Jumanne, 28 Februari 2017

KAZI ya MTU hupimwa mwishoni siyo mwanzoni

BWANA YESU APEWE SIFA SANA SANA

KAZI YA MTU ALIYOPEWA NA MUNGU UPIMWA MWISHONI SIO MWANZONI NA KUPEWA MALIPO

KUTOKA 39:32-43

Mungu uwa anapima kazi aliyokupa kuifanya kuhanzia mwishoni yaan pale ulipomalizia ndio hapo Yeye uwa anahesabu kuwa umefanikiwa kuifanya ,mwisho wa kumalizia kazi aliyokupa n bora kuliko mwanzo wako

👉Alafu mtu anapo maliza kuifanya Mungu uhanza kutazama je amefanikiwa kuifanya kama moyo wake ulivyotaka ,haijalishi n kazi gan nzuri umeifanya dunia lakin kama aiendani na kusudi lake LA moyon mwake hapo ujue Mungu atakukataa wewe pamoja na ulichokifanya

👉Msisitizo wa Mungu sio kufanya huduma tu Bali je umefanya sawa sawa na mapenzi yake yaan moyo wake unavyotaka au la

👉Bwana Mungu akaniambia "ivi siku ya kubagua watu yaan kutenga kondoo na mbuzi inakaribia sana wengi wataniambia kuwa Bwana je hatukufanya miujiza na kutoa pepo kwa jina lako naye atawaambia ondoken nyie watenda maovu ,sikuwajuha kamwe , niliposikia hayo maneno nilijiuliza moyoni nkasema Baba Naomba unipe siri ya kuwakataa wale waliofanya matendo na huduma kwa jina lako na ukawakataa mwishoni ndipo kama vile alijuha swali langu moyoni mwangu akanijibu ivi akasema "Ni matendo yao ,matendo ndio yatawafanya niwakatae siku ile " Matendo yao yalikuwa kinyume na YESU wao kwaiyo YESU kumbe hatazami tuu ufanyaji wako wa kazi bali  anatazama je unaenenda sawa sawa na mapenzi yake ,je kile unachofanya kimebeba kusudi la Mungu wako

Ukisoma mstari 43-42👉Unaona kuwa walipata heri au baraka mwisho kwa sababu walifanya vile vile kama Mungu alivyo mwagiza Musa na ndipo neno heri au baraka likatoka juu yao
Msisitizo wa Mungu n kufanya kazi au huduma ya Mungu wako sawa sawa na mapenzi yake

Mungu atusaidie tusije kuwa mbuzi badala ya kondoo ,tutakapo ufikia mwisho wetu

Ule mwisho nao unasogea sana sana

BWANA YESU KARIBU ANAKUJA TUKAE MACHO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni