✨1⃣ *SEMINA YA NENO LA MUNGU DAR ES SALAAM TANGANYIKA PACKERS*
*HALI YA KIROHO YA ARDHI INAVYOHUSIKA NANKUFUNGWA AU KUFUNGULIWA KWA MAFANIKIO YAKO*
*MWL MWAKASEGE*
*DAY 1: 5 MARCH 2017*
Semina hii italenga maeneo ya ardhi maalumu ya muhimu yanayohusika kufunga watu namna ya kuwafungulia.
*LENGO: KUHAKIKISHA MAFANIKIO YAKO YALIYOFUNGWA KATIKA ARDHI YANAFUNGULIWA*.
*1* *KUFUNGUA MAFANIKIO YAKO YALIYOFUNGWA NA HALI YA KIROHO YA ARDHI INAYOFANYA HALI YA MAHALI UNAPOSIHI PAWE NYUMBA YA UTUMWA*.
_Kumbukumbu la Torati 6 : 12 ndipo ujitunze, usije ukamsahau Bwana aliyekutoa nchi ya Misri, nyumba ya utumwa._ Kufuatana na 2 Nyakati 7:14 ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, *na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao*. Nchi maana yake ni ardhi yenye mipaka halali ya kiumiliki
>>Hapa anazungumzia nchi na sio taifa.. maana taifa linahusisha mkusanyiko wa watu walio katika uongozi wa waliokubaliana.Taifa nalo lina mlololongo wake. Katika biblia kuna taifa.. jamaa kabisa.. jamaa na lugha. Taifa linaweza kuwepo lakini halipo katika nchi yake.. biblia inasema _Au Mungu amekwenda wakati gani akajitwalia taifa toka kati ya taifa lingine, kwa majaribu, na kwa ishara, na kwa maajabu, na kwa vita, na kwa mkono hodari, na kwa mkono ulionyoshwa, na kwa maogofya makuu, kama vile Bwana, Mungu wenu, alivyowatendea ninyi katika Misri, mbele ya macho yenu? Kumbu 4:34_ . Israel walikuwa taifa lakini walikuwa katika nchi ya Misri.
Wakati unasoma jua namna ya kutofautisha kati ya nchi na taifa, na nilipoanza kulitazama hili suala la ardhi lilinipa kujua mambo mengi sana. Nilipoanza kufundisha hali ya ardhi katika mkoa mmoja.. watu walianza kuzunguka na kusema Mwakasege kapata wapi hiki kitu.. watu wa kule waliniambia na niliwaambia muwe na amani.. maana hili neno ni la Mungu. Maana si wengi wanajua kuwa haya mambo ninayoongea yapo kwenye biblia.
Huwa nafundisha waalimu kuwa kabla ya kufundisha hilo neno liweke kwenye matendo kwanza wewe mwenyewe maana yake fundisha kwa shuhuda na hapa tutafanya maombi hapa ili mpate kuona. Ukiona nakufundisha masomo haya ujue mimi mwenyewe nimeyaweka kwenye matendo na ndio nimeona matokeo yake na ndipo nakuja kukufundisha kitu halisi ninanchokijua.
*2.UKILINGANISHA 2 NYAKATI 7:14 NA KUMB 6.12 UTAONA YA KUWA HALI YA KIROHO YA ARDHI INAWEZA GEUZA ENEO KUWA NYUMBA YA UTUMWA.*
Kumbukumbu la Torati 6 :12 ndipo ujitunze, usije ukamsahau Bwana aliyekutoa nchi ya Misri, *nyumba ya utumwa*
Nchi ni ardhi yenye mipaka halali na nchi hapa kwa mujibu wa kumbu 6:12.. *nchi ya misri nyumba ya utumwa* kwa hiyo ardhi ya Misri imefanyika nyumba ya utumwa.Ardhi ina uwezo wa kufanya eneo kuwa nyumba ya utumwa.. tunaenda sawa sawa?Ukitazama kiroho utaona kiupana ardhi maana hamna nchi iliyojengwa kama nyumba lakini Mungu anaita nchi ya Misri nyumba ya utumwa.
*3.UTUMWA WA WANA WA ISREAEL ULIKUWA WA KIROHO LAKINO ULIJITOKEZA KATIKA MAISHA YAO YA KILA SIKU*
Hapa kuna sababu 3
*I) Shida haikuwa kazi.. bali mazingira ya kiroho ya kazi waliyokuwa wanafanya hiyo kazi*
_Kutoka 1 :11-14 Basi wakaweka wasimamizi juu yao wawatese kwa mizigo yao. Nao wakamjengea Farao miji ya kuwekea akiba, Pithomu na Ramesesi. 12 Lakini kwa kadiri ya walivyowatesa ndivyo walivyoongezeka na kuzidi kuenea. Nao walichukiwa kwa sababu ya wana wa Israeli. 13 Wamisri wakawatumikisha wana wa Israeli kwa ukali; 14 wakafanya maisha yao kuwa uchungu kwa kazi ngumu; kazi ya chokaa na ya matofali, na kila namna ya kazi ya mashamba; kwa kazi zao zote walizowatumikisha kwa ukali._
Tuangalie kazi walizokuwa wanafanya maana kazi zile walizofanya wakiwa Misri ndizo hata Kanani walifanya maana walikuwa wanajenga miji ya akiba na majumba. Biblia inasema wakifanya kazi ngumu, sasa hapa nataka uelewe si kila kazi ngumu ni utumwa. Maana maeneo yote kama ni kushughukika na chokaa na ujenzi kote walifanya (Kanani na Misiri) sasa tatizo lilkuwa ni mazingira ya kiroho.
Hata walipomlilia Mungu kwa sababu ya Utumwa. _Kutoka 2 :23 Hata baada ya siku zile nyingi mfalme wa Misri akafa; wana wa Israeli wakaugua kwa sababu ya ule utumwa, wakalia; kilio chao kikafika juu kwa Mungu kwa sababu ya ule utumwa._
Utumwa si kazi bali ni mazingira ya kiroho yanayitengeneza hali ya kimaisha, na yanabana fikra na kuweka mipaka namna Ya kufanya kazi. Na si wengi wanajua hili. Utasema kwanini kwa sababu
*2. WALISHINDWA KUJITOA*.
Maana ingekuwa ni kazi wangeacha.. ni sawa na mtu analalamika kuwa kazi ngumu na bado yuko kazini nalalamika weeee lakini kazi haachi .. sasa si utoke utafute nyepesi, kuna maana gani kulalamika na kuendelea kubaki mazingira yale yale.
Unaweza ukawa mtumwa katika mazingira ya nyumbani na ni tofauti na mazingira ya gereza maana mazingira ya nyumbani yanadanganya lakini bado utumwa ni utumwa haijalishi uko gerezani au nyumbani.
Katika mazingira ya kawaida hawakujua kama wako utumwani.. kama Mungu asingewatangazia kuwa watumwa wasingejua. Maana walipoanza kulia Mungu aliwaondolea utumwa na hakushughulika na uchungu bali alishughulika na utumwa..Mzee Yakobo alikufa walimzika Kanani na hamna mtu alibaki kule waliacha kaburi tu. Na wote walirudi Misri, hawakujua kwanini wanarudi Misri, sababu ilikuwa ni ya kiroho zaidi.
*3.ILIBIDI MUNGU AWATOE KWA NGUVU*
Kumbukumbu la Torati 7 :8 bali kwa sababu Bwana anawapenda, na kwa sababu alitaka kuutimiza kiapo chake alichowaapia baba zenu, ndiyo sababu Bwana akawatoa kwa mkono wa nguvu, akawakomboa katika nyumba ya utumwa, katika mkono wa Farao, mfalme wa Misri. Sio swala la kazi bali yalikuwa ni mazingira ya kiroho. Na ilikuwa kazi ya kulima, au kutengeneza matofali lakini ilikuwa ni kazi ya utumwa..
Japo walikuwa wanalima lakini walikuwa wanaona uchungu.. na hawakujua nini kimewabana.. maana kama kazi ingekuwa utumwa basi kila mtu asingetafuta kazi. Maana kuna baadhi ya wapendwa hawataki kufanya kazi na wanaaza kuhalalisha kwa kutumia mistari ya biblia na kusema kuwa utaishi kwa imani lakini Biblia inasema asitefanya kazi na asile
*4. WAISHIO NDANI YA NYUMBA WANATAMBULIWA KIROHO KWA KUANGALIA JINA LA MMILIKI WA NYUMBA HIYO.*
_Esta 8 :1-2 1 Siku ile mfalme Ahasuero alimpa malkia Esta nyumba yake Hamani, yule adui ya Wayahudi. Mordekai naye akahudhuria mbele ya mfalme; kwa maana Esta alikuwa amedhihirisha alivyomhusu. 2 Basi mfalme akaivua pete yake, aliyompokonya Hamani, akampa Mordekai. Naye Esta akamweka Mordekai kuwa juu ya mlango wake Hamani._
>>Ukisoma ile sura _Esta 7 :10 Basi wakamtundika Hamani juu ya mti aliomwekea tayari Mordekai. Ghadhabu ya mfalme ikatulia._
Sasa ubganisha na Esta 8:1.. Ester alipewa nyumba ya hamani.. Nyumba katika ngazi ya kiroho inatazamwa tofauti sana.
Naanza kueleza Kumb 6:12 ndipo ujitunze, usije ukamsahau Bwana aliyekutoa nchi ya Misri, *nyumba ya utumwa* Ondoa misri weka utumwa.. hajailishi uko wapi kama wewe ni Mmsiri watakujua kuwa wewe ni mtumwa hata kama uko usa au china.
Na walipokuwa wanabishana juu ya kuteliwa kwa Haruni kuwa Kuhani wa Mungu, Mungu alisema walete fimbo kwa ajili ya nyumba moja.. maana kila familia wana ID (Utambulisho) . Haruni hakuhitaji kuleta fimbo ya watoto wake, maana fimbo moja tu ilitosha kutambulisha familia yake.
Nyumba ya Yakobo wana kitambulisho kinacho fanana. Kwa hiyo ukisema nyumba ya Yakobo haijalishi wako wapi ila wanatambulika kama ni watoto wa Yakobo. HAMANI alipokufa alikuwa na alama na alipokufa Hamani Ester ndiye alipewa mamlaka (yaani adui ndio alipewa madaraka) .. haijalishi wanajipanga kiasi gani kurithi lakini Ester ndiye msimamizi mkuu wa nyumba yao yaani ndiye mwenye sauti. .
Ile Pete ya Hamani alipewa modekai na alipewa na mamlaka kwenye lango.. na nyumba ile ya Hamani waliobaki wote waliuwa. Haijalishi hawako nyumbani lakini wako marked kiroho kuwa ni wa nyumba ya Hamani .. haijalishi wayahudi wako wapi.. walikuwa marked..
Nyumba ya baba yako kama wamepewa adui zako utapa shida sana.. maana biblia inasema uzao wako utamiliki malango ya adui
_Mathayo 12 :29 Ama awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? Ndipo atakapoiteka nyumba yake._
Maana yake nani anayemiliki nyumba na uzao wako.. huwezi wafungua waliofungwa kama hauna nguvu ya kumshika yule aliyewashika au wafungwa
*5.MUNGU ALIWATOA WANA WA ISRAEL KUTOkA KATIKA NYUMBA YA UTUMWA KWA KUPITIA KWENYE MALANGO WA NYUMBA YA UTUMWA*
_Mathayo 12 :29 Ama awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? Ndipo atakapoiteka nyumba yake._
Alitumia damu ya agano na nchi ya misri kipindi kile ilikuwa ina mazingira ya kitumwa na Mungu alifuata uzao wa Ibarahim na alienda kuwatoa kwa sababu ya agano.. walikuwa na alama za kiagano, japo walikaa maiaka 400 na utumwani na walikuwa hawasogei kimaisha lakini Mungu aliwatoa.
Je Mafanikio yako hayasogei kwa kuwa uko nyumba ya Misri ya utumwa nayo imekufunga?
Hata kama ni kwenu ardhi yenu imekuwa nyumba ya utumwa utapata shida sana. Ndio maana utaona Kijana ana akili lakini yuko nyumbani, muda wote anazubaa tu nyumbani, na hatafuti hata kazi yupo yupo tu , na unashangaa watoto wa jirani wanasogea ila wako wamekwama kabisa..
Wewe unafikiri ni sawasawa hapa kumbe katika ukoo mna alama ya kuwa ni watumwa, yaani mmefungwa na ndio maana hamsogei na kama mna agano na Mungu na shetani hata waaachia kirahisi rahisi
Maana unalima kama watu wengine, lakini wako utumwani Wana wa Israel hawakujua na ndio maana waliona uchungu wakati wanafanya kazi, kumbe sababu ya mazingira ya kiroho..
Hata wale wasimamizi walikuwa wanasimamia kwa sababu ya mazingira ya kiroho na waliwatesa sana wana wa Isarel, ndio maana utaona Mtu anahama nyumba kutoka nyumba ya kupanga kwenda kwenye nyumba yake unakuta hata kazi anachaaaza na anakuwa mvivu
Watu wengi hawajui kwanini Mungu aliwapitiasha wana wa Israel langoni katika nyimba na hawajui kwanini. Na alitumia malango na alitunia damu ya Pasaka waliyopaka katika malango. Watu wako hapa wafungwa asipate kazi.. na hata nyumbani kwake hatoki na kakwama hapo yaani kafungwa kabisa
Wengine wamefungwa kwa kitu cha imani na wapo wapo na asilimia kubwa sana ni vijana wa kiume hawafanyi kazi na wanafika muda wa kuona lakini ukiwauliza kazi hawana majib u wanasema katika mlima wa Bwana inapatikana, msichana anakuuliza hivyo anajua kuwa huyu kijana hajajioanga bado. Sasa ili kukuheshimu anatesema ngoja nikaliombeee kumbe kakuheshimu tuu na hataki kukuabisha.
Kuna kitu cha imani kimepita mahali na kina shida. Ukiwaukiza wako wapi watakueleza jina la nyumba ya baba yao. Yesu anasema kanisa ni nyumba alama ya kiroho kanisa inategemea jina la kanisa.. na wengine ukiwauliza unasali wapi watakupa jina la Mtumishi na badala jina la kanisa..
Na ina maana ni alama.. ukisema mimi ni mlutheri ina maana una alama au mpetekoste inaonesha alama yao . Lakini akikuambia jina la mtumishi ina maana alama aliyoweka mtumishi ni kubwa (sina shida au ni vibaya ila nakufundisha tu namna ya kutafsiri haya mambo kiroho kwanza. Pia mwingine ukimuuliza jina la mchungaji wako ni nani unakuta hata hajui, ina maana kuan shida mahali mpaka umesahau jina la mchungaji wako. Kwa sababu umeshindwa kukaa chini ya mchungaji na ndio maana unasahau na jina lake .
Ardhi ni kama computer kubwa, nikakanyaga hapa ardhi inajua huyu mtu ni nani.. Ardhi ya kule nilikozaliwa inaleta ripoti na ile ya kule ninakoishi nayo inaleta report kwa maana ardhi inatunza kumbukumbu na ndio maana Ukikataliwa mjini utakataliwa na mashambani..
Yesu anapitisha kondoo langoni.. na sio dirishani.. , na ndio maana na wewe uli utoke inabidi upite mlangoni maana wanaopita dirishani ni wezi , sasa naenda kufanya maombi hapa naunganisha ardhi ya hapa na ya huko kwako popote ulipo unapotufuatilia. Weka mikono yako katika magoti yako .
Akani alipokorofisha ardhi ilimeza wote wa nyumbani mwake, sasa chukulia mmoja hayupo na kawaida ardhi inaambiana ina maana nae kule kule alikokuwa nae alimezwa . ndio maana utakuta ardhi ya kwenu umewafunga na wewe uko mbali na kwenu lakini utaona pale wenzio wanapochanua wewe unachakae.