Jumanne, 28 Februari 2017

MAMLAKA YA YESU

Ndugu msomaji karibu katika blog hii ujifunze, Mungu akusaidie use na moyo wa kujifunza Neno lake na uuishi wokovu.




Kuna swala ambalo watu wengi hudhani kuwa ni LA kawaida japokuwa in zito mno KWA MWENYE kutaka ufalme wa mbinguni.



Mada iliyopo hapa inahusu maagizo ya Yesu na Mamlaka take.


Mathayo 28

16 Na wale wanafunzi kumi na mmoja wakaenda Galilaya mpaka mlima ule aliowaagiza Yesu.

17 Nao walipomwona, walimsujudia; lakini baadhi yao waliona shaka.


18 Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.


19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;


20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.




Baada ya Yesu kufufuka aliwaagiza wanafunzi wake wale kumi na moja  (11) 
Na walipomwona baadhi yao waliona shaka Ila aliwaambia waamini.

Ndipo alipo waambia kuwa AMEPEWA MAMLAKA YOTE MBINGUNI NA DUNIANI,

Hivyo wanafunzi waendr Duniani waihubiri Injili na kila aamini abatizwe na kufundishwa kufundishwa kuyashika yote aliyoagiza. Kama mkristo/mwanafunzi wa Yesu in wajibu wako baada ya kuijua kweli pia nawe uihubiri KWA wengine nao waijue waepukane na uovu katika dunia hii, mwisho wa yote WAURITHI UFALME WA MUNGU (MBINGUNI).


FANYA HIMA mpendwa uhubiri KWA wengine nao waijue kweli ya INJILI KUWA BAADA YA KUIAMINI NA KUTENDA SAWA NA MAAGIZO YA YESU WATAINGIA MBINGUNI kiyama ikifika.


Katika kumhubiri huyu Mwokozi wetu YESU KRISTO kaa ukijua kuwa makwazo hayana budi kuja, ila avumiliaye mpaka mwisho ataurithi UZIMA WA MILELE (Mathayo 5:10-12).


Namshukuru MUNGU KWA ujumbe huu nikitumai kuwa utakuinua kiroho na kimwili.

Usiogope YESU yuko nawe hata ukamilifu wa dahari, yaani nyakati zote atakuwa nawe, Hubiri usiogope YESU ANAKUPENDA, ANAKULINDA & ANAKUFADHILI .  

MUNGU akubariki




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni