA NA YESU. 


Kwanza Yohana atazaliwa na atatabiri kuhusu Ujio wa Yesu, na ya kuwa Yesu atakuwa Bwana.
Tafsiri ya BARWAN inasema MHEAHIMIWA MBINGUNI NA AKHERA.


Ni kweli huyu ATAKAYEKUWA MHESHIMIWA ndiye aliyejiita MWANA WA MUNGU?



Kwa kauli hii unapata picha kuwa Walitumwa na Miungu tofauti.


Kauli ya mwisho ya YESU NI HII


17 Yesu akamwambia. Usinishike; kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu (YOHANA 20:17)




MUNGU NI BABA YAKE, PIA NI BABA YETU. Huo ndio ukweli.

HUO NDIO UKWELI.

Aliyemtuma  YESU ni Tofauti na aliyemtuma Muhammad.


Huo ndio utofauti wao.
Mmoja ana mwana mwingine hana.



KAULI YA WA KWANZA HAIWEZI kupingwa baada ya miaka 600




TAMBUA KUWA ALIYEMTUMA YESU ANAKUBALI KUITWA BABA, Hii ni tofauti na aliyemtuma Muhammad.

Jumamosi, 25 Machi 2017

SUALA ZIMA ZA USHOGA KIBIBLIA

SUALA ZIMA LA USHOGA (MWANAUME KUOLEWA AU KUMUOA MWANAUME MWENZIWE)

Ni jambo ambalo ni chukizo kubwa sana mbele za MUNGU BABA, na mbele za Mwana-kondoo pamoja na Malaika WATAKATIFU wote. Wakati wa Ibrahimu na LUTU, MUNGU aliamua kuichoma Miji miwili, SODOMA NA GOMORA. kwa sababu ya dhambi hiyo 👇

Mwanzo 19: 12 Basi wale watu wakamwambia Lutu, Je! Unaye mtu hapa zaidi? Mkwe, wanao, na binti zako, na wo wote ulio nao katika mji, uwatoe katika mahali hapa;

13 maana tutapaharibu sisi mahali hapa, kwa kuwa kilio chake kimezidi mbele za BWANA; naye BWANA ametupeleka tupaharibu.

MUNGU hakuishia tu kuwaangamiza watu wa SODOMA na GOMORA, walioendekeza vitendo vya UFIRAJI na ULAWITI! hata wakati wa MUSA, Mungu aliweka sheria hiyo hiyo ya KIFO kwa watu wanaojihusisha na mapenzi ya JINSIA moja. 👇

Walawi 18:22 Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo.

Walawi 20:13 Tena mtu mume akilala pamoja na mtu mume, kama alalavyo na mtu mke, wote wawili wamefanya machukizo; hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao.

Suala zima la USHOGA, ni dhambi mbaya ambayo adhabu yake ni KIFO! haikuwa na msamaha kama ulivyo UONGO, uzushi, Ufisadi. Wahusika hawakupewa nafasi ya kutubia dhambi zao, hata kama wamefanya pasina kujua kuwa ni MACHUKIZO mbele za MUNGU! maana watu wa SODOMA na GOMORA hawakuwa wamepewa sheria ya kuwakataza kufanya kitendo hicho, lakini waliweza kuangamizwa! Kanisa LEO lipo kimya kabisa, na halichukui hatua yo yote kwa Wahuni wanaofungua makanisa kisha kufungisha ndoa za JINSIA hiyo, kitendo Ambacho kinatafsiriwa na wasiokuwa Wakristo kuwa, ni Halali KUFUNGISHWA ndoa hizo katika makanisa, na ukimya wa VIONGOZI wakubwa, ndiyo sababu ya Vitendo hivyo kushamiri, na kuendelea kuliharibia SIFA kanisa la MUNGU! japo maandiko yanasema 👇

Warumi 1:26 Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili;

27 wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao.

28 Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.

Haina maana kwamba, MUNGU ameruhusu, la hasha! bali aliwaacha wayafanye hayo kisha wakapata malipo yaliyowastahili ambayo ni Mauti! Mungu hakutoa kibali hicho, kitendo cha KANISA, kukaa tu na kuwaacha Wahuni hao waendelee kujenga makanisa na kisha kufungisha ndoa za JINSIA MOJA ni dhahiri kuwa KANISA linakubaliana na Wahuni, maandiko yanasema. 👇

Warumi 1:32 ambao wakijua sana hukumu ya haki ya Mungu, ya kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti, wanatenda hayo, wala si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao.

Maandiko yanasema, hao wayatendayo hayo, kwa hukumu ya MUNGU ambayo ni ya haki wamestahili mauti, siyo tu wanaojihusisha na VITENDO hivyo, bali hata na wale wanaokubaliana navyo! nao pia wamestahili mauti. Kukubaliana navyo siyo lazima uifungishe ndoa hiyo, hata kitendo cha Kuwaacha wayatumie Makanisa na hatua ya kuwazuia haichukuliwi, basi ni kitendo cha kukubaliana nacho! na imekuwa ni machukizo kwa MUNGU, hata kuzififisha nguvu za KANISA, Yesu alipoona Hekalu limegeuzwa kuwa PANGO LA WAFANYA BIASHARA, alichukua hatua. 👇

Yohana 2:13 Na Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu; naye Yesu akakwea mpaka Yerusalemu.

14 Akaona pale hekaluni watu waliokuwa wakiuza ng'ombe na kondoo na njiwa, na wenye kuvunja fedha wameketi.

15 Akafanya kikoto cha kambaa, akawatoa wote katika hekalu, na kondoo na ng'ombe; akamwaga fedha za wenye kuvunja fedha, akazipindua meza zao;

16 akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, Yaondoeni haya; msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya biashara.

17 Wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa imeandikwa, Wivu wa nyumba yako utanila.

Sisi LEO ujasiri huu wa YESU KRISTO, tunashindwaje kuwa nao? tunashindwaje kupindua madhabahu zao wafungishao ndoa za JINSIA moja? Paulo alipoona KANISA LA KORINTHO limeanza kuingiza mambo ambayo hayastahili kuwamo ndani ya Kanisa, alichukua hatua ya kuwakemea, kuwa Mkusanyiko waoABEL SULEIMAN SHILIWA:
siyo wa WAFAIDA bali kwa hasara. 👇

1 Korintho 11:16 Lakini mtu ye yote akitaka kuleta fitina, sisi hatuna desturi kama hiyo, wala makanisa ya Mungu.

17 Lakini katika kuagiza haya, siwasifu, ya kwamba mnakusanyika, si kwa faida bali kwa hasara.

18 Kwa maana kwanza mkutanikapo kanisani nasikia kuna faraka kwenu; nami nusu nasadiki;

19 kwa maana lazima kuwapo na uzushi kwenu, ili waliokubaliwa wawe dhahiri kwenu.

20 Basi mkutanikapo pamoja haiwezekani kula chakula cha Bwana;

21 kwa maana kila mmoja hutangulia kutwaa chakula chake katika kule kula; hata huyu ana njaa, na huyu amelewa.

22 Je! Hamna nyumba za kulia na kunywea? Au mnalidharau kanisa la Mungu, na kuwatahayarisha hao wasio na kitu? Niwaambieni? Niwasifu? La! Siwasifu kwa ajili ya hayo.

Hata kama unaamini kuwa wewe haushi CHINI ya sheria, bado siyo sababu ya kukaa kimya! Kwani hao ambao wanafanya hayo, sheria bado inawahusu. 👇

1 TIMOTHEO 1:8 Lakini twajua ya kuwa sheria ni njema, kama mtu akiitumia kwa njia iliyo halali;

9 akilifahamu neno hili, ya kuwa sheria haimhusu mtu wa haki, bali waasi, na wasio wataratibu, na makafiri, na wenye dhambi, na wanajisi, na wasiomcha Mungu, na wapigao baba zao, na wapigao mama zao, na wauaji,

10 na wazinifu, na wafiraji, na waibao watu, na waongo, nao waapao kwa uongo; na likiwapo neno lo lote linginelo lisilopatana na mafundisho yenye uzima;

HAO WATU NI LAZIMA WASHUGHULIKIWE KWA SABABU SHERIA INAWAHUSU WAO, WEWE AMBAYE HUFANYI HAYO, UHUSIKI KATIKA SHERIA. KANISA LIAMKE.

Asanteni Wote mliosoma post hii

Mungu awabariki

Ijumaa, 17 Machi 2017

BWANA YESU ANAWATAFUTA WALIO WAKE Waihubiri INJILI

Bwana YESU anawatafuta watu walio waaminifu  ili waipeleke injili yake.
Anawatafute wateule wanaojua wajibu wao, majukumu yao na wito wao.
Ndugu, inakuaje unapenda kusifiwa na bosi wako kazini lakini hutaki kusifiwa na Bwana YESU aliyekupa injili yake ili uipeleke kwa watu wote?
Wewe hutaki kuipeleka injili, uko busy tu na kazi yako yenye malipo duniani tu na sio mbinguni.
Ndugu peleka injili ya KRISTO mbele, peleka injili kwa kuhubiri watu. Kama huna muda wa kuhubiri basi ipeleke injili kwa pesa yako kwa kuwasapoti wanaoipeleka injili. Peleka injili hata kwa kusambaza vipeperushi vya Neno la MUNGU, peleka injili hata kwa kuwaalika watu kwenda kwenye mikutano ya injili na ibadani kanisani, ni jukumu lako kuipeleka injili, ndugu timiza jukumu lako.
Kuna faida katika kumwamini YESU KRISTO na kulitii Neno la MUNGU.

Faida baadhi za kumwamini YESU na kulitii neno lake ni:

1.  Kuwa pamoja na KRISTO.
Mathayo 28:19-20 " Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la BABA, na MWANA, na ROHO MTAKATIFU ; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari."

2.  Kutenda mema.
2 Timotheo 3:16-17 " Kila andiko, lenye pumzi ya MUNGU, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;  ili mtu wa MUNGU awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema."

3.  Kushiriki pendo la MUNGU baada ya kumaliza kazi duniani.
Yohana 3:16 " Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele."

Ndugu yangu nakuomba sana ihubiri injili ya KRISTO siku zote, huku ukiishi maisha matakatifu katika yeye na huku ukimtii ROHO MTAKATIFU.
MUNGU akubariki sana.

Jumanne, 14 Machi 2017

ALIYEMJUA YESU HAWEZI KUMWACHA KIRAHISI

UKIPATA NEEMA YA KUSOMA BIBLIA NA KUELEWA KILICHOANDIKWA HUMO, Hakika wewe ni mheri.

Mengi yamesemwa kuhusu waliokuwa wakristo hatimaye kuamua kumwacha YESU kwa visingizio visivyokuwa na maana yoyote, hivyo basi wamekuwa mashuhuri wa kupotosha maandiko kama ilivyoandikwa ya kuwa HUYAPOTOSHA MAANDIKO KWA HASARA YA NAFSI ZAO na ni hatari kwa mpotoshaji maana haina maana yoyo ili anaiangamiza nafsi yake.

Soma hapa 👇👇

2PETRO 3

14 Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia mambo hayo, fanyeni bidii ili mwonekane katika amani kuwa hamna mawaa wala aibu mbele yake.
15 Nanyi uhesabuni uvumilivu wa Bwana wetu kuwa ni wokovu, kama vile na ndugu yetu mpenzi Paulo alivyowaandikia kwa hekima aliyopewa;
16 vile vile kama katika nyaraka zake zote pia, akitoa humo habari za mambo hayo; katika nyaraka hizo yamo mambo ambayo ni vigumu kuelewa nayo; na mambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara, huyapotoa, kama vile wayapotoavyo na maandiko mengine, kwa uvunjifu wao wenyewe.

Wao hujifanya waalimu wa neno wakati hawana maarifa, elimu wala uelewa juu ya madai yao.

Nakupa faida ya kulijua Neno la MUNGU, na kwa nini huwezi kumwacha YESU kama unalinua  na umeliewa Neno lake.

Ni ujumbe mrefu ila jitahita kusoma aya na fafanuzi zake kama niatakavyo elezea katika Mathayo 5-7 ni sura 3 ambazo najaribu kukupa mwanga kwazo.

Mathayo 5

8 Heri wenye moyo safi;Maana hao watamwona Mungu.

1. Huwezi kumwacha Mungu eti kisa una Moyo safi.

Yesu amesema wewe una heri. Je waweza kumwacha Yesu kisa hilo?
Jibu ni hapana kwa kuwa unajua kuwa YESU alisema kweli hivyo huwezi kumwacha.

9 Heri wapatanishi;Maana hao wataitwa wana wa Mungu.

2. Ukijua kuwa Yesu ndiye Aliyesema neno hili Huwezi kumwacha.
Upatanishi wako hukuunganisha na Mungu.

10 Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki;Maana ufalme wa mbinguni ni wao.

Unapoijua haki huwezi kumwacha Yesu kwa kuwa haki yote yapatikana kwa Yesu

11 Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu.
12 Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu.

Ukimjua YESU huwezi kumwacha eti kisa wanakusema vibaya kwa ajiri yake, maana jibu unalo kuwa Thawabu yako ni kubwa mbinguni. katika kuudhiwa kwa ajili ya YESU Kuna malipo mazuri sana kule mbinguni kwa ajili yako.

13 Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu.
14 Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima.
15 Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani.
16 Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.

Unapomjua Yesu unapata nibu kuwa kakufanya kuwa nuru na chumvi ya Ulimwengu.

Sote tunajua kuwa nuru ni njema, pia chumvi ni njema pindi iwapo katika ubora wake. Ubora wako ni katika Yesu kristo na si vinginevyo.

Unapotembea katika neno lake huitwa chumvi safi/ nuru. Ukimwacha huitwa giza / chumvi iliyo haribiki.
Ukimjua Yesu ipasavyo huwezi kukubari kuitwa giza au chumvi iliyoharibika.

Kitendo cha kumwacha maana Yake wewe na mbingu ni kama maji na mafuta. Huna nafasi yoyote mbinguni, maana yake unajivua nguo na kubaki uchi!!! Hii ni hatari.
Ukilijua hilo huwezi kumwacha YESU.

17 Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.
18 Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie.
19 Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.
20 Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.

Huwezi kumwacha Yesu kwa kuwa tayari ashakwambia Torati ni kamili haijachakachuliwa (amri na sheria) hivyo yakupasa kutenda haki kuliko mafarisayo na waandishi.
YAKUPASA
Kuzitii amri na sheria kwa ajili ya UFALME WA MUNGU. Ukimwacha Yesu huwezi kuzitenda maana ukiwa na Yesu anakukumbusha ipasavyo kutenda ili uende mbinguni.

Je uko tayari kumwacha baada ya kumjua kuwa Yeye anataka uzitii ili uwe nae mbinguni?

21 Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu.
22 Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto.
23 Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako,
24 iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako.
25 Patana na mshitaki wako upesi, wakati uwapo pamoja naye njiani; yule mshitaki asije akakupeleka kwa kadhi, na kadhi akakupeleka kwa askari, ukatupwa gerezani.
26 Amin, nakuambia, Hutoki humo kamwe hata uishe kulipa senti ya mwisho.

Uko tayari kumwacha Yesu kisa unakosna najirani yako?
Njia nyepesi amekupa ili uendelee kuwa nae moyoni ya kuwa Ni kwenda kumuomba msamaha mshtaki wako ili uwe huru.
Je unaweza kukataa kutubu ? Jibu ni hapana, hicho sicho kiwezacho kukutenga na na Yesu baada ya kumjua.

27 Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini;
28 lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.

Kuzini kunaepukika ili uendelee kuwa na Yesu.
Je, hicho ndo cha kukutenga Yesu?
Ukitenganishwa na hicho wewe hukumjua Yesu. Aliyemjua Yesu huikimbia dunia na tamaa zake.

31 Imenenwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe hati ya talaka;
32 lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.

Uko tayari kuongeza kimada? Ukiongeza hukumjua Yesu na hiyo siyo sababu ya KUMWACHA YESU. ukimwacha Yesu kwa tatizo ni dhahiri kuwa hukumjua hata usidanganye watu.

33 Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana nyapo zako;
34 lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu;
35 wala kwa nchi, kwa maana ndiyo pa kuwekea miguu yake; wala kwa Yerusalemu, kwa maana ndio mji wa Mfalme mkuu.
36 Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi.
37 Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu.

Ukimjua YESU huwezi kuwa na viapo vya ajabu ajabu, maana jibu liko hapo juu kwenye aya hizo.

38 Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino;
39 Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili.
40 Na mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia.
41 Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye mbili.
42 Akuombaye, mpe; naye atakaye kukopa kwako, usimpe kisogo.

Aliyemjua Yesu hana mda wa visasi, ukiona umehadaliwa kwa hilo ujue wewe hukumjua Yesu.

Aliyemjua Yesu hana mkono wa birika hata kwa adui yake.


43 Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;
44 lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,
45 ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.
46 Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo?
47 Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo?
48 Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.

Aliyemjua Yesu ni mtu wa uprndo. Ukiona mtu asiye na upendo huyo hakumjua Yesu.
Alikuwa msanii wa maneno ya ajabu ajabu hatimae akaanguka katika dunia. Hilo si la kukufanya umwache Yesu.

Ukimwacha kwa hilo ni bayana na hakika kuwa hukumjua YESU .

Mathayo 6

1 Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni.
2 Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu.
3 Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume;
4 sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.

Unakuta mtu analalamika eti hasifiwi atendapo mema, anaanza kugoma hata kwenda kanisani.
Nani kasema umeumbwa usifiwe?

Faida ya kusifiwa ni nini hata umwachr Yesu. Amwachaye Yesu kwa sababu hiyo ujue huyo hakumjua Yesu.

9 Basi ninyi salini hivi;Baba yetu uliye mbinguni,Jina lako litukuzwe,Ufalme wako uje,
10 Mapenzi yako yatimizwe,hapa duniani kama huko mbinguni.
11 Utupe leo riziki yetu.
12 Utusamehe deni zetu,kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.
13 Na usitutie majaribuni,lakini utuokoe na yule mwovu.[Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele.Amina.]
14 Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi.
15 Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.

Aliyemjua YESU anasamehe aliyemkosea
hicho ndicho cha kukufanya umwache Yesu?

ukiamwacha kisa tu hutaki kumsamehe aliyekukosea, hiyo inathibitisha kuwa hukumjua YESU.

19 Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba;
20 bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi;
21 kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.

Aliye mjua YESU hazina Yake iko mbinguni, unaweza kumwacha Yesu eti kisa unataka maghorofa duniani?

Aliyemjua Yesu hafanyi hivyo. Afanyaye hivyo hakumjua hata asidanganye watu.


24 Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.

25 Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi?
26 Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao?
27 Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja?
28 Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti
29 nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo.
30 Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?
31 Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?
32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.
33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
34 Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.

Aliyemjua Yesu anamtukia Mungu na si mali. Ukiona mtu anakwambia mi hata kanisani siendi, natafuta mali,
Ujue huyo hakumjua Yesu.

Ndio maana YESU anakwambia mapema usiisumbukie dunia.

Mathayo 7
13 Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo.
14 Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.

Aliyemjua Yesu hatishwi na wingi wa walio kinyume nae, maana anajua kabisa kuwa Yesu ndiye kielelezo na si wingi wa wale wajisifiao kuwa wsko wsko kihaki kuliko wingine.

24 Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;
25 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba.
26 Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga;
27 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa.
28 Ikawa, Yesu alipoyamaliza maneno hayo, makutano walishangaa mno kwa mafundisho yake;
29 kwa maana alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye amri, wala si kama waandishi wao.

Aliye mjua YESU hawezi kuwa na tumaini kwa mwingine, ila tumaini liko kwa YESU, ukiona anayemwacha YESU na kuweka tumaini kwa mwingine huyo hakumjua YESU.

NDIO MAANA NINASEMA ALIYEMJUA YESU HAWEZI KUWACHA KIRAHISI.   YESU NI NJIA KWELI NA UZIMA.

UKISHAJUA KUWA YESU NDIYE NJIA, KWELI NA UZIMA je tumaini lako utakuwa umelielekeza kwa nani?

ALIYE MJUA YESU HAWEZI KUMWACHA NA Kumfuata asiye na tumaini la maisha yake.

YESU NI YOTE NDANI YA YOTE.

NDIO MAANA IMEANDIKWA KUWA ATARUDI KUWACHUKUA WALIO WAKE. Je ukimwacha utakuwa mgeni wa nani?

TAFAKARI CHUKUA HATUA.
.

Jumamosi, 11 Machi 2017

NAMNA YA KUJUA KUWA UMEITWA NA MUNGU KUWA MWALIMU WA NENO LAKE

✍📖📚 *NAMNA YA KUJUA KAMA UMEITWA NA MUNGU KUWA MWALIMU WA NENO LAKE*

*NA MWL MWAKASEGE*

*JANUARY 2017  (ARUSHA UWANJA WA RELI)*

>>Ni muhimu sana kujua kama umeitwa mapema hata kabla ya kuanza huduma ya ualimu. Jambo hili limetokana na ushuhuda wangu mwenyewe wa namna nilivyohangaika sana kujua nimeitwa kuwa Mwalimu wa neno la Mungu.

>>Wakati ule wito ulipokuwa unawaka ndani yangu nilifikiria kazi moja ya kuwa inatakiwa niwe *mchungaji*. Sasa kwa wakati ule huduma ya ualimu ilikuwa haijulikani sana labda mwalimu wa kufundisha tu darasa la waliokoka hivi karibuni au ufundishe Sunday school. Lengo la mimi kwenda kusomea uchungaji ilikuwa ni ili niwe na watu wangu wa kuwafundisha. Kwa wakati ule kupata nafasi ya kuhubiri mahali kama wewe sio mwinjilisti au mchungaji  ilikuwa ni ngumu sana.

>>Na wakati nimeandaa mazingira tayari yakwenda kusomea uchungaji, siku moja  nimekaa kwangu ghafla Roho Mtakatifu anisema na mimi wazi wazi *Kuwa kule kusomea uchungaji kakutuma nani?*  na aliniambia *nitakufundisha mwenyewe*.

Niliwaza sana namna wale watu humo katikati walivyonisaidia hadi kupata nafasi ya kusomea uchungaji, basi niliwatafuta wale watu na nikawaomba msamaha kuwa sikusikia vizuri kwa Mungu. Lakini ilikuwa ni gharama sana.

Sasa fikiria wangenisaidia kusomea uchungaji lakini ni nje ya mapenzi ya Mungu, na ningekuwa mchungaji  lakini nje ya mapenzi ya Mungu, unafikiri gharama yake ingekuaje.

>>Niliomba Mungu anisaidie kujua namna ya kusikia sauti yake.  Na kwa wito wa kipindi kile wa kumtumikia Mungu ilikuwa ni kuimba Kwaya au kuwa mwinjilisti. Basi nilienda kuimba kwaya sasa nako ilikuwa ngumu kweli kweli. Maana nilimwambia yule mwalimu wa kwaya kuwa nahitaji kumuimbia Mungu. Aliniuliza unaimba sauti ya ngapi sasa na mimi nilikuwa sijui kuwa naimba sauti ya ngapi?. Akasema sawa akanipanga sauti ya kwanza. Sasa nako nikawa naimba sauti mara inapanda na kushukua, basi akanihamishia base. Nako nilijua kuwa sifit maana niliona kuna watu wanabase nzuri kuliko ya kwangu. Nikahamia kwa wapiga vyombo niliona namna watu walivyowatalaam kupiga gitaa basi nako kulinishinda. Nilijaribu drums nazo zilinishinda kuchanganya. Sasa nikajaribu tumba nazo ikawa tabu. Sasa niliona kuna mabati yale yamekaa kama mifuniko ya sufuria(crush) basi ndio nikawa napiga maana sikuona mtu anapiga kwa hiyo nikayawahi mimi. Ndio nikawa mpigaji wa hayo mabati.

>>Baadae nikaacha nikaanza kuhubiri kama mwinjilisti lakini naiga. Si unajua unaweza ukawa unacopy kila kitu kutoka kwa mwinjilisti Fulani. Siku moja nilikuwa nahubiri Kijenge kwenye mkutano wa nje. Mzee Moses Kulola alikuja nae kusikiilza akasema _*Yoooooh huyu ni Mwalimu sio mwinjilisti.*_

>>Usipofahamu  kuwa umeitiwa wapi inakuwa ni tabu sana. Maana kwa wakati ule hata kupata vitabu vya kukuelezea ualimu kama huduma moja wapo ambayo Mungu kaitoa , vitabu havielezi sana juu ya ualimu.  Na nilisoma ushuhuda wa  mtumishi mmoja huko Marekani  kuwa yeye alikuwa mchungaji kwa miaka kama 12 ivi na alipoacha kuwa mchungaji na kuwa Mwl wa neno la Mungu ndipo Mungu akasema kuanzia hapa sasa ndio umeanza kunitumika. Yule mtu alisema ngoja kwanza,  yaani miaka yote niliyokutumikia ilikuaje na mbona ulikuwa unanibariki. Mungu alimwambia yule mtu kuwa sikukuita ili  uwe mchungaji na nilikuwa nabariki neno langu. Nilikuwa sikubariki wewe.

>> Pia wakati Fulani nilipigiwa simu na askofu Fulani wa Califonia Marekani, aliniambia Bwana Mwakasege tumesikia huduma yako ila tunahitaji uje kanisani kwetu uwe askofu, na ukikubali tu umasikini bye bye.  Ila nilikataa, akasema basi ngoja tundelee kuomba wazee wake wa kanisa wakawa wanaomba kwa Mungu na kukemea ili nikubali, ila nilikataa maana nilijua ule sio wito nilioitiwa mimi. Kanisani kwake huyo askofu nimewahi hubiri ila nafasi waliyotaka kunipa ndio nilikataa maana ilikuwa nje ya mapenzi ya Mungu.

>>Siku moja nilikuwa Nairobi, na kulikuwa na semina ya wainjilist ilikuwa inaandaliwa Uholanzi, na kulikuwa na shirika moja linaandikisha watu kwa ajili ya kwenda hiyo semina. Basi kulikuwa na rafiki yangu aliniuliza vp umejaza? Nikamwambia hapana sijajaza akasema kwanini,, nilisema naona uzito yule ndugu aliniambia wewe jaza tu. Basi akanijazia na akaituma. Baada ya muda kidogo nikiwa Tanzania nilipata ujumbe Toka Marekani kwa ile huduma ya Bilgram iliyokuwa inaandaa ile semina kuwa ndugu tumekaa kwenye maombi na fomu yako ila tumeona kuwa Mungu hajakuita kuwa mwinjilisti kwa hiyo tunaona bora tuwape nafasi watu wengine wenye huduma hii.

                                                                        *HATUA ZA KUJUA KAMA WEWE NI MWALIMU*

*1 Ualimu ni kundi mojawapo katika utumishi wa neno la Mungu*

_Waefeso 4:11 Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na *waalimu;*_

*2 Nisababu zipi zilimfanya Mungu aweke makundi ya aina tofauti tofauti za watumishi wake*

>>Biblia iko wazi kabisa kuwa kila kitu ambacho Mungu amekiumba kinatenda kazi kwa namna yake, Pia kwa hata shetani nae huwa anaomba kumtumikia Mungu. Nenda kwenye biblia utaona wapi shetani alipoomba kumtumikia Mungu.

>>Kama Mungu anakuita na kukuweka  sehemu Fulani anakupa na sababu. Kwa hiyo nauliza swali *maana yako kama Mwalimu ni nini*

*Ualimu unakusaidia kufikia mahali  ndio maana* 

_Waefeso 4:11-16 Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, *hata* kazi ya huduma itendeke, *hata* mwili wa Kristo ujengwe; *hata* na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, *hata* kuwa mtu mkamilifu, *hata* kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu_. _Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo. Katika yeye mwili wote ukiungamanishwa na kushikanishwa kwa msaada wa kila kiungo, kwa kadiri ya utendaji wa kila sehemu moja moja, huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika upendo._

>>Katika Mistari hii tunaona sababu zifuatazo.

*a). KUWAKAMILISHA WATAKATIFU*

Neno *WATAKATIFU*  ni Zaidi ya kutokuwa na dhambi,  maana mtakatifu ni mtu aliyetengwa kwa kusudi la Mungu.

Sasa hapo nataka uone neno *hata* ziko tano.  Kumbuka maana ya hata ni mpaka au hadi, angalia tena hapo juu.

>>Ualimu ni miongoni mwa makundi matano ya kiutumishi ambayo Mungu kayaweka kwalengo *Kuwakamilisha watakatifu*

>>Sasa ukifuatiliakutoka kwenye zile hata au utaona

*a) Kazi ya huduma itendeke*

*b) Mwili wa Kristo ujengwe*

Kwa hiyo kuwa mwalimu ni ili uwasaidie wengine (wainjilisti, wachungaji.n.k) ili wasimame kwenye nafasi zao ili kwa pamoja msaidiane kujenga kazi ya Mungu.

*c) Umoja wa imani* 

Na kuna tofauti ya umoja wa Roho maana umoja wa Roho unakuja kwa kuokoka na kuna sababu zingine kwenye biblia.

>>Umoja wa Imani, tunajua kuwa imani huja kwa neno la Kristo, baada ya watu kupata ufahamu wa imani na msingi wa kuelewa maandiko yanayotuunganisha ili kuhakikisha neno haliwagawi watu bali linawaweka pamoja.

>> Tunafahamu kwa sehemu mambo ya Mungu na mwana wa Mungu, ile sehemu ninayomfahamu Mungu  inatakiwa itumie kutii neno na Mungu na kuwaunganisha wengine kwa pamoja.

*d) Hata kuwa wakamilifu*

*e) Kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; ili tusiwe tena watoto wachanga ili tufike  kwa yeye aliye kwa Kristo*.

>>Vitu hivyo vyote vimekaa kwa ajili ya makundi matano.
Mwalimu afanye kwa njia ya kufundisha

Mwinjilisti afanye kwa njia ya kuhubiri

Mchungaji afanye kwa njia ya kuchunga

Nabii nae hivyo kwa kutoa unabii

Mtume nae afanye kwa njia yake.

*3 Kuna vitu ambavyo Mungu anaweka ndani ya mtu vinavyoweka alama ya kujulisha ili kujua anamuweka katika kundi lipi la kiutumishi wake*.

_Kutoka 35: 30-34 Kisha Musa akawaambia wana wa Israeli, Angalieni, Bwana amemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila ya Yuda; naye amemjaza roho ya Mungu, katika hekima, na akili, na ujuzi, na kazi ya ustadi kila aina; na kuvumbua kazi za werevu, na kufanya kazi ya dhahabu, na fedha, na shaba, na kukata vito vya kutilia, na kuchora miti, atumike katika kazi za werevu kila aina. Naye amemtilia moyoni mwake ili *apate kufundisha*, yeye, na Oholiabu mwana wa Ahisamaki, wa kabila ya Dani._

>>Ina maana kuna vitu Mungu alimuwekea ndani ya moyo wake ili aweze kufundisha. Hivi ni vitu vilivyoko ndani ya mtu na sio vya kuiga. Maana kuna wengine hawajui kama kuiga ni kilema.  Hujawahi ona mtu anajifanya kilema na anakaa hadi kwenye wheelchair na unaona kuna hatari inakuja unaona ananyanyuka na kuanza kukimbia. Ndipo unaanza kushangaa kuwa huyu hakuwa kilema, bali unakuja gundua kuwa alikuwa anaiga.  Kuna wengine wanajipachika huduma na unajua huyu ni mwalimu kumbe sio yaani kaiga na amekuwa kilema, wacha kitokeze ndani chenyewe maana kama Mungu kakiweka ndani yako utakiona tu. Haijalishi uko wapi kitatoea tu maaana ni cha Mungu.

>>Utatambuaje kuwa wewe ni mwalimu, kuna vitu vimewekwa ndani yako ili kusukuma na kukupa kupenda kile kitu ambacho Mungu kakupa.  Kama Mungu kaweka kuwa nabii basi ujue atafanya kudhihirisha ndani yako kitu cha unabii, vivyo hivyo na kwa huduma zingine.

*NAMNA   VITU HIVI VINAVYOWEKWA NDANI YA MTU*

>>Kila mtu kuna vitu Mungu kamuwekea ndani yake,   ngoja nikuoneshe kidogo.

*1 Kufundisha ni Kipawa*

_Waefeso 4:7,11 Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha *kipawa* chake Kristo, Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu;_

*2 Ni neema*

_Waefeso 4:7 akini kila mmoja wetu alipewa *neema* kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo_
Kumbuka kuwa ukipewa kipawa ni lazima na neema iwe juu yako.  Kwa hiyo kufundisha ni neema

*3 Kufundisha ni karama*

_Warumi 12:4-6 Kwa kuwa kama vile katika mwili mmoja tuna viungo vingi, wala viungo vyote havitendi kazi moja; Vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake. Basi kwa kuwa tuna *karama zilizo mbalimbali*, *kwa kadiri ya neema mliyopewa*; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani;_

*4 Kufundisha ni Upako* (Mafuta ya Roho Mtakatifu)
_1 Yohana 2:27 *Nanyi, mafuta yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha*; lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha habari za mambo yote, tena ni kweli wala si uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani yake._

*5 Ualimu ni hazina*
_Mathayo 13:52 Akawaambia, Kwa sababu hiyo, kila mwandishi mwenye elimu ya ufalme wa mbinguni amefanana na mtu mwenye nyumba atoaye katika *hazina yake vitu vipya na vya kale*._

*6 Ualimu ni wito*

_Waefeso 4:1 Kwa hiyo nawasihi, mimi niliye mfungwa katika Bwana, mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa;_

>>Kwa hiyo katika yale makundi matano ya huduma, na katika ile Kutoka 35:34 tumeona namna Mungu alivyoweka vitu ndani ya Ohaliba ili aweze kufundisha.  Kwa hiyo hivyo vitu sita vilivyotajwa hapo juu ndivyo Mungu anavitumia katika kuweka vitu vyake ndani ya Mtu.

>>Kwa hiyo ni lazima ujue tofauti yake ni nini , kwenye tafsiri ya kawaida ina maana Mungu aligawa vipawa, kwa hiyo *Ualimu ni kipawa ndani ya kipawa*

>>Kwa kiingereza tungesema ni *gift* sasa kwenye Kiswahili ni *zawadi*, ualimu ni kipawa na imebeba kipawa, na. tambua kuwa kipawa ni ofisi. Kipawa cha ualimu kinakupa authority yaani mamlaka ya kufundisha

>> *Neema* Ukienda kuangalia katika maandiko Paulo anasema  _tena walipokwisha kuijua ile *neema niliyopewa*; Yakobo, na Kefa, na Yohana, wenye sifa kuwa ni nguzo, walinipa mimi na Barnaba mkono wa kuume wa shirika; ili sisi tuende kwa Mataifa, na wao waende kwa watu wa tohara;_*Wagalatia 2:9*

>>Kwa hiyo neema inakupa nafasi. Kwenye ualimu hatufanani kila mtu ana neema ya kwake na ni tofauti kati ya mwalimu wa kufundisha masomo ya awali na yule anayefundisha ya ngazi ya juu. Haina maana ya kuwa kuna kufundisha masomo ya chuo kikuu au kufundisha darasa la kwanza au kindergarten  wewe sio mwalimu hapana. Ili mwalimu wa chuo kikuu aweze kumfundisha mwanafunzi vizuri chuo inategemea msingi aliouweka mwalimu wa shule ya awali au darasa la kwanza. kwa hiyo wote ni wa muhimu mnoo.

>>Mama yangu alisomea ualimu na alikuwa anafundisha darasa la kwanza na la pili. Miaka yote alifundisha hapo na hadi alikuja kuwa mwalimu mkuu bado aliendelea kufundisha darasa la kwanza na la pili. Na watu waliopita mikononi mwake wanamkumbuka mpake leo maana kuna alama aliweka katika maisha yao na haiwezi futika. Haijalishi wewe katika neno la Mungu unafundisha katika ngazi ipi wewe ifanye kwa uaminifu na hakika alama utakayoiweka haitafutika.

>>ile wote mmejifunza physics na chemistry na wewe ukawa unafundisha form one na mwingine anafundisha chuo kikuu, haimanishi kuwa yule wa chuo kikuu ni bora sana kuliko yule mwalimu wa form one. Ila jua kuwa katika hii nafasi ya ualimu wote tunatenda kazi ya kuujenga mwili wa Kristo. Tunakwenda sawa sawa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

*4) Karama maana yake vitendea kazi ndani ya ofisi*

>>Kwa hiyo katika kufundisha pia kuna teaching aids, yaani kinachorahisisha kufundisha. Hata kwenye neno la Mungu kuna teaching aids(zana za kufundishia). Sasa kwa wale waliopita ile shule kama tuliyosoma sisi tulikuwa tuanenda *ndude*, ehehe mnazifahamu *ndude* yaani vile vizibo vya soda kule kwetu tunaita ndude. Sasa zile tulikuwa tunatumia kuhesabu ili kujua kuongeza na kutoa. Na ilikuwa inafanyika kwa vitendo ili tuweze kuelewa namna ya kuhesabu.  *Hata kwa Mungu kuna teaching aids yaani mfano na shuhuda* kazi yake ni kusaidia kuelewa.

>> sasa sio kila mtu atakuwa nacho hiki kitu cha kufundisha,ndio maana kuna mahali napenda sana kweye biblia inasema hawata ambizana kuwe mjue Bwana kwa maan watanijua wao. Jifunze na wewe watoto wako kumjua Bwana. Sasa upako alio nao Bonnke ni tofauti na Upako wa wewe mwinjilisti wa kijiji. Bonnke ni mwinjilisti wa Africa sasa upako ulio juu yake ni tofauti na ule utakao kuwa juu yako ewe ambaye ni mwinjilisti wa kijiji. Sasa unakuta uomba Mungu akupe upako kama wa Bonnke wakati wewe ni mwinjilisti wa kijiji. Na usiige omba Mungu akupe kwa kadri yako wewe na ile nafasi aliyokupangia.

>>Sasa niulize mimi ukitaka kuiga, unasimama kwa siku nane kila baada ya muda mchache kwa mwaka mzima, na unatakiwa kila siku ufundishe kitu kipya, upate na muda wa kuomba, kusoma na kuandika vitabu na kazi zingine. Sasa ndio maana nasema usiige maana huwezi jua mzigo aliobeba mtu. Na ukiwa na karama kama hii *haitakiwi ujivune maana hii ni neema Mungu kakupa*

*5) Mwalimu ni mtu ambaye ndani yake kuna elimu ya ufalme.*

>>Elimu inayooanisha mahitaji yaliyoko katika ufalme huu na ujao na sio mfumo huu wa elimu ya kawaida ya huku duniani bali ni elimu ya ufalme.  Hii elimu ya ufalme ya Mungu ina mfumo wa syllabus yake, sasa chukulia mtu anatumia mfumo wa duniani huku anatoa elimu ya mfumo wa kanisa lake badaya ile ya ufalme wa Mungu, ujue tu kuna mahali tutakanyagana kwa maana hatuendani sawa.

>>Ndio maana Yesu alikuwa anabishana na Mafarisayo juu ya elimu waliyokuwa wanaitoa ilikuwa tofauti na ile ya ufalme wa Mungu. Japo wote walisoma torati ile ile ila walikuwa wanazitazama kwa macho tofauti, Mafarisayo waliitazama kidini wakati Yesu aliitazama kwa mfumo wa ufalme wa mbinguni.

*6) Ualimu ni tabia*

Tabia hujidhihirisha katika mwenendo wako, ndio maana ualimu sio kipawa tu bali inageuka kuwa tabia, ndio maana utaona kwa mwalimu kuwa na tabia ya kuuliza maswali ni suala la kawaida kwa maana anataka kuelewa. Na ukiona hata mtoto nyumbani ni mdadisi na anakuwa na maswali mengi basi jua kuwa kuna kipawa cha ualimu ndani yake maana waalimu huwa wanahitaji uelewa.

*7 Cheki ndani yako je moyo wako unakupa kufundisha?*
>>Kufundisha ni kutoa maelekezo

>>Kufundisha ni kufahamisha (kutoa ufahamu)

>>Kufundisha ni kusahihisha, ndio maana mwalimu mzuri hutoa usahihi mahali watu wamekosea au hawajaelwa.

>>Kufundisha ni kujenga madaraja kitu Mungu anataka uweke.
Ndio maana kabla ya kula chakula kigumu unaanza kwanza kunywa maziwa ndipo unakuja kuanza kula chakula kigumu ukisha komaa.

.. Ndio maana kama kuna mahali mwalimu haelewi anataka kuuliza swali, kwa hiyo kama unafundisha usisikie vibaya watu wakikuuliza maswali na wewe unaanza kukemea kuwa sihitahi injili za maswali, ila jua kuwa maswali yanasaidia kuelewa.

>>Kufundisha ni kuadibisha (kumtolea Shetani mtu huyo, ili mwili uadhibiwe, ili na roho iokolewe katika siku ya Bwana Yesu.) 1 Wakorintho 5;5

Kwa hiyo kama wewe unamheshimu Mungu  lazima utahitaji sana Mungu apate heshima anayostahili kuliko mapokeo ya dini yako, na endapo utaona kuna kitu kinaenda tofauti ni lazima tu utasikia vibaya.

>>Katika kulea huduma yako ya ualimu, cheki kwanza nae kulea ana huduma gani, chukulia wewe ni mwalimu unalelewa na mwinjilist si unajua lazima atakuwa anakuonesha vitu vya kuinjilisti Zaidi unakuta na wewe unaanza kuwa mwinjilist lakini huduma hiyo siyo ambayo Mungu alikupangia. Sasa hapo unakuwa unaoa huduma yako. Omba Roho Mtakatifu akusaidie ili upate watu sahihi wa kulea huduma yako. 

>>Pia ukiwa mwalimu lazima *usome sana vitabu mbali mbali kwa msaada wa Roho Mtakatifu ili uweze kuelewa vitu mbali mbali. Hivyo ni muhimu ulewe na kanuni ya kuwa mwalimu bora ni lazima uhakikishe kile kitu unachokifundisha na wewe unakiapply na ndio maana biblia inasema*

*_Jitunze nafsi yako, na mafundisho yako. Dumu katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo utajiokoa nafsi yako na wale wakusikiao pia._1 Timotheo 4:16*

>>Siku nyingine kutakuwa na sehemu ya Maswali, darasa hili litakuwa ni endelevu na tutalifanya si kila mkoa ila pale Mungu atakapotupa nafasi. Zidi kuliweka katika maombi.

*Naamini sasa umeanza kujitambua kuwe wewe ni mwalimu au sio mwalimu. Baada ya hapo jiweke wakfu kwa Bwana ili akusaidie katika huduma hii. Ubarikiwe mnoo*.

✍✍✍✍✍✍✍✍✍
🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏.

Ijumaa, 10 Machi 2017

USHIRIKA NA SANAMU NI KUIABUDU SANAMU

USHIRIKA NA SANAMU NI KUIABUDU SANAMU.

BWANA YESU apewe sifa ndugu yangu.
Karibu tujifunze jambo la kutuvusha kutoka kwenye giza.

1 Kor 10:14 ‘’ Kwa ajili ya hayo, wapenzi wangu, ikimbieni ibada ya sanamu. ‘’

Ujumbe wa MUNGU unakuonya kwamba uikimbie ibada ya sanamu maana yake ondoka kwenye Kanisa au dini wanaoabudu sanamu na Biblia inakushauri vizuri kwamba ingia katika Nuru ya ajabu ya BWANA YESU.

1 Petro 2:9-10 Biblia inasema ‘’ Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya MUNGU, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika NURU YAKE YA AJABU; ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la MUNGU; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema. ‘’

-Watu hawa walioingia kwenye nuru ya MUNGU ya ajabu ni watu wa kitofauti sana, hawafuata tu taratibu kisa taratibu hizo zilikuwepo kwa miaka mingi.
-Wakristo hawa wametengwa mbali na dunia.
-Wanajitambua na wako mbali kabisa na machukizo, -wanamtii MUNGU katika utakatifu wake.

Ndugu zangu, Kama unataka kumpendeza MUNGU hakikisha unamtii MUNGU.

Yako mambo mengi sana ya kumtii MUNGU lakini leo nazungumzia ubaya wa sanamu. 1 Thesalonike 1:9 ‘’ Kwa kuwa wao wenyewe wanatangaza habari zetu, jinsi kulivyokuwa kuingia kwetu kwenu; na jinsi mlivyomgeukia MUNGU mkaziacha sanamu, ili kumtumikia MUNGU aliye hai, wa kweli; ‘’

-Ndugu, kumbe MUNGU wa kweli haabudiwi kwa kuchanganya na sanamu.

Ndugu zangu vitu vingi ambavyo tunadhani ni vitu vizuri na vitakatifu kwa macho yetu, hivyo ni vibaya sana na ukikaa rohoni unaweza kugundua jambo hilo, Mwaka 2012 nilipita mtaa Fulani na kukutana na kijana mmoja anayeuza yale makaratasi makubwa magumu yenye ujumbe wa MUNGU na picha kubwa za Yule wanaodhani wanadamu kwamba ni YESU na Mariamu, sikuipenda picha ile ila nilipenda andiko ambalo lilikuwa limeandikwa kwenye karatasi hiyo, nilinunua na kwenda kubandika chumbani kwangu, ilikuwa ni picha kubwa sana ikiwa na andiko ambalo ndilo hasa mimi nililipenda. Baada ya muda nilianza kuona ugumu Fulani katika maombi, sikujua kwamba tatizo lilikuwa ni nini, usiku niliona katika maono kwamba lile karatasi ni antenna ya kuzimu ili kuona kila ninalofanya. Nilishtuka sana na kuomba kwa juhudi, kesho yake nililitoa lile karatasi lenye picha ya sanamu na tangu siku hiyo nikajifunza jambo jipya. Ndugu zangu haina maana kila karatasi yenye picha ya Mariamu au Yusufu ni mbaya ila kumbuka shetani hutaka kujipenyeza kwenye kila eneo ili tu akupate wewe mteule wa MUNGU.

Kuisujudia sanamu na kuitumikia ni kujiunganisha nayo, Hosea 4:17 -19‘’ Efraimu amejiungamanisha na sanamu; mwache. Kileo chao kimegeuka kuwa uchungu; huzini daima; wakuu wake hupenda aibu. Upepo umemfunikiza kwa mbawa zake; nao watatahayarika kwa sababu ya dhabihu zao. ‘’.

Ndugu Efraimu wa leo ni wewe mwabudu sanamu na unayesujudia sanamu, ni machukizo na kuna adhabu usipotubia na kubadilika.

Dada mmoja alishuhudia kwamba kasanamu ka mariamu kalikokuwa nyumbani kwao alikuwa anakaona usiku kakigeuka nyoka na kuanza kutembea, kasanamu hako walikatoa kanisani, ndugu, MUNGU anapokataza sanamu ni kwa kukusaidia wewe maana macho yako ya kibinadamu hayaoni. Dada mmoja aliota ndoto akiwa anapiga picha na majoka, aliumia sana na akanishirikisha ili ajue maana ya ndoto hiyo, nilipata ufunuo katika hilo, kumbe kila wakipiga picha huwa wanazi-edit kwa picha zao kuweka ndani ya picha nyingine ambazo zimetengeneza huko Ulaya, picha ile nzuri kumbe wala sio picha ya kawaida ni majini. Sasa Yule dada alipoona anapiga picha na majoka na kuogopa kumbe ni kwa picha yake kuunganisha na picha mbaya ambao wemeitoa kwenye internet. Hata wateule wengine mimi binafsi huwa nawashangaa sana, utakuta mtu kaweka picha anayodai ni ya YESU na kukulazimisha uandike amen ili ubarikiwe. Hakuna Baraka za hivyo ndugu yangu, na usiamnini kila picha zingine zimetengeneza na kuzimu kabisa hata kama zinavutia kiasi gani. Hii mifano yote ni picha tu na visanamu vidogo lakini vina madhara makubwa sasa sanamu ni zaidi.

Watu wa zamani waliangushwa sana na kujihisisha na sanamu lakini kanisa la leo hata hatujifunzi kwako.

Waisraeli waliabudu sanamu ya ndama jangwani na ndio maana wengi sana MUNGU aliwaangamiza huko huko jangwani, hata hatujifunzi kwao.

MUNGU anasema kwamba heshima yake wala sifa zake hatawapa sanamu.

Isaya 42:8 ‘’ Mimi ni BWANA; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu. ‘’

Ndugu zangu, jambo la muhimu naomba mtambue kwamba MUNGU hana mwakilishi katika vitu vyote duniani. MUNGU hutumia neno lake kama mwakilishi wa matakwa yake. Neno la MUNGU husomwa na kufafanuliwa na wanadamu waaminifu wakielekezwa na ROHO MTAKATIFU. Hakuna zaidi ya hapo. Sanamu haimwakilishi MUNGU kwa vyovyote vile.

-MUNGU hatawapa sanamu heshima yake.
-BWANA hatawapa sanamu sifa zake.
-MUNGU wa kweli haambatani na sanamu kwa namna yeyote ile.
-Sanamu ni mungu wa kutengeneza na wanadamu, wala sanamu hazihusiki na MUNGU aliye hai.
-Ukitumia sanamu katika mazingira yeyote ya ibada unamkosea MUNGU aliye hai.

Kuna watu hutumia sanamu za Bikra Mariamu na watakatifu wengine wa zamani kwa kuzibusu kwa heshima na kuomba kwa kutumia hizo, Ndugu yangu unayefanya hivyo tambua neno hili ya kwamba unafanya machukizo makuu.

-Kuna watu husujudia sanamu, ni makosa makubwa sana.

Kusujudia sanamu ni kumsujudia shetani(Ufunuo 13:12 ‘’ Naye atumia uwezo wote wa mnyama yule wa kwanza mbele yake. Naye aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona. ‘’)

Mtume Yohana kwa hofu alitaka kumsujudia Malaika, Malaika alimkataza na kumwambia Yohana kwamba wa kusujudiwa ni MUNGU pekee(Ufunuo 22:8-9), MUNGU wa pekee ni MUNGU katika utatu mtakatifu ndio maana BWANA YESU katika maandiko mengi alisujudiwa na hata mbinguni malaika wote humsujudia(Ufunuo 5:8-14, Ufunuo 7:9-12).

-Ndugu yangu, MUNGU BABA amekataza kusujudia sanamu wala kuitumikia, Kumb 5:8-9 ‘’ Usijifanyie sanamu ya kuchonga, mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, au kilicho chini duniani, au kilicho majini chini ya nchi. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi BWANA, MUNGU wako, ni MUNGU mwenye wivu, nawapatiliza wana uovu wa baba zao; hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, ‘’

Kutokana na neno la MUNGU hapo kuna mambo 3 kuhusu sanamu ambayo mwanadamu hatakiwi kuyafanya.

1. Usitengeneze sanamu ya mfano wa kitu chochote kiwe mbinguni, duniani wala kuzimu.

-Hivyo wanaotengeneza sanamu na wewe unaitumia wote wawili mmepotoka.
-Yawezekana wewe hujatengeneza lakini hata kutumia tu katika Ibada ni dhambi.

2. Usisujudie sanamu.

-Wengi wanasujudia sanamu, ni dhambi.
-Wengi wanajishughilisha na sanamu, ni makosa.

-Wengi hudhani kuna uwepo wa MUNGU wakiwa karibu na Sanamu, kumbe kuna uwepo wa shetani, ni dhambi ndugu.

3. Usiitumikie sanamu.

-Maelfu ya watu wanazitumikia sanamu, ni dhambi.
-Watu wengi hutumia sanamu katika ibada zao, ni dhambi.
-Hata kuweka masanamu kanisani kutawasababisha kanisa lenu liwe la kimwili badala ya kuwa la kiroho.
-Kanisa lenu likijaa masanamu, huo ni mlango wa shetani kuwa sehemu ya ibada yenu, ni dhambi.

Makampuni mengi yanatengeneza sanamu za wale ambao majina yao yamo ndani ya Biblia ili tu kuwakosesha watu wengi ambao huzitumi asanamu hizo katika ibada.

MUNGU hataki wewe ndugu uhusike na sanamu katika mazingira yako yoyote ya kiteule. Unadhani kwanini sanamu zimejaaa zaidi makanisani? Ni kwa sababu shetani anawatafuta zaidi watu wa kanisa maana hao wakipata akili ya kuzichoma sanamu hizo watakuwa ni kama wamechoma macho yake ya kuwaona watu wa kanisani. Sanamu zile ni mpango wa shetani kuhakikisha mwanadamu hafiki uzima wa milele.

-Kuna watu ukikemea sanamu wanadhani unaanza kuwavuta watu wahame kanisa lao, lakini ndugu kama kanisa lako lina masanamu hakika ni heri kuhama maana nyie kunena kwa Lugha mtakuwa tu mnakusoma kweli Biblia nyie hakuwahusu.
-Kuombea mtu mapepo yakamtoka mtakuwa tu mnaona kwenye TV na kudhani kwamba hao mnaowaona wanatumia nguvu za giza kumbe ni mamlaka ya MUNGU aliye hai.
-Mkiwa na masanamu kanisani kwenu, Nguvu za MUNGU aliye hai mtakuwa tu mnazisikia redioni.
-Mkiwa na masanamu kanisani Karama za ROHO MTAKATIFU mtakuwa tu mnaziona kwenye TV.

MUNGU anachukizwa na sanamu. Na kibaya zaidi ambacho MUNGU hataki ni kanisa lenu kufuata ratiba ya kanisa la Ulaya, hivyi kanisa la Ulaya likianguka dhambini na nyie lazima tu mtaanguka maana mnawafuata wao, kanisa la Marekani wakitekwa na shetani na kuchapicha kitu kibaya na nyie tu kitawanajisi maana nyie mnawafuata hao kwa kila kitu. Ndio maana Biblia inasema Tuongozwe na ROHO MTAKATIFU na sio kanisa Fulani. Wagalatia 5:18-21 ‘’ Lakini mkiongozwa na ROHO, hampo chini ya sheria. Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa MUNGU. ‘’

Biblia inatutaka tusijiunganishe na sanamu, tena tujilinde na sanamu, yaani tuziepuke sanamu ,1 Yohana 5:21 ‘’ Watoto wadogo, jilindeni nafsi zenu na sanamu. ‘’

Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.