Jumanne, 7 Machi 2017

HALI YA KIROHO YA ARHI INAYOHUSIKA NA KUFUNGWA AU KUFUNGULIWA KWA MAFANIKIO YAKO sehemu 2

2⃣SOMO: *HALI YA KIROHO YA ARDHI INAVYOHUSIKA NA KUFUNGWA AU KUFUNGULIWA KWA MAFANIKIO YAKO*

ENEO: *DAR ES SALAAM*

SIKU: 2 March, 06 2017

MWL. C. MWAKASEGE

*TANGAZO MUHIMU*
👌🏽Jumamosi asubuhi kama una huduma ya ualimu hata kama hujui njoo kuna mafundisho na shule ya ualimu kujua na kutambua

👌🏽Na tarehe 14 May Diamond Jubilee siku ya vijana

👌🏽Kila siku maombi yatakuwa yanafanyika mahali hapa kufuatana na somo la siku hiyo

👌Semina pia iko live katika
Channel ya *Swahili Africa* ambayo inapatikana ktk king'amuzi cha Azam channel 120 startimes channel 121.

Itakuwa LIVE ktk siku zote ambazo semina itakuwa inaendelea hapa viwanja vya Tanganyika parkers Kawe Jijini Dar es salaam

https://youtu.be/ryFv_R47ScM
👆👆Semina ya Jana(Video)

*LENGO YA SOMO:*
Kuhakikisha ya kwamba Mafanikio yako yaliofungwa kwenye hali ya kiroho ya ardhi yanafunguliwa

*Kumb 6:12, 2Nyk 7:14*

✅Pitia somo la jana ili kujua tulipotoka na yale mambo ya msingi 5 juu ya kufungua mafanikio yako yaliyofungwa na hali ya kiroho ya ardhi inayofanya mahali unapoishi pawe nyumba ya utumwa

Day 1: https://m.facebook.com/story.php?story_fbid=1288841767871251&id=100002363196786

👆👆Summary

✅Kumbuka jambo la msingi utumwa wa wana wa Israel  haukuwa kwa sababu ya kazi walizokuwa wanafanya bali ni kwa ajili ya hali ya kiroho ya mazingira ya kazi walizokuwa wanafanya

✅Walimlilia MUNGU juu ya uchungu mioyoni mwao wakati wanafanya kazi wala si kwa sababu ya kazi kuwa ngumu

➡Leo tuangalie *NAMNA YA KUJIONDOA KWENYE MADHARA YA LANGO YA ARDHI YA NYUMBA UNAYOISHI INAPOMILIKIWA KIROHO YA NGUVU ZA SHETANI*

➡Ni jambo pana na jipya kwa watu wengi neema ya MUNGU na iwe juu yako kuweza kuona na kufahamu jambo hili maana kujua na kufunguliwa katika jambo hili utafunguliwa katika mambo mengi sana

*Esta 8:1-2, 13-14*
*Mwz 22:17*
*Math 12:29*
*Kut 12:12-23*

*Tuangalie vipengele vichache vya jambo hili ili iwe rahisi kuelewa*

1⃣Ardhi na nyumba iliyojengwa juu yake vina uhusiano wa kiroho

➡Unasema unajuaje…..?

➡Kufuatana na *Kumb 6:12* MUNGU amelinganisha nchi na nyumba kwa hiyo ardhi ile ambayo ina mipaka halali inauhusiano wa kiroho na nyumba inayojengwa

2⃣Mlango wa nyumba una uhusiano na mlango wa ardhi

➡Kwanini? sababu kama ardhi ina uhusiano wa kiroho na nyumba basi na milango yao ina mahusiano

3⃣Ukigusa mlango wa ardhi kiroho unagusa pia mlango wa nyumba kiroho

*Matendo 16:26*

➡Tetemeko lile halikuwa la kawaida lile la kuangusha nyumba bali lilikuwa lile la kushughulika na ardhi ambayo juu yake gereza lilikuwa lipo

➡Sababu walikuwa wapo gerezani kwa jinsi ya mwili isingekuwa rahisi wao kutoka maana hawakufungwa kimwili bali kesi yao mpaka kufungwa kwao ilikuwa kiroho

➡Ndiyo maana MUNGU alileta tetemeko akatikisa misingi ya gereza na Biblia inasema milango ya gereza ikafunguka haisemi ikavunjwa na vifungo walivyokuwa wamefungwa vikaachia

➡Yule askari alipoona milango iko wazi alitaka kujiua maana alijua wametoroka lakini walimwambia asijiue akawakaribisha kwake akawanawisha miguu na kuwatayarishia chakula na baada ya hapo walirudi gerezani

➡Kulipokucha asubuhi wale makadhi waliowafunga walitoa order ya wakina Paulo kuachiliwa.

➡Nini nataka uone hapa gereza halikuvunjwa wala kuwa na nyufa hata moja kutoka kwenye lile tetemeko
MUNGU hakuwa na shida na gereza la nje bali alikuwa na shida na gereza la kiroho ambalo kwa jinsi ya nje watu wanaona kama vile kuta tu na linaweza kuwa sehemu yoyote ile

➡MUNGU alikuwa anashughulika na ardhi  ili kushughulika na nyumba iliyo juu ya ardhi akafungua milango ya ardhi ili kufungua milango ya gereza iliyoko juu yake

➡Kama nyumba yako ni ya utumwa imezungukwa na mazingira ya utumwa usihangaike kuombea nyumba bila kuombea ardhi ya nyumba hiyo maana mlango wa ardhi una uhusiano na mlango wa nyumba yako

➡Vita ya ardhi si vita ya kumshirikisha kila mtu maana ina mapamabano yake mabaya kama hujajipanga

➡Kama huna NENO la kutosha ndani yako MUNGU akikusemesha huwezi kusikia maana kusikia huja kwa *NENO la KRISTO* maana waweza kushughulika na ardhi MUNGU akikwambia shughulikia mlango la ardhi

➡Wakina paulo walienda kuhubiri wakatengeneza mahali pa kusali bila kucheck na kushughulikia nani anamiliki lango la ardhi/nani ni mmiliki wa lile eneo

➡Waulize watu wa nyumba ya Hamani maana kiroho nyumba yake ilikabidhiwa Esta na Modekai sasa haijalishi kikao cha mirathi kimeamua nini maana wamiliki ndio wanaoamua na kutoa ruhusa hali ya kiroho na hali ya maisha ya nyumba hiyo inaendaje

➡Unaanzisha kanisa/fellowship mahali badala ya kuangalia na kucheck nani ameshikilia lango la roho nyingine inayopingana na kitu unachofanya na ambaye ameshikilia lango la ardhi ambalo pia ndilo limeshikilia lango la nyumba ya sehemu hiyo na msingi wa kiroho unayotumia kusali sasa kama vifungo hivi vimefungwa kwenye ardhi na vikaja kuonenakana mpaka kwa nje usipojua namna ya kuvifungua kwenye ardhi uwezi kufunguka

➡Angalia habari ya kina Paulo  kama waliendele na maombi kikundi cha cha ibada kikavurugika wakafungwa jela hata baada ya kutolewa gerezani walifukuzwa kutoka nje ya mji sababu walianzisha huduma mjini bila kusimamia malango ya ardhi ya mji

*Matendo 16:39-40*

➡Walipotoka gerezani walienda kwa Lidya na kukutana na ndugu/wapendwa tu na wale wapendwa waliwafariji tu hawakuwa wa msaada nao wakaenda zao

➡Ndiyo maana chunga sana watu wanaokushabikia huduma wakati hawajui vita unayopitia, chunga sana watu wanakusumizia  front line wakati hawajui kupigana sababu ukifungwa gerezani watakufariji na kukupa pole na kusema tunakuombea na wakati hawajui hata wanachoomba

➡Mji ule ulikuwa na wapendwa lakini hawakuweza kuwasaidia kina Paulo sababu inategemea ni nani aliyeshikilia lango la ardhi kiroho la mji ule.

➡Maana walioshikilia kama hawaitaki huduma kuwa na uhakika itafungwa na watu kuhamia kwenye huduma ama kanisa jingine hata kama wapendwa wapo na usije fikiri watakusaidia watakufariji tu

➡Vikundi vingi sana vya maombi watu hawajui ni kwanini ghafla vimechanua na ghafla vimekufa sababu ni moja tu ulianzisha kikundi cha maombi bila kushughulikia lango la ardhi ambalo Modekai ndiye aliyeshikilia lango hilo na kama uko kinyume naye kuwa na uhakika kikundi hicho kitafungwa kabisa

➡Ndiyo maana unaweza kukuta makanisa mengine yanapata shida eneo hilo lakini nyumba nyingine hazipati hiyo shida ama kanisa moja linapata shida na jingine wala sasa ni mambo mawili au moja lina operate kwa viwango vya juu sana au siyo tishio

➡Ndiyo maana watu wengi wanapata shida kwenye nyumba zao Biblia inaita nyumba za kitumwa na wako kwao.

➡Umewahi kufikiri kwa mfano hicho kiwanja ulichonunua ni nani anamiliki lango la hicho kiwanja katika ulimwengu wa roho?

➡Nani amepewa kumiliki ardhi uliyojenga? Wengine alipewa marehemu sasa ukichanganya jambo hili kiroho kuwa na uhakika kama usipojua namna ya kutengeneza kisiwa cha ardhi ya kwako utapata shida sana kuvuka na vita yake si nyepesi

4⃣Kama vile nyumba ilivyo na mlango zaidi ya mmoja vile vile na ardhi ina milango zaidi ya mmoja inayoweza kutumika kumfunga mtu

*Isay 26:1-2*

➡Nchi ili kurikaribisha taifa, taifa lazima lipite kwenye lango.

➡Anapozungumzia lango kwenye nchi anazungumzia lango la kwenye ardhi linaloruhusu watu kupitia, kuingia na kutoka

*Matendo 16:26-27, 24*

➡….milango… Biblia haituambii milango ilikuwa mingapi mlinzi alipoamka alikuta milango yote imefunguliwa na funguo anazo yeye.

5⃣Kila lango la kiroho katika ardhi au nyumba lina walinzi wa kiroho

*Matendo 12:6,10*

➡Kulikuwa na walinzi kwa ajili ya Petro  na kulikuwa na walinzi kwa ajili ya mlango/nyumba

➡Kuna mapepo unapewa wewe ukitoka nyumbani unakuwa nayo na kuna yale yamepewa kulinda ardhi ya nyumba yako hayatoki.

➡Alipofika kwa wapendwa waliokuwa wanaomba aligonga mlango (maana yake wakikupa kibali na kukufungulia ingia) malaika halazimishi wapendwa kufungua, wakati huku pengine malaika alimpitisha na milango kufunguka yenyewe. Swala ni kwanini hawakumfungulia? maana yuke dada hakufungua mlango baadaye walikuja wakamfungulia

➡Ardhi ile ilikuwa na malango 4, walipita lindo la kwanza na la pili hata mlango wa chuma na wa kuingilia mjini na mpaka kwa wale wapendwa waliokuwa wanamwombea kuna watu ambao wamefunguliwa lakini wako gerezani.

➡Fikiri Petro kama malaika alipomtokea angemwambia avae nguo na viatu kisha akapotea maana yake nini yuko huru keshavaa nguo na viatu lakini yuko gerezani kafungwa hana uhuru tena

➡Ndiyo maana tuna watu wengi sana tunawaombea na inapofika kwenye kufunguliwa kwao tunafunga mlango tunatamani kuwaona kwenye chumba cha maombi lakini kuwafungulia hatufanyi hivyo.

➡Wengi tunawaombea halafu tukikutana nao tunakumbuka na kuona lile tatizo bado kwako hata kama wamebadilika kwa hiyo tunajikuta bado hatujawafungulia ghafla wanarudi gerezani

6⃣Omba kwa imani na kwa juhudi hadi aliyefungwa apite milango yote iliyomkwamisha

*Matendo 12:5*
*Waamuzi 5:8*

➡Kati ya eneo la uwanja la mapambano la MUNGU ni langoni

➡Petro ililazimika avuke geti 4, mbili ndani ya gereza, moja ndani ya mji na nyingine kwa waliokuwa wanamwombea hivyo MUNGU akikupa eneo la kuwavusha watu na kukupa namna ya kuomba omba mpaka uwavushe geti zote

➡Wakati mwingine unapohitaji msaada wa vita unahitaji watu ambao wanajua kupigana uhitaji msaada wa pole hata kama ni pole bali hawata nyamaza mpaka umetoka

➡MUNGU atakupa mamlaka ya kukanyaga na kupita malangoni na kuachilia *DAMU YA YESU* hapo maana hii ni ahadi ya MUNGU kwa Ibrahimu

*MAOMBI*

Angalia  link hii kule  mwishoni kushiriki maombi

https://youtu.be/ryFv_R47ScM

#MUNGU_akubariki_Mtumishi_wa_MUNGU_Mwl_C_Mwakasege

#Usiache_kumwombea_rafiki

#Usiache_kuombea_semina

#UFALME_KWANZA

*……”Jesus Up”…

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni