Jumatano, 1 Machi 2017

KWA NINI BAADHI YA WAKRISTO WANASUMBULIWA NA NGUVU ZA GIZA HUKU WAMEOKOKA

Karibu katika mada hii ujifunze kitu, kuhusu MTU kuokoka ila akasumbuliwa na nguvu za Giza / uchawi.


Zajue sababu zinazo sababisha halo hiyo.


KWA NINI baadhi ya WAKRISTO WANASUMBULIWA NA WACHAWI ilhali WAMEMPOKEA Yesu KRISTO?
________________________________________
________________________________________.

Kuna sababu kama nne zinazosababisha.

1. Dhambi - ukiwa na dhambi hakuna kizuizi lazima mchawi atakusumbua maana uko mbali na MUNGU.

2. Woga - ukimuogopa mchawi lazima akusumbue. cha msingi kwako ni IMANI DHABITI KUWA uchawi si kitu kwako.

3. Ujinga - Hapa ni pale unapojua wazi fika kwamba mchawi hana mamlaka juu yako bado unaamini maneno ya walioshindwa na kukuogopesha unashindwa kujiamini.

4. KUDUMAA / KUTOKUKUA - Mpendwa usipokuwa katika KUMUAMINI MUNGU hakika umedumaa. hapo lazima wachawi wakusumbue maana Hujakua bado fikra zako ziko pale pale hujiongezi.

Ukijitenga na MUNGU imani yako huwa chini ya viwango yakupasa UAMINI KWELI KWELI uwe na IMANI YA DHATI.

USIYUMBISHWE NA LOLOTE.

naishia hapo kwa leo.


cha msingi ACHA DHAMBI , DUMU KATIKA KUOMBA, MTEGEMEE MUNGU hakika WACHAWI SI KITU kwako.


Mungu akubariki.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni