Jumanne, 28 Februari 2017

Ufalme wa Mungu umekaribia.

Ni jambo jema kuwaambia watu kuwa ufalme wa Mungu umekaribia, kulingana na maelezo ya YESU.
HABARI za ufalme wa Mungu ni njema, Ila sharti lake huambatana na
Marko 16
15 Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.
16 Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.
Usipoamini bado huwezi kuwa na tumaini la kuingia katika ufalme wa MUNGU (MBINGUNI)
Na unapoamini inatakiwa UBATIZWE, ILI KUZIKA DHAMBI NA UTU WA KALE, NA HIVYO KUWA KIUMBE KIPYA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO.
Marko : Mlango 1
15 akisema, Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili.
Ukishaamini na kubatizwa, uksachana na dhambi, endapo ukitenda dhambi inatakiwa Utubu upesi ili uirudie hali ya kukubarika mbele za Mungu muumba MBINGU na dunia na vyote vilivyomo.
YESU ASISITIZA JUU YA KUBATIZWA (KUZALIWA MARA YA PILI)
YOHANA  Mlango 3
1 Basi palikuwa na mtu mmoja wa Mafarisayo, jina lake Nikodemo, mkuu wa Wayahudi.
2 Huyo alimjia usiku, akamwambia, Rabi, twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezaye kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, isipokuwa Mungu yu pamoja naye.
3 Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.
4 Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?
5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.
6 Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.
7 Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili.
8 Upepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho.
NI wajibu wako kutii maagizi ya YESU KUHUSU INJILI.
Natumai umejifunza kitu, usiwe na roho ngumu naomba utubu, uiamini Injili na kutenda Sawa saw a na MAPENZI YA MUNGU, HAKIKA HUTAJUTA.
Mungu akubariki, pia akujalie kuijua INJILI IOKOAYO SIKU ZOTE,
                                       AMINA.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni