Jumamosi, 25 Machi 2017

SUALA ZIMA ZA USHOGA KIBIBLIA

SUALA ZIMA LA USHOGA (MWANAUME KUOLEWA AU KUMUOA MWANAUME MWENZIWE)

Ni jambo ambalo ni chukizo kubwa sana mbele za MUNGU BABA, na mbele za Mwana-kondoo pamoja na Malaika WATAKATIFU wote. Wakati wa Ibrahimu na LUTU, MUNGU aliamua kuichoma Miji miwili, SODOMA NA GOMORA. kwa sababu ya dhambi hiyo 👇

Mwanzo 19: 12 Basi wale watu wakamwambia Lutu, Je! Unaye mtu hapa zaidi? Mkwe, wanao, na binti zako, na wo wote ulio nao katika mji, uwatoe katika mahali hapa;

13 maana tutapaharibu sisi mahali hapa, kwa kuwa kilio chake kimezidi mbele za BWANA; naye BWANA ametupeleka tupaharibu.

MUNGU hakuishia tu kuwaangamiza watu wa SODOMA na GOMORA, walioendekeza vitendo vya UFIRAJI na ULAWITI! hata wakati wa MUSA, Mungu aliweka sheria hiyo hiyo ya KIFO kwa watu wanaojihusisha na mapenzi ya JINSIA moja. 👇

Walawi 18:22 Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo.

Walawi 20:13 Tena mtu mume akilala pamoja na mtu mume, kama alalavyo na mtu mke, wote wawili wamefanya machukizo; hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao.

Suala zima la USHOGA, ni dhambi mbaya ambayo adhabu yake ni KIFO! haikuwa na msamaha kama ulivyo UONGO, uzushi, Ufisadi. Wahusika hawakupewa nafasi ya kutubia dhambi zao, hata kama wamefanya pasina kujua kuwa ni MACHUKIZO mbele za MUNGU! maana watu wa SODOMA na GOMORA hawakuwa wamepewa sheria ya kuwakataza kufanya kitendo hicho, lakini waliweza kuangamizwa! Kanisa LEO lipo kimya kabisa, na halichukui hatua yo yote kwa Wahuni wanaofungua makanisa kisha kufungisha ndoa za JINSIA hiyo, kitendo Ambacho kinatafsiriwa na wasiokuwa Wakristo kuwa, ni Halali KUFUNGISHWA ndoa hizo katika makanisa, na ukimya wa VIONGOZI wakubwa, ndiyo sababu ya Vitendo hivyo kushamiri, na kuendelea kuliharibia SIFA kanisa la MUNGU! japo maandiko yanasema 👇

Warumi 1:26 Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili;

27 wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao.

28 Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.

Haina maana kwamba, MUNGU ameruhusu, la hasha! bali aliwaacha wayafanye hayo kisha wakapata malipo yaliyowastahili ambayo ni Mauti! Mungu hakutoa kibali hicho, kitendo cha KANISA, kukaa tu na kuwaacha Wahuni hao waendelee kujenga makanisa na kisha kufungisha ndoa za JINSIA MOJA ni dhahiri kuwa KANISA linakubaliana na Wahuni, maandiko yanasema. 👇

Warumi 1:32 ambao wakijua sana hukumu ya haki ya Mungu, ya kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti, wanatenda hayo, wala si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao.

Maandiko yanasema, hao wayatendayo hayo, kwa hukumu ya MUNGU ambayo ni ya haki wamestahili mauti, siyo tu wanaojihusisha na VITENDO hivyo, bali hata na wale wanaokubaliana navyo! nao pia wamestahili mauti. Kukubaliana navyo siyo lazima uifungishe ndoa hiyo, hata kitendo cha Kuwaacha wayatumie Makanisa na hatua ya kuwazuia haichukuliwi, basi ni kitendo cha kukubaliana nacho! na imekuwa ni machukizo kwa MUNGU, hata kuzififisha nguvu za KANISA, Yesu alipoona Hekalu limegeuzwa kuwa PANGO LA WAFANYA BIASHARA, alichukua hatua. 👇

Yohana 2:13 Na Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu; naye Yesu akakwea mpaka Yerusalemu.

14 Akaona pale hekaluni watu waliokuwa wakiuza ng'ombe na kondoo na njiwa, na wenye kuvunja fedha wameketi.

15 Akafanya kikoto cha kambaa, akawatoa wote katika hekalu, na kondoo na ng'ombe; akamwaga fedha za wenye kuvunja fedha, akazipindua meza zao;

16 akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, Yaondoeni haya; msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya biashara.

17 Wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa imeandikwa, Wivu wa nyumba yako utanila.

Sisi LEO ujasiri huu wa YESU KRISTO, tunashindwaje kuwa nao? tunashindwaje kupindua madhabahu zao wafungishao ndoa za JINSIA moja? Paulo alipoona KANISA LA KORINTHO limeanza kuingiza mambo ambayo hayastahili kuwamo ndani ya Kanisa, alichukua hatua ya kuwakemea, kuwa Mkusanyiko waoABEL SULEIMAN SHILIWA:
siyo wa WAFAIDA bali kwa hasara. 👇

1 Korintho 11:16 Lakini mtu ye yote akitaka kuleta fitina, sisi hatuna desturi kama hiyo, wala makanisa ya Mungu.

17 Lakini katika kuagiza haya, siwasifu, ya kwamba mnakusanyika, si kwa faida bali kwa hasara.

18 Kwa maana kwanza mkutanikapo kanisani nasikia kuna faraka kwenu; nami nusu nasadiki;

19 kwa maana lazima kuwapo na uzushi kwenu, ili waliokubaliwa wawe dhahiri kwenu.

20 Basi mkutanikapo pamoja haiwezekani kula chakula cha Bwana;

21 kwa maana kila mmoja hutangulia kutwaa chakula chake katika kule kula; hata huyu ana njaa, na huyu amelewa.

22 Je! Hamna nyumba za kulia na kunywea? Au mnalidharau kanisa la Mungu, na kuwatahayarisha hao wasio na kitu? Niwaambieni? Niwasifu? La! Siwasifu kwa ajili ya hayo.

Hata kama unaamini kuwa wewe haushi CHINI ya sheria, bado siyo sababu ya kukaa kimya! Kwani hao ambao wanafanya hayo, sheria bado inawahusu. 👇

1 TIMOTHEO 1:8 Lakini twajua ya kuwa sheria ni njema, kama mtu akiitumia kwa njia iliyo halali;

9 akilifahamu neno hili, ya kuwa sheria haimhusu mtu wa haki, bali waasi, na wasio wataratibu, na makafiri, na wenye dhambi, na wanajisi, na wasiomcha Mungu, na wapigao baba zao, na wapigao mama zao, na wauaji,

10 na wazinifu, na wafiraji, na waibao watu, na waongo, nao waapao kwa uongo; na likiwapo neno lo lote linginelo lisilopatana na mafundisho yenye uzima;

HAO WATU NI LAZIMA WASHUGHULIKIWE KWA SABABU SHERIA INAWAHUSU WAO, WEWE AMBAYE HUFANYI HAYO, UHUSIKI KATIKA SHERIA. KANISA LIAMKE.

Asanteni Wote mliosoma post hii

Mungu awabariki

Ijumaa, 17 Machi 2017

BWANA YESU ANAWATAFUTA WALIO WAKE Waihubiri INJILI

Bwana YESU anawatafuta watu walio waaminifu  ili waipeleke injili yake.
Anawatafute wateule wanaojua wajibu wao, majukumu yao na wito wao.
Ndugu, inakuaje unapenda kusifiwa na bosi wako kazini lakini hutaki kusifiwa na Bwana YESU aliyekupa injili yake ili uipeleke kwa watu wote?
Wewe hutaki kuipeleka injili, uko busy tu na kazi yako yenye malipo duniani tu na sio mbinguni.
Ndugu peleka injili ya KRISTO mbele, peleka injili kwa kuhubiri watu. Kama huna muda wa kuhubiri basi ipeleke injili kwa pesa yako kwa kuwasapoti wanaoipeleka injili. Peleka injili hata kwa kusambaza vipeperushi vya Neno la MUNGU, peleka injili hata kwa kuwaalika watu kwenda kwenye mikutano ya injili na ibadani kanisani, ni jukumu lako kuipeleka injili, ndugu timiza jukumu lako.
Kuna faida katika kumwamini YESU KRISTO na kulitii Neno la MUNGU.

Faida baadhi za kumwamini YESU na kulitii neno lake ni:

1.  Kuwa pamoja na KRISTO.
Mathayo 28:19-20 " Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la BABA, na MWANA, na ROHO MTAKATIFU ; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari."

2.  Kutenda mema.
2 Timotheo 3:16-17 " Kila andiko, lenye pumzi ya MUNGU, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;  ili mtu wa MUNGU awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema."

3.  Kushiriki pendo la MUNGU baada ya kumaliza kazi duniani.
Yohana 3:16 " Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele."

Ndugu yangu nakuomba sana ihubiri injili ya KRISTO siku zote, huku ukiishi maisha matakatifu katika yeye na huku ukimtii ROHO MTAKATIFU.
MUNGU akubariki sana.

Jumanne, 14 Machi 2017

ALIYEMJUA YESU HAWEZI KUMWACHA KIRAHISI

UKIPATA NEEMA YA KUSOMA BIBLIA NA KUELEWA KILICHOANDIKWA HUMO, Hakika wewe ni mheri.

Mengi yamesemwa kuhusu waliokuwa wakristo hatimaye kuamua kumwacha YESU kwa visingizio visivyokuwa na maana yoyote, hivyo basi wamekuwa mashuhuri wa kupotosha maandiko kama ilivyoandikwa ya kuwa HUYAPOTOSHA MAANDIKO KWA HASARA YA NAFSI ZAO na ni hatari kwa mpotoshaji maana haina maana yoyo ili anaiangamiza nafsi yake.

Soma hapa 👇👇

2PETRO 3

14 Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia mambo hayo, fanyeni bidii ili mwonekane katika amani kuwa hamna mawaa wala aibu mbele yake.
15 Nanyi uhesabuni uvumilivu wa Bwana wetu kuwa ni wokovu, kama vile na ndugu yetu mpenzi Paulo alivyowaandikia kwa hekima aliyopewa;
16 vile vile kama katika nyaraka zake zote pia, akitoa humo habari za mambo hayo; katika nyaraka hizo yamo mambo ambayo ni vigumu kuelewa nayo; na mambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara, huyapotoa, kama vile wayapotoavyo na maandiko mengine, kwa uvunjifu wao wenyewe.

Wao hujifanya waalimu wa neno wakati hawana maarifa, elimu wala uelewa juu ya madai yao.

Nakupa faida ya kulijua Neno la MUNGU, na kwa nini huwezi kumwacha YESU kama unalinua  na umeliewa Neno lake.

Ni ujumbe mrefu ila jitahita kusoma aya na fafanuzi zake kama niatakavyo elezea katika Mathayo 5-7 ni sura 3 ambazo najaribu kukupa mwanga kwazo.

Mathayo 5

8 Heri wenye moyo safi;Maana hao watamwona Mungu.

1. Huwezi kumwacha Mungu eti kisa una Moyo safi.

Yesu amesema wewe una heri. Je waweza kumwacha Yesu kisa hilo?
Jibu ni hapana kwa kuwa unajua kuwa YESU alisema kweli hivyo huwezi kumwacha.

9 Heri wapatanishi;Maana hao wataitwa wana wa Mungu.

2. Ukijua kuwa Yesu ndiye Aliyesema neno hili Huwezi kumwacha.
Upatanishi wako hukuunganisha na Mungu.

10 Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki;Maana ufalme wa mbinguni ni wao.

Unapoijua haki huwezi kumwacha Yesu kwa kuwa haki yote yapatikana kwa Yesu

11 Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu.
12 Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu.

Ukimjua YESU huwezi kumwacha eti kisa wanakusema vibaya kwa ajiri yake, maana jibu unalo kuwa Thawabu yako ni kubwa mbinguni. katika kuudhiwa kwa ajili ya YESU Kuna malipo mazuri sana kule mbinguni kwa ajili yako.

13 Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu.
14 Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima.
15 Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani.
16 Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.

Unapomjua Yesu unapata nibu kuwa kakufanya kuwa nuru na chumvi ya Ulimwengu.

Sote tunajua kuwa nuru ni njema, pia chumvi ni njema pindi iwapo katika ubora wake. Ubora wako ni katika Yesu kristo na si vinginevyo.

Unapotembea katika neno lake huitwa chumvi safi/ nuru. Ukimwacha huitwa giza / chumvi iliyo haribiki.
Ukimjua Yesu ipasavyo huwezi kukubari kuitwa giza au chumvi iliyoharibika.

Kitendo cha kumwacha maana Yake wewe na mbingu ni kama maji na mafuta. Huna nafasi yoyote mbinguni, maana yake unajivua nguo na kubaki uchi!!! Hii ni hatari.
Ukilijua hilo huwezi kumwacha YESU.

17 Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.
18 Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie.
19 Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.
20 Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.

Huwezi kumwacha Yesu kwa kuwa tayari ashakwambia Torati ni kamili haijachakachuliwa (amri na sheria) hivyo yakupasa kutenda haki kuliko mafarisayo na waandishi.
YAKUPASA
Kuzitii amri na sheria kwa ajili ya UFALME WA MUNGU. Ukimwacha Yesu huwezi kuzitenda maana ukiwa na Yesu anakukumbusha ipasavyo kutenda ili uende mbinguni.

Je uko tayari kumwacha baada ya kumjua kuwa Yeye anataka uzitii ili uwe nae mbinguni?

21 Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu.
22 Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto.
23 Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako,
24 iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako.
25 Patana na mshitaki wako upesi, wakati uwapo pamoja naye njiani; yule mshitaki asije akakupeleka kwa kadhi, na kadhi akakupeleka kwa askari, ukatupwa gerezani.
26 Amin, nakuambia, Hutoki humo kamwe hata uishe kulipa senti ya mwisho.

Uko tayari kumwacha Yesu kisa unakosna najirani yako?
Njia nyepesi amekupa ili uendelee kuwa nae moyoni ya kuwa Ni kwenda kumuomba msamaha mshtaki wako ili uwe huru.
Je unaweza kukataa kutubu ? Jibu ni hapana, hicho sicho kiwezacho kukutenga na na Yesu baada ya kumjua.

27 Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini;
28 lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.

Kuzini kunaepukika ili uendelee kuwa na Yesu.
Je, hicho ndo cha kukutenga Yesu?
Ukitenganishwa na hicho wewe hukumjua Yesu. Aliyemjua Yesu huikimbia dunia na tamaa zake.

31 Imenenwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe hati ya talaka;
32 lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.

Uko tayari kuongeza kimada? Ukiongeza hukumjua Yesu na hiyo siyo sababu ya KUMWACHA YESU. ukimwacha Yesu kwa tatizo ni dhahiri kuwa hukumjua hata usidanganye watu.

33 Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana nyapo zako;
34 lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu;
35 wala kwa nchi, kwa maana ndiyo pa kuwekea miguu yake; wala kwa Yerusalemu, kwa maana ndio mji wa Mfalme mkuu.
36 Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi.
37 Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu.

Ukimjua YESU huwezi kuwa na viapo vya ajabu ajabu, maana jibu liko hapo juu kwenye aya hizo.

38 Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino;
39 Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili.
40 Na mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia.
41 Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye mbili.
42 Akuombaye, mpe; naye atakaye kukopa kwako, usimpe kisogo.

Aliyemjua Yesu hana mda wa visasi, ukiona umehadaliwa kwa hilo ujue wewe hukumjua Yesu.

Aliyemjua Yesu hana mkono wa birika hata kwa adui yake.


43 Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;
44 lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,
45 ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.
46 Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo?
47 Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo?
48 Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.

Aliyemjua Yesu ni mtu wa uprndo. Ukiona mtu asiye na upendo huyo hakumjua Yesu.
Alikuwa msanii wa maneno ya ajabu ajabu hatimae akaanguka katika dunia. Hilo si la kukufanya umwache Yesu.

Ukimwacha kwa hilo ni bayana na hakika kuwa hukumjua YESU .

Mathayo 6

1 Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni.
2 Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu.
3 Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume;
4 sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.

Unakuta mtu analalamika eti hasifiwi atendapo mema, anaanza kugoma hata kwenda kanisani.
Nani kasema umeumbwa usifiwe?

Faida ya kusifiwa ni nini hata umwachr Yesu. Amwachaye Yesu kwa sababu hiyo ujue huyo hakumjua Yesu.

9 Basi ninyi salini hivi;Baba yetu uliye mbinguni,Jina lako litukuzwe,Ufalme wako uje,
10 Mapenzi yako yatimizwe,hapa duniani kama huko mbinguni.
11 Utupe leo riziki yetu.
12 Utusamehe deni zetu,kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.
13 Na usitutie majaribuni,lakini utuokoe na yule mwovu.[Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele.Amina.]
14 Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi.
15 Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.

Aliyemjua YESU anasamehe aliyemkosea
hicho ndicho cha kukufanya umwache Yesu?

ukiamwacha kisa tu hutaki kumsamehe aliyekukosea, hiyo inathibitisha kuwa hukumjua YESU.

19 Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba;
20 bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi;
21 kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.

Aliye mjua YESU hazina Yake iko mbinguni, unaweza kumwacha Yesu eti kisa unataka maghorofa duniani?

Aliyemjua Yesu hafanyi hivyo. Afanyaye hivyo hakumjua hata asidanganye watu.


24 Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.

25 Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi?
26 Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao?
27 Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja?
28 Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti
29 nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo.
30 Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?
31 Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?
32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.
33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
34 Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.

Aliyemjua Yesu anamtukia Mungu na si mali. Ukiona mtu anakwambia mi hata kanisani siendi, natafuta mali,
Ujue huyo hakumjua Yesu.

Ndio maana YESU anakwambia mapema usiisumbukie dunia.

Mathayo 7
13 Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo.
14 Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.

Aliyemjua Yesu hatishwi na wingi wa walio kinyume nae, maana anajua kabisa kuwa Yesu ndiye kielelezo na si wingi wa wale wajisifiao kuwa wsko wsko kihaki kuliko wingine.

24 Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;
25 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba.
26 Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga;
27 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa.
28 Ikawa, Yesu alipoyamaliza maneno hayo, makutano walishangaa mno kwa mafundisho yake;
29 kwa maana alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye amri, wala si kama waandishi wao.

Aliye mjua YESU hawezi kuwa na tumaini kwa mwingine, ila tumaini liko kwa YESU, ukiona anayemwacha YESU na kuweka tumaini kwa mwingine huyo hakumjua YESU.

NDIO MAANA NINASEMA ALIYEMJUA YESU HAWEZI KUWACHA KIRAHISI.   YESU NI NJIA KWELI NA UZIMA.

UKISHAJUA KUWA YESU NDIYE NJIA, KWELI NA UZIMA je tumaini lako utakuwa umelielekeza kwa nani?

ALIYE MJUA YESU HAWEZI KUMWACHA NA Kumfuata asiye na tumaini la maisha yake.

YESU NI YOTE NDANI YA YOTE.

NDIO MAANA IMEANDIKWA KUWA ATARUDI KUWACHUKUA WALIO WAKE. Je ukimwacha utakuwa mgeni wa nani?

TAFAKARI CHUKUA HATUA.
.

Jumamosi, 11 Machi 2017

NAMNA YA KUJUA KUWA UMEITWA NA MUNGU KUWA MWALIMU WA NENO LAKE

✍📖📚 *NAMNA YA KUJUA KAMA UMEITWA NA MUNGU KUWA MWALIMU WA NENO LAKE*

*NA MWL MWAKASEGE*

*JANUARY 2017  (ARUSHA UWANJA WA RELI)*

>>Ni muhimu sana kujua kama umeitwa mapema hata kabla ya kuanza huduma ya ualimu. Jambo hili limetokana na ushuhuda wangu mwenyewe wa namna nilivyohangaika sana kujua nimeitwa kuwa Mwalimu wa neno la Mungu.

>>Wakati ule wito ulipokuwa unawaka ndani yangu nilifikiria kazi moja ya kuwa inatakiwa niwe *mchungaji*. Sasa kwa wakati ule huduma ya ualimu ilikuwa haijulikani sana labda mwalimu wa kufundisha tu darasa la waliokoka hivi karibuni au ufundishe Sunday school. Lengo la mimi kwenda kusomea uchungaji ilikuwa ni ili niwe na watu wangu wa kuwafundisha. Kwa wakati ule kupata nafasi ya kuhubiri mahali kama wewe sio mwinjilisti au mchungaji  ilikuwa ni ngumu sana.

>>Na wakati nimeandaa mazingira tayari yakwenda kusomea uchungaji, siku moja  nimekaa kwangu ghafla Roho Mtakatifu anisema na mimi wazi wazi *Kuwa kule kusomea uchungaji kakutuma nani?*  na aliniambia *nitakufundisha mwenyewe*.

Niliwaza sana namna wale watu humo katikati walivyonisaidia hadi kupata nafasi ya kusomea uchungaji, basi niliwatafuta wale watu na nikawaomba msamaha kuwa sikusikia vizuri kwa Mungu. Lakini ilikuwa ni gharama sana.

Sasa fikiria wangenisaidia kusomea uchungaji lakini ni nje ya mapenzi ya Mungu, na ningekuwa mchungaji  lakini nje ya mapenzi ya Mungu, unafikiri gharama yake ingekuaje.

>>Niliomba Mungu anisaidie kujua namna ya kusikia sauti yake.  Na kwa wito wa kipindi kile wa kumtumikia Mungu ilikuwa ni kuimba Kwaya au kuwa mwinjilisti. Basi nilienda kuimba kwaya sasa nako ilikuwa ngumu kweli kweli. Maana nilimwambia yule mwalimu wa kwaya kuwa nahitaji kumuimbia Mungu. Aliniuliza unaimba sauti ya ngapi sasa na mimi nilikuwa sijui kuwa naimba sauti ya ngapi?. Akasema sawa akanipanga sauti ya kwanza. Sasa nako nikawa naimba sauti mara inapanda na kushukua, basi akanihamishia base. Nako nilijua kuwa sifit maana niliona kuna watu wanabase nzuri kuliko ya kwangu. Nikahamia kwa wapiga vyombo niliona namna watu walivyowatalaam kupiga gitaa basi nako kulinishinda. Nilijaribu drums nazo zilinishinda kuchanganya. Sasa nikajaribu tumba nazo ikawa tabu. Sasa niliona kuna mabati yale yamekaa kama mifuniko ya sufuria(crush) basi ndio nikawa napiga maana sikuona mtu anapiga kwa hiyo nikayawahi mimi. Ndio nikawa mpigaji wa hayo mabati.

>>Baadae nikaacha nikaanza kuhubiri kama mwinjilisti lakini naiga. Si unajua unaweza ukawa unacopy kila kitu kutoka kwa mwinjilisti Fulani. Siku moja nilikuwa nahubiri Kijenge kwenye mkutano wa nje. Mzee Moses Kulola alikuja nae kusikiilza akasema _*Yoooooh huyu ni Mwalimu sio mwinjilisti.*_

>>Usipofahamu  kuwa umeitiwa wapi inakuwa ni tabu sana. Maana kwa wakati ule hata kupata vitabu vya kukuelezea ualimu kama huduma moja wapo ambayo Mungu kaitoa , vitabu havielezi sana juu ya ualimu.  Na nilisoma ushuhuda wa  mtumishi mmoja huko Marekani  kuwa yeye alikuwa mchungaji kwa miaka kama 12 ivi na alipoacha kuwa mchungaji na kuwa Mwl wa neno la Mungu ndipo Mungu akasema kuanzia hapa sasa ndio umeanza kunitumika. Yule mtu alisema ngoja kwanza,  yaani miaka yote niliyokutumikia ilikuaje na mbona ulikuwa unanibariki. Mungu alimwambia yule mtu kuwa sikukuita ili  uwe mchungaji na nilikuwa nabariki neno langu. Nilikuwa sikubariki wewe.

>> Pia wakati Fulani nilipigiwa simu na askofu Fulani wa Califonia Marekani, aliniambia Bwana Mwakasege tumesikia huduma yako ila tunahitaji uje kanisani kwetu uwe askofu, na ukikubali tu umasikini bye bye.  Ila nilikataa, akasema basi ngoja tundelee kuomba wazee wake wa kanisa wakawa wanaomba kwa Mungu na kukemea ili nikubali, ila nilikataa maana nilijua ule sio wito nilioitiwa mimi. Kanisani kwake huyo askofu nimewahi hubiri ila nafasi waliyotaka kunipa ndio nilikataa maana ilikuwa nje ya mapenzi ya Mungu.

>>Siku moja nilikuwa Nairobi, na kulikuwa na semina ya wainjilist ilikuwa inaandaliwa Uholanzi, na kulikuwa na shirika moja linaandikisha watu kwa ajili ya kwenda hiyo semina. Basi kulikuwa na rafiki yangu aliniuliza vp umejaza? Nikamwambia hapana sijajaza akasema kwanini,, nilisema naona uzito yule ndugu aliniambia wewe jaza tu. Basi akanijazia na akaituma. Baada ya muda kidogo nikiwa Tanzania nilipata ujumbe Toka Marekani kwa ile huduma ya Bilgram iliyokuwa inaandaa ile semina kuwa ndugu tumekaa kwenye maombi na fomu yako ila tumeona kuwa Mungu hajakuita kuwa mwinjilisti kwa hiyo tunaona bora tuwape nafasi watu wengine wenye huduma hii.

                                                                        *HATUA ZA KUJUA KAMA WEWE NI MWALIMU*

*1 Ualimu ni kundi mojawapo katika utumishi wa neno la Mungu*

_Waefeso 4:11 Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na *waalimu;*_

*2 Nisababu zipi zilimfanya Mungu aweke makundi ya aina tofauti tofauti za watumishi wake*

>>Biblia iko wazi kabisa kuwa kila kitu ambacho Mungu amekiumba kinatenda kazi kwa namna yake, Pia kwa hata shetani nae huwa anaomba kumtumikia Mungu. Nenda kwenye biblia utaona wapi shetani alipoomba kumtumikia Mungu.

>>Kama Mungu anakuita na kukuweka  sehemu Fulani anakupa na sababu. Kwa hiyo nauliza swali *maana yako kama Mwalimu ni nini*

*Ualimu unakusaidia kufikia mahali  ndio maana* 

_Waefeso 4:11-16 Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, *hata* kazi ya huduma itendeke, *hata* mwili wa Kristo ujengwe; *hata* na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, *hata* kuwa mtu mkamilifu, *hata* kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu_. _Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo. Katika yeye mwili wote ukiungamanishwa na kushikanishwa kwa msaada wa kila kiungo, kwa kadiri ya utendaji wa kila sehemu moja moja, huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika upendo._

>>Katika Mistari hii tunaona sababu zifuatazo.

*a). KUWAKAMILISHA WATAKATIFU*

Neno *WATAKATIFU*  ni Zaidi ya kutokuwa na dhambi,  maana mtakatifu ni mtu aliyetengwa kwa kusudi la Mungu.

Sasa hapo nataka uone neno *hata* ziko tano.  Kumbuka maana ya hata ni mpaka au hadi, angalia tena hapo juu.

>>Ualimu ni miongoni mwa makundi matano ya kiutumishi ambayo Mungu kayaweka kwalengo *Kuwakamilisha watakatifu*

>>Sasa ukifuatiliakutoka kwenye zile hata au utaona

*a) Kazi ya huduma itendeke*

*b) Mwili wa Kristo ujengwe*

Kwa hiyo kuwa mwalimu ni ili uwasaidie wengine (wainjilisti, wachungaji.n.k) ili wasimame kwenye nafasi zao ili kwa pamoja msaidiane kujenga kazi ya Mungu.

*c) Umoja wa imani* 

Na kuna tofauti ya umoja wa Roho maana umoja wa Roho unakuja kwa kuokoka na kuna sababu zingine kwenye biblia.

>>Umoja wa Imani, tunajua kuwa imani huja kwa neno la Kristo, baada ya watu kupata ufahamu wa imani na msingi wa kuelewa maandiko yanayotuunganisha ili kuhakikisha neno haliwagawi watu bali linawaweka pamoja.

>> Tunafahamu kwa sehemu mambo ya Mungu na mwana wa Mungu, ile sehemu ninayomfahamu Mungu  inatakiwa itumie kutii neno na Mungu na kuwaunganisha wengine kwa pamoja.

*d) Hata kuwa wakamilifu*

*e) Kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; ili tusiwe tena watoto wachanga ili tufike  kwa yeye aliye kwa Kristo*.

>>Vitu hivyo vyote vimekaa kwa ajili ya makundi matano.
Mwalimu afanye kwa njia ya kufundisha

Mwinjilisti afanye kwa njia ya kuhubiri

Mchungaji afanye kwa njia ya kuchunga

Nabii nae hivyo kwa kutoa unabii

Mtume nae afanye kwa njia yake.

*3 Kuna vitu ambavyo Mungu anaweka ndani ya mtu vinavyoweka alama ya kujulisha ili kujua anamuweka katika kundi lipi la kiutumishi wake*.

_Kutoka 35: 30-34 Kisha Musa akawaambia wana wa Israeli, Angalieni, Bwana amemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila ya Yuda; naye amemjaza roho ya Mungu, katika hekima, na akili, na ujuzi, na kazi ya ustadi kila aina; na kuvumbua kazi za werevu, na kufanya kazi ya dhahabu, na fedha, na shaba, na kukata vito vya kutilia, na kuchora miti, atumike katika kazi za werevu kila aina. Naye amemtilia moyoni mwake ili *apate kufundisha*, yeye, na Oholiabu mwana wa Ahisamaki, wa kabila ya Dani._

>>Ina maana kuna vitu Mungu alimuwekea ndani ya moyo wake ili aweze kufundisha. Hivi ni vitu vilivyoko ndani ya mtu na sio vya kuiga. Maana kuna wengine hawajui kama kuiga ni kilema.  Hujawahi ona mtu anajifanya kilema na anakaa hadi kwenye wheelchair na unaona kuna hatari inakuja unaona ananyanyuka na kuanza kukimbia. Ndipo unaanza kushangaa kuwa huyu hakuwa kilema, bali unakuja gundua kuwa alikuwa anaiga.  Kuna wengine wanajipachika huduma na unajua huyu ni mwalimu kumbe sio yaani kaiga na amekuwa kilema, wacha kitokeze ndani chenyewe maana kama Mungu kakiweka ndani yako utakiona tu. Haijalishi uko wapi kitatoea tu maaana ni cha Mungu.

>>Utatambuaje kuwa wewe ni mwalimu, kuna vitu vimewekwa ndani yako ili kusukuma na kukupa kupenda kile kitu ambacho Mungu kakupa.  Kama Mungu kaweka kuwa nabii basi ujue atafanya kudhihirisha ndani yako kitu cha unabii, vivyo hivyo na kwa huduma zingine.

*NAMNA   VITU HIVI VINAVYOWEKWA NDANI YA MTU*

>>Kila mtu kuna vitu Mungu kamuwekea ndani yake,   ngoja nikuoneshe kidogo.

*1 Kufundisha ni Kipawa*

_Waefeso 4:7,11 Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha *kipawa* chake Kristo, Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu;_

*2 Ni neema*

_Waefeso 4:7 akini kila mmoja wetu alipewa *neema* kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo_
Kumbuka kuwa ukipewa kipawa ni lazima na neema iwe juu yako.  Kwa hiyo kufundisha ni neema

*3 Kufundisha ni karama*

_Warumi 12:4-6 Kwa kuwa kama vile katika mwili mmoja tuna viungo vingi, wala viungo vyote havitendi kazi moja; Vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake. Basi kwa kuwa tuna *karama zilizo mbalimbali*, *kwa kadiri ya neema mliyopewa*; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani;_

*4 Kufundisha ni Upako* (Mafuta ya Roho Mtakatifu)
_1 Yohana 2:27 *Nanyi, mafuta yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha*; lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha habari za mambo yote, tena ni kweli wala si uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani yake._

*5 Ualimu ni hazina*
_Mathayo 13:52 Akawaambia, Kwa sababu hiyo, kila mwandishi mwenye elimu ya ufalme wa mbinguni amefanana na mtu mwenye nyumba atoaye katika *hazina yake vitu vipya na vya kale*._

*6 Ualimu ni wito*

_Waefeso 4:1 Kwa hiyo nawasihi, mimi niliye mfungwa katika Bwana, mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa;_

>>Kwa hiyo katika yale makundi matano ya huduma, na katika ile Kutoka 35:34 tumeona namna Mungu alivyoweka vitu ndani ya Ohaliba ili aweze kufundisha.  Kwa hiyo hivyo vitu sita vilivyotajwa hapo juu ndivyo Mungu anavitumia katika kuweka vitu vyake ndani ya Mtu.

>>Kwa hiyo ni lazima ujue tofauti yake ni nini , kwenye tafsiri ya kawaida ina maana Mungu aligawa vipawa, kwa hiyo *Ualimu ni kipawa ndani ya kipawa*

>>Kwa kiingereza tungesema ni *gift* sasa kwenye Kiswahili ni *zawadi*, ualimu ni kipawa na imebeba kipawa, na. tambua kuwa kipawa ni ofisi. Kipawa cha ualimu kinakupa authority yaani mamlaka ya kufundisha

>> *Neema* Ukienda kuangalia katika maandiko Paulo anasema  _tena walipokwisha kuijua ile *neema niliyopewa*; Yakobo, na Kefa, na Yohana, wenye sifa kuwa ni nguzo, walinipa mimi na Barnaba mkono wa kuume wa shirika; ili sisi tuende kwa Mataifa, na wao waende kwa watu wa tohara;_*Wagalatia 2:9*

>>Kwa hiyo neema inakupa nafasi. Kwenye ualimu hatufanani kila mtu ana neema ya kwake na ni tofauti kati ya mwalimu wa kufundisha masomo ya awali na yule anayefundisha ya ngazi ya juu. Haina maana ya kuwa kuna kufundisha masomo ya chuo kikuu au kufundisha darasa la kwanza au kindergarten  wewe sio mwalimu hapana. Ili mwalimu wa chuo kikuu aweze kumfundisha mwanafunzi vizuri chuo inategemea msingi aliouweka mwalimu wa shule ya awali au darasa la kwanza. kwa hiyo wote ni wa muhimu mnoo.

>>Mama yangu alisomea ualimu na alikuwa anafundisha darasa la kwanza na la pili. Miaka yote alifundisha hapo na hadi alikuja kuwa mwalimu mkuu bado aliendelea kufundisha darasa la kwanza na la pili. Na watu waliopita mikononi mwake wanamkumbuka mpake leo maana kuna alama aliweka katika maisha yao na haiwezi futika. Haijalishi wewe katika neno la Mungu unafundisha katika ngazi ipi wewe ifanye kwa uaminifu na hakika alama utakayoiweka haitafutika.

>>ile wote mmejifunza physics na chemistry na wewe ukawa unafundisha form one na mwingine anafundisha chuo kikuu, haimanishi kuwa yule wa chuo kikuu ni bora sana kuliko yule mwalimu wa form one. Ila jua kuwa katika hii nafasi ya ualimu wote tunatenda kazi ya kuujenga mwili wa Kristo. Tunakwenda sawa sawa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

*4) Karama maana yake vitendea kazi ndani ya ofisi*

>>Kwa hiyo katika kufundisha pia kuna teaching aids, yaani kinachorahisisha kufundisha. Hata kwenye neno la Mungu kuna teaching aids(zana za kufundishia). Sasa kwa wale waliopita ile shule kama tuliyosoma sisi tulikuwa tuanenda *ndude*, ehehe mnazifahamu *ndude* yaani vile vizibo vya soda kule kwetu tunaita ndude. Sasa zile tulikuwa tunatumia kuhesabu ili kujua kuongeza na kutoa. Na ilikuwa inafanyika kwa vitendo ili tuweze kuelewa namna ya kuhesabu.  *Hata kwa Mungu kuna teaching aids yaani mfano na shuhuda* kazi yake ni kusaidia kuelewa.

>> sasa sio kila mtu atakuwa nacho hiki kitu cha kufundisha,ndio maana kuna mahali napenda sana kweye biblia inasema hawata ambizana kuwe mjue Bwana kwa maan watanijua wao. Jifunze na wewe watoto wako kumjua Bwana. Sasa upako alio nao Bonnke ni tofauti na Upako wa wewe mwinjilisti wa kijiji. Bonnke ni mwinjilisti wa Africa sasa upako ulio juu yake ni tofauti na ule utakao kuwa juu yako ewe ambaye ni mwinjilisti wa kijiji. Sasa unakuta uomba Mungu akupe upako kama wa Bonnke wakati wewe ni mwinjilisti wa kijiji. Na usiige omba Mungu akupe kwa kadri yako wewe na ile nafasi aliyokupangia.

>>Sasa niulize mimi ukitaka kuiga, unasimama kwa siku nane kila baada ya muda mchache kwa mwaka mzima, na unatakiwa kila siku ufundishe kitu kipya, upate na muda wa kuomba, kusoma na kuandika vitabu na kazi zingine. Sasa ndio maana nasema usiige maana huwezi jua mzigo aliobeba mtu. Na ukiwa na karama kama hii *haitakiwi ujivune maana hii ni neema Mungu kakupa*

*5) Mwalimu ni mtu ambaye ndani yake kuna elimu ya ufalme.*

>>Elimu inayooanisha mahitaji yaliyoko katika ufalme huu na ujao na sio mfumo huu wa elimu ya kawaida ya huku duniani bali ni elimu ya ufalme.  Hii elimu ya ufalme ya Mungu ina mfumo wa syllabus yake, sasa chukulia mtu anatumia mfumo wa duniani huku anatoa elimu ya mfumo wa kanisa lake badaya ile ya ufalme wa Mungu, ujue tu kuna mahali tutakanyagana kwa maana hatuendani sawa.

>>Ndio maana Yesu alikuwa anabishana na Mafarisayo juu ya elimu waliyokuwa wanaitoa ilikuwa tofauti na ile ya ufalme wa Mungu. Japo wote walisoma torati ile ile ila walikuwa wanazitazama kwa macho tofauti, Mafarisayo waliitazama kidini wakati Yesu aliitazama kwa mfumo wa ufalme wa mbinguni.

*6) Ualimu ni tabia*

Tabia hujidhihirisha katika mwenendo wako, ndio maana ualimu sio kipawa tu bali inageuka kuwa tabia, ndio maana utaona kwa mwalimu kuwa na tabia ya kuuliza maswali ni suala la kawaida kwa maana anataka kuelewa. Na ukiona hata mtoto nyumbani ni mdadisi na anakuwa na maswali mengi basi jua kuwa kuna kipawa cha ualimu ndani yake maana waalimu huwa wanahitaji uelewa.

*7 Cheki ndani yako je moyo wako unakupa kufundisha?*
>>Kufundisha ni kutoa maelekezo

>>Kufundisha ni kufahamisha (kutoa ufahamu)

>>Kufundisha ni kusahihisha, ndio maana mwalimu mzuri hutoa usahihi mahali watu wamekosea au hawajaelwa.

>>Kufundisha ni kujenga madaraja kitu Mungu anataka uweke.
Ndio maana kabla ya kula chakula kigumu unaanza kwanza kunywa maziwa ndipo unakuja kuanza kula chakula kigumu ukisha komaa.

.. Ndio maana kama kuna mahali mwalimu haelewi anataka kuuliza swali, kwa hiyo kama unafundisha usisikie vibaya watu wakikuuliza maswali na wewe unaanza kukemea kuwa sihitahi injili za maswali, ila jua kuwa maswali yanasaidia kuelewa.

>>Kufundisha ni kuadibisha (kumtolea Shetani mtu huyo, ili mwili uadhibiwe, ili na roho iokolewe katika siku ya Bwana Yesu.) 1 Wakorintho 5;5

Kwa hiyo kama wewe unamheshimu Mungu  lazima utahitaji sana Mungu apate heshima anayostahili kuliko mapokeo ya dini yako, na endapo utaona kuna kitu kinaenda tofauti ni lazima tu utasikia vibaya.

>>Katika kulea huduma yako ya ualimu, cheki kwanza nae kulea ana huduma gani, chukulia wewe ni mwalimu unalelewa na mwinjilist si unajua lazima atakuwa anakuonesha vitu vya kuinjilisti Zaidi unakuta na wewe unaanza kuwa mwinjilist lakini huduma hiyo siyo ambayo Mungu alikupangia. Sasa hapo unakuwa unaoa huduma yako. Omba Roho Mtakatifu akusaidie ili upate watu sahihi wa kulea huduma yako. 

>>Pia ukiwa mwalimu lazima *usome sana vitabu mbali mbali kwa msaada wa Roho Mtakatifu ili uweze kuelewa vitu mbali mbali. Hivyo ni muhimu ulewe na kanuni ya kuwa mwalimu bora ni lazima uhakikishe kile kitu unachokifundisha na wewe unakiapply na ndio maana biblia inasema*

*_Jitunze nafsi yako, na mafundisho yako. Dumu katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo utajiokoa nafsi yako na wale wakusikiao pia._1 Timotheo 4:16*

>>Siku nyingine kutakuwa na sehemu ya Maswali, darasa hili litakuwa ni endelevu na tutalifanya si kila mkoa ila pale Mungu atakapotupa nafasi. Zidi kuliweka katika maombi.

*Naamini sasa umeanza kujitambua kuwe wewe ni mwalimu au sio mwalimu. Baada ya hapo jiweke wakfu kwa Bwana ili akusaidie katika huduma hii. Ubarikiwe mnoo*.

✍✍✍✍✍✍✍✍✍
🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏.

Ijumaa, 10 Machi 2017

USHIRIKA NA SANAMU NI KUIABUDU SANAMU

USHIRIKA NA SANAMU NI KUIABUDU SANAMU.

BWANA YESU apewe sifa ndugu yangu.
Karibu tujifunze jambo la kutuvusha kutoka kwenye giza.

1 Kor 10:14 ‘’ Kwa ajili ya hayo, wapenzi wangu, ikimbieni ibada ya sanamu. ‘’

Ujumbe wa MUNGU unakuonya kwamba uikimbie ibada ya sanamu maana yake ondoka kwenye Kanisa au dini wanaoabudu sanamu na Biblia inakushauri vizuri kwamba ingia katika Nuru ya ajabu ya BWANA YESU.

1 Petro 2:9-10 Biblia inasema ‘’ Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya MUNGU, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika NURU YAKE YA AJABU; ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la MUNGU; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema. ‘’

-Watu hawa walioingia kwenye nuru ya MUNGU ya ajabu ni watu wa kitofauti sana, hawafuata tu taratibu kisa taratibu hizo zilikuwepo kwa miaka mingi.
-Wakristo hawa wametengwa mbali na dunia.
-Wanajitambua na wako mbali kabisa na machukizo, -wanamtii MUNGU katika utakatifu wake.

Ndugu zangu, Kama unataka kumpendeza MUNGU hakikisha unamtii MUNGU.

Yako mambo mengi sana ya kumtii MUNGU lakini leo nazungumzia ubaya wa sanamu. 1 Thesalonike 1:9 ‘’ Kwa kuwa wao wenyewe wanatangaza habari zetu, jinsi kulivyokuwa kuingia kwetu kwenu; na jinsi mlivyomgeukia MUNGU mkaziacha sanamu, ili kumtumikia MUNGU aliye hai, wa kweli; ‘’

-Ndugu, kumbe MUNGU wa kweli haabudiwi kwa kuchanganya na sanamu.

Ndugu zangu vitu vingi ambavyo tunadhani ni vitu vizuri na vitakatifu kwa macho yetu, hivyo ni vibaya sana na ukikaa rohoni unaweza kugundua jambo hilo, Mwaka 2012 nilipita mtaa Fulani na kukutana na kijana mmoja anayeuza yale makaratasi makubwa magumu yenye ujumbe wa MUNGU na picha kubwa za Yule wanaodhani wanadamu kwamba ni YESU na Mariamu, sikuipenda picha ile ila nilipenda andiko ambalo lilikuwa limeandikwa kwenye karatasi hiyo, nilinunua na kwenda kubandika chumbani kwangu, ilikuwa ni picha kubwa sana ikiwa na andiko ambalo ndilo hasa mimi nililipenda. Baada ya muda nilianza kuona ugumu Fulani katika maombi, sikujua kwamba tatizo lilikuwa ni nini, usiku niliona katika maono kwamba lile karatasi ni antenna ya kuzimu ili kuona kila ninalofanya. Nilishtuka sana na kuomba kwa juhudi, kesho yake nililitoa lile karatasi lenye picha ya sanamu na tangu siku hiyo nikajifunza jambo jipya. Ndugu zangu haina maana kila karatasi yenye picha ya Mariamu au Yusufu ni mbaya ila kumbuka shetani hutaka kujipenyeza kwenye kila eneo ili tu akupate wewe mteule wa MUNGU.

Kuisujudia sanamu na kuitumikia ni kujiunganisha nayo, Hosea 4:17 -19‘’ Efraimu amejiungamanisha na sanamu; mwache. Kileo chao kimegeuka kuwa uchungu; huzini daima; wakuu wake hupenda aibu. Upepo umemfunikiza kwa mbawa zake; nao watatahayarika kwa sababu ya dhabihu zao. ‘’.

Ndugu Efraimu wa leo ni wewe mwabudu sanamu na unayesujudia sanamu, ni machukizo na kuna adhabu usipotubia na kubadilika.

Dada mmoja alishuhudia kwamba kasanamu ka mariamu kalikokuwa nyumbani kwao alikuwa anakaona usiku kakigeuka nyoka na kuanza kutembea, kasanamu hako walikatoa kanisani, ndugu, MUNGU anapokataza sanamu ni kwa kukusaidia wewe maana macho yako ya kibinadamu hayaoni. Dada mmoja aliota ndoto akiwa anapiga picha na majoka, aliumia sana na akanishirikisha ili ajue maana ya ndoto hiyo, nilipata ufunuo katika hilo, kumbe kila wakipiga picha huwa wanazi-edit kwa picha zao kuweka ndani ya picha nyingine ambazo zimetengeneza huko Ulaya, picha ile nzuri kumbe wala sio picha ya kawaida ni majini. Sasa Yule dada alipoona anapiga picha na majoka na kuogopa kumbe ni kwa picha yake kuunganisha na picha mbaya ambao wemeitoa kwenye internet. Hata wateule wengine mimi binafsi huwa nawashangaa sana, utakuta mtu kaweka picha anayodai ni ya YESU na kukulazimisha uandike amen ili ubarikiwe. Hakuna Baraka za hivyo ndugu yangu, na usiamnini kila picha zingine zimetengeneza na kuzimu kabisa hata kama zinavutia kiasi gani. Hii mifano yote ni picha tu na visanamu vidogo lakini vina madhara makubwa sasa sanamu ni zaidi.

Watu wa zamani waliangushwa sana na kujihisisha na sanamu lakini kanisa la leo hata hatujifunzi kwako.

Waisraeli waliabudu sanamu ya ndama jangwani na ndio maana wengi sana MUNGU aliwaangamiza huko huko jangwani, hata hatujifunzi kwao.

MUNGU anasema kwamba heshima yake wala sifa zake hatawapa sanamu.

Isaya 42:8 ‘’ Mimi ni BWANA; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu. ‘’

Ndugu zangu, jambo la muhimu naomba mtambue kwamba MUNGU hana mwakilishi katika vitu vyote duniani. MUNGU hutumia neno lake kama mwakilishi wa matakwa yake. Neno la MUNGU husomwa na kufafanuliwa na wanadamu waaminifu wakielekezwa na ROHO MTAKATIFU. Hakuna zaidi ya hapo. Sanamu haimwakilishi MUNGU kwa vyovyote vile.

-MUNGU hatawapa sanamu heshima yake.
-BWANA hatawapa sanamu sifa zake.
-MUNGU wa kweli haambatani na sanamu kwa namna yeyote ile.
-Sanamu ni mungu wa kutengeneza na wanadamu, wala sanamu hazihusiki na MUNGU aliye hai.
-Ukitumia sanamu katika mazingira yeyote ya ibada unamkosea MUNGU aliye hai.

Kuna watu hutumia sanamu za Bikra Mariamu na watakatifu wengine wa zamani kwa kuzibusu kwa heshima na kuomba kwa kutumia hizo, Ndugu yangu unayefanya hivyo tambua neno hili ya kwamba unafanya machukizo makuu.

-Kuna watu husujudia sanamu, ni makosa makubwa sana.

Kusujudia sanamu ni kumsujudia shetani(Ufunuo 13:12 ‘’ Naye atumia uwezo wote wa mnyama yule wa kwanza mbele yake. Naye aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona. ‘’)

Mtume Yohana kwa hofu alitaka kumsujudia Malaika, Malaika alimkataza na kumwambia Yohana kwamba wa kusujudiwa ni MUNGU pekee(Ufunuo 22:8-9), MUNGU wa pekee ni MUNGU katika utatu mtakatifu ndio maana BWANA YESU katika maandiko mengi alisujudiwa na hata mbinguni malaika wote humsujudia(Ufunuo 5:8-14, Ufunuo 7:9-12).

-Ndugu yangu, MUNGU BABA amekataza kusujudia sanamu wala kuitumikia, Kumb 5:8-9 ‘’ Usijifanyie sanamu ya kuchonga, mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, au kilicho chini duniani, au kilicho majini chini ya nchi. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi BWANA, MUNGU wako, ni MUNGU mwenye wivu, nawapatiliza wana uovu wa baba zao; hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, ‘’

Kutokana na neno la MUNGU hapo kuna mambo 3 kuhusu sanamu ambayo mwanadamu hatakiwi kuyafanya.

1. Usitengeneze sanamu ya mfano wa kitu chochote kiwe mbinguni, duniani wala kuzimu.

-Hivyo wanaotengeneza sanamu na wewe unaitumia wote wawili mmepotoka.
-Yawezekana wewe hujatengeneza lakini hata kutumia tu katika Ibada ni dhambi.

2. Usisujudie sanamu.

-Wengi wanasujudia sanamu, ni dhambi.
-Wengi wanajishughilisha na sanamu, ni makosa.

-Wengi hudhani kuna uwepo wa MUNGU wakiwa karibu na Sanamu, kumbe kuna uwepo wa shetani, ni dhambi ndugu.

3. Usiitumikie sanamu.

-Maelfu ya watu wanazitumikia sanamu, ni dhambi.
-Watu wengi hutumia sanamu katika ibada zao, ni dhambi.
-Hata kuweka masanamu kanisani kutawasababisha kanisa lenu liwe la kimwili badala ya kuwa la kiroho.
-Kanisa lenu likijaa masanamu, huo ni mlango wa shetani kuwa sehemu ya ibada yenu, ni dhambi.

Makampuni mengi yanatengeneza sanamu za wale ambao majina yao yamo ndani ya Biblia ili tu kuwakosesha watu wengi ambao huzitumi asanamu hizo katika ibada.

MUNGU hataki wewe ndugu uhusike na sanamu katika mazingira yako yoyote ya kiteule. Unadhani kwanini sanamu zimejaaa zaidi makanisani? Ni kwa sababu shetani anawatafuta zaidi watu wa kanisa maana hao wakipata akili ya kuzichoma sanamu hizo watakuwa ni kama wamechoma macho yake ya kuwaona watu wa kanisani. Sanamu zile ni mpango wa shetani kuhakikisha mwanadamu hafiki uzima wa milele.

-Kuna watu ukikemea sanamu wanadhani unaanza kuwavuta watu wahame kanisa lao, lakini ndugu kama kanisa lako lina masanamu hakika ni heri kuhama maana nyie kunena kwa Lugha mtakuwa tu mnakusoma kweli Biblia nyie hakuwahusu.
-Kuombea mtu mapepo yakamtoka mtakuwa tu mnaona kwenye TV na kudhani kwamba hao mnaowaona wanatumia nguvu za giza kumbe ni mamlaka ya MUNGU aliye hai.
-Mkiwa na masanamu kanisani kwenu, Nguvu za MUNGU aliye hai mtakuwa tu mnazisikia redioni.
-Mkiwa na masanamu kanisani Karama za ROHO MTAKATIFU mtakuwa tu mnaziona kwenye TV.

MUNGU anachukizwa na sanamu. Na kibaya zaidi ambacho MUNGU hataki ni kanisa lenu kufuata ratiba ya kanisa la Ulaya, hivyi kanisa la Ulaya likianguka dhambini na nyie lazima tu mtaanguka maana mnawafuata wao, kanisa la Marekani wakitekwa na shetani na kuchapicha kitu kibaya na nyie tu kitawanajisi maana nyie mnawafuata hao kwa kila kitu. Ndio maana Biblia inasema Tuongozwe na ROHO MTAKATIFU na sio kanisa Fulani. Wagalatia 5:18-21 ‘’ Lakini mkiongozwa na ROHO, hampo chini ya sheria. Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa MUNGU. ‘’

Biblia inatutaka tusijiunganishe na sanamu, tena tujilinde na sanamu, yaani tuziepuke sanamu ,1 Yohana 5:21 ‘’ Watoto wadogo, jilindeni nafsi zenu na sanamu. ‘’

Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Alhamisi, 9 Machi 2017

JINSI WANAFUNZI WA YESU WALIVYO KUFA

JINSI WANAFUNZI WA YESU WALIVYOKUFA.!

1. #Mathayo.
Huyu aliuawa kwa upanga huko Uhabeshi (Ethiopia ya leo) baada ya kuonyesha imani kali kwa kutetea kanisa. Alijeruhiwa kwa upanga na kidonda chake hakikupona hadi umauti ulipomfika.

2. #Simoni_Zelote (Mkananayo)
Huyu alifariki huko Alexandria Misri ya sasa baada ya kuangushwa na farasi barabarani, aliangushwa vibaya na hakupata msada. Mwishowe akafariki.

3. #Filipo
Alinyongwa huko Ugiriki, hii ni kutokana na msimamo wake mkali aliouonesha dhidi ya Kristo.

4. #Yohana (nduguye Yakobo)
Huyu alitumbukizwa katika pipa lenye mafuta yanayochemka huko Roma, (Italia ya sasa). Hata hivyo kwa miujiza hakuungua na  alitolewa akiwa mzima kabisa.

Alipelekwa katika gereza lililokuwa katika migodi huko kisiwa cha Patmos. Na huko ndiko alipofunuliwa na mwenyezi Mungu na kuandika kitabu cha "Ufunuo wa Yohana". Baadae aliachiwa huru na kwenda kutumika kama Askofu huko Edessa (Uturuki ya sasa). Alifariki akiwa mzee sana. Na ni mtume pekee aliuefariki bila mateso.

5. #Simoni (Petro)
Huyu alipata adhabu ya kifo cha msalaba. Ila yeye alisulubiwa tofauti na Yesu kristo. Kusulubiwa kwa Petro ilikuwa kichwa chini miguu juu katika msalaba wenye nembo ya "X". Petro mwenyewe aliomba asulubiwa kwa namna hii kwani hakutaka kusulubiwa kama Yesu (Yohana 21:18)

6.#Yakobo (wa Alfayo)
Alikuwa Kiongozi wa kanisa huko Jerusalemu Israel ya sasa. Yeye alitupwa kutoka juu kabisa ya mnara wa hekalu wenye urefu wa meta 100 baada ya kugoma kumpinga Kristo. Mnara huo ni ule ambao Shetani aliutumia kumjaribu Yesu kwa kumwambia kama yeye ni mwana wa Mungu ajirushe.  Walipogundua kuwa hajafa baada ya kumdondosha tokea juu ya mnara, walimpiga na mawe mpaka akafa.

7. #Yakobo (mwana wa Zebedayo nduguye Yohana)
Alikuwa ni mvuvi kabla Yesu hajamteua kuwa mwanafunzi wake. Akiwa kiongozi mkubwa wa kanisa lakini alichinjwa huko Yerusalemu kwa kukatwa kichwa kwa amri ya Herode (Matendo 12:2).

8. #Batholomayo
Pia alijulikana kama Nathanieli. Alikuwa ni mmisionari huko Armeni (Asia ya sasa). Alimshuhudia Yesu Kristo huko Uturuki. Yeye aliuawa kwa kupigwa fimbo baada ya kugoma kuacha mafundisho yake dhidi ya Kristo. Alipigwa fimbo nyingi zilizochubua ngozi yake na kutengeneza vidonda. Kisha akawekewa chumvi ktk vidonda hivyo, na kuanikwa juani hadi mauti ilipomfika.

9. #Andrea
Aliuawa kama Petro huko Ugiriki kwa kusulubiwa kwenye msalaba wenye umbo la "X" miguu juu kichwa chini sawa na Petro Petro. Ila baada ya kuwambwa msalabani aliendelea kupaza sauti akihubiri neno la Mungu mpaka mauti ilipomchukua. Akiwa msalabani aliwaambia wafuasi wake "nilikua naisubiri sana saa kama hii"

10. #Tomaso
Aliuwa kwa kupigwa na mshale huko Chennai (India ya sasa) katika moja ya safari zake kama Mmisionari kwenda kuanzisha Kanisa huko.

11. #Yuda (Thadayo)
Aliuawa kwa kupigwa na mshale ubavuni.

12. #Yuda (Iskariote)
Huyu alijiua kwa kujinyonga baada ya kumuuza Yesu kwa vipande 30 vya fedha. Alinunua shamba kwa zile fedha alizomuuza nazo Yesu. Lakini alijinyongea kwenye shamba hilohilo. Kamba aliyojinyongea ilikatika na akaanguka na tumbo lake kupasuka na matumbo kutoka nje. Shamba lile likaitwa "Akel Dama" yani Shamba la damu (Matendo 1:18-19).

NOTE:
13. #Mathia
Ni Mwanafunzi aliyechaguliwa kuziba nafasi ya Yuda Iskariote (msaliti). Alipigiwa kura na wanafunzi 11 wa Yesu baada ya kifo cha Yuda (Matendo 1:26). Huyu alipigwa na mawe  hadi kufa na baada ya hapo walimkata kichwa.

14. #Paulo
Hakuwa mmoja wa wale wanafunzi 12 wa Yesu. Lakini huhesabika kuwa mfuasi wa Kristo na mtetezi wa mwanzo wa Kanisa. Huyu aliteswa na baadaye akachinjwa na Emperor Nero huko Roma mwaka 65 (A.D).

Kabla ya kuchinjwa Paulo aliishi muda mrefu sana gerezani ambapo akiwa huko aliandika barua (nyaraka) nyingi kwa makanisa mbalimbali. Ndio hizi ambazo zinafundisha misingi ya ukristo katika agano jipya, kama vile Waraka wa Paulo mtume kwa Warumi, Wakoritho, Waefeso, Wakolosai, Wathesalonike, Timotheo etc.

NB: Si muhimu kujua ni namna gani mitume walikufa, ila ni muhimu kujua kuwa mitume wote walikufa wakitetea imani yao. Walikua tayari kuchukiwa na kufa vifo vya mateso kwa ajili ya kumtetea na kumshuhudia Kristo.

Biblia imesema, "Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu, lakini mwenye kuvumilia mpaka mwisho, ndiye atakayeokoka." Mathayo Mtakatifu 10:23

MUNGU AKUBARIKI

USIWE KWAZO KWA NAMNA YOYOTE ILE

USIWE KWAZO LA NAMNA YEYOTE

Bwana YESU atukuzwe mpendwa wangu.

Karibu tujifunze Neno la MUNGU.

Wakati mwingine si mara zote watu hukulaumu kwa kukusingizia, wakati mwingine jichunguze ili usiwe laumu au kwazo pasipo sababu.

2 Kor 6:3-10 '' Tusiwe kwazo la namna yo yote katika jambo lo lote, ili utumishi wetu usilaumiwe;  bali katika kila neno tujipatie sifa njema, kama watumishi wa MUNGU; katika saburi nyingi, katika dhiki, katika misiba, katika shida; katika mapigo, katika vifungo, katika fitina, katika taabu, katika kukesha, katika kufunga; katika kuwa safi, katika elimu, katika uvumilivu, katika utu wema, katika ROHO MTAKATIFU, katika upendo usio unafiki; katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu; kwa silaha za haki za mkono wa kuume na za mkono wa kushoto; kwa utukufu na aibu; kwa kunenwa vibaya na kunenwa vema; kama wadanganyao, bali tu watu wa kweli; kama wasiojulikana, bali wajulikanao sana; kama wanaokufa, kumbe tu hai; kama wanaorudiwa, bali wasiouawa;
kama wenye huzuni, bali siku zote tu wenye furaha; kama maskini, bali tukitajirisha wengi; kama wasio na kitu, bali tu wenye vitu vyote.''

Mtumishi wa MUNGU hapaswi kuwa kwazo.

Kama watu wanakwazika na wewe basi wakwazike kwa sababu ya injili, na kama wanakwazika kwa sababu ya injili basi wewe sio kwazo maana hujawakwaza lolote ila Neno la MUNGU ulisemalo ndilo limewakwaza, na Neno la MUNGU limekamilika na limejitosheleza ili kumsaidia mwanadamu haijalishi anakwazika au anafurahi.

Mtumishi wa MUNGU hutakiwi kuwa mtu wa kusambaza maneno ya uongo maana kwa hayo utakwaza watu.

Mtumishi wa MUNGU hupaswi kuwa mnafiki maana kwa unafiki huo utakwaza watu.
Kama wanadamu wanakusingizia wewe songa mbele maana wao wamekwishapata thawabu yao duniani na wewe endelea kuichuchumilia thawabu ya mbinguni yenye uzima wa milele katika Wokovu wa KRISTO..
YESU KRISTO akusaidie kama unaendelea kumtumainia yeye Mfalme wa Uzima wa milele ila usikubali kuwa kwazo.

Luka 17:1-4 '' Akawaambia wanafunzi wake, Makwazo hayana budi kuja, lakini ole wake mtu yule ambaye yaja kwa sababu yake!  Ingemfaa zaidi mtu huyo jiwe la kusagia lifungwe shingoni mwake, akatupwe baharini, kuliko kumkosesha mmojawapo wa wadogo hawa. Jilindeni; kama ndugu yako akikosa, mwonye; akitubu msamehe. Na kama akikukosa mara saba katika siku moja, na kurudi kwako mara saba, akisema, Nimetubu, msamehe.''

Kuna baadhi ya watu wa kanisa wamegeuka kwazo hata kwa imani maana wanaipotosha kweli.

Unakuta mtumishi anaombea kwa pesa, huko ni kuwa kwazo na ni uovu.

Mathayo 10:8 '' Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.''

Badala ya kuulinda ufalme wa MUNGU wewe unauuza ufalme wa MUNGU?
Umekuwa Mkristo mbaya, umejitenga na KRISTO kwa kufuata tamaa zidanganyazo.
Umekuwa mtumishi mbaya, umejitenga mbali na KRISTO kwa kufuata tamaa zidanganyazo.

Wengine pia wamekuwa makwazo yanayosababisha hata watu waende jehanamu kwa sababu yao.

Wengine hata kweli inatukanwa kwa ajili yao kwa sababu ya uovu wao.

Kila Mteule wa KRISTO ni mtumishi wa MUNGU hivyo haiwapasi watumishi wa MUNGU kuwa makwazo ya kweli ya kuwafanya watu wasije kwa YESU hata wapate uzima.
Ni Mara ngapi umeikataa dhambi kama Yusufu alivyoikataa dhambi?
Ni Mara ngapi umeikimbia dhambi iliyokuwa inakunyemelea?
Ndugu yangu ni muhimu sana kuikataa dhambi na kuikimbia dhambi.
Kumbuka dhambi ni uasi kwa MUNGU, hivyo hatutakiwi kuwa waasi kwa MUNGU.

" Bali ninyi, sivyo mlivyojifunza KRISTO; ikiwa mlimsikia mkafundishwa katika yeye, kama kweli ilivyo katika YESU, mvue kwa habari ya mwenendo wa kwanza utu wa zamani, unaoharibika kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya; na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu;
mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya MUNGU katika haki na utakatifu wa kweli. Basi uvueni uongo, mkaseme kweli kila mtu na jirani yake; kwa maana tu viungo, kila mmoja kiungo cha wenzake. Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka; wala msimpe Ibilisi nafasi. Mwibaji asiibe tena; bali afadhali afanye juhudi, akitenda kazi iliyo nzuri kwa mikono yake mwenyewe, apate kuwa na kitu cha kumgawia mhitaji. Neno lo lote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia. Wala msimhuzunishe yule ROHO MTAKATIFU wa MUNGU; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi. Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya; tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na MUNGU katika KRISTO alivyowasamehe ninyi.-Waefeso 4:20-32"

Mtu mwingine anaweza kugeuka kwazo kwa sababu hajifunzi Neno la MUNGU hata akue kiroho.

Unakuta mtu ameokoka na huu ni mwaka wa 15 lakini hata akiambiwa kufunga masaa 12 tu hawezi.

Ndugu zangu ni muhimu kujua kwamba Mtu anayekua kiroho ni mtu yule anayejituma mwenyewe katika yaliyo ya KRISTO na MUNGU.

Warumi 12:11 "kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia BWANA;"

Je wewe unakua kiroho au umedumaa?
Je unakua kiroho au unashuka viwango vya kiroho?

Ukitaka kukua kiroho chukua kanuni ambayo ya Warumi 12:11  na zingatia maelekezo ya andiko hilo itakusaidia.

Kuna watu pia wamegeuka makwazo kwa sababu tu ya kutetea uovu.

Unakuta Mchungaji anatetea pombe.

Unakuta mtumishi anasifia nyimbo za kidunia.

Unakuta Mtumishi kwa sababu tu ya mapenzi yake kwa chama fulani au taasisi fulani ya kidunia au dhehebu fulani basi hutetea hata ujinga unaofanywa na kikundi hicho au kanisa hilo kwa sababu tu ni watu anaopendezwa nao.

Ndugu pendezwa na Neno la MUNGU na sio machukizo.

Je unaitetea kweli ya MUNGU au unatetea machukizo?
Ndugu, katika utumishi wako hakikisha unaitetea kweli ya injili ya KRISTO.

Hakikisha unakuwa muombaji na  kesha macho ya rohoni.
Omba MUNGU akupe macho ya rohoni ya kukesha.
Hata wakati umelala kimwili lakini macho ya rohoni ya kukesha huona kinachoendelea kwenye ulimwengu wa roho wakati huo.

1 Thesalonike 5:17 '' ombeni bila kukoma;''

Je unataka kufanikiwa katika maisha yako?
Je unataka kufanikiwa kiroho na kimwili?
Jambo muhimu mpokee YESU kama hujampokea.
Ishi maisha matakatifu katika yeye na zingatia hii huku ukihakikisha kwamba wewe sio kwazo la kutafuta pesa kitapeli;

Mithali 16:1-3 "Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu; Bali jawabu la ulimi hutoka kwa BWANA. Njia zote za mtu ni safi machoni pake mwenyewe; Bali BWANA huzipima roho za watu. Mkabidhi BWANA kazi zako, Na mawazo yako yatathibitika."

Najua una matarajio mengi sana lakini kama huna YESU moyoni mwako ni hasara kwako. Biblia inasema

"Usijisifu kwa ajili ya kesho; Kwa maana hujui yatakayozaliwa na siku moja. Mwingine na akusifu wala si kinywa chako mwenyewe; Mtu mgeni wala si midomo yako wewe.-Mithali 27:1-2

Ukiwaza ushindi waza pia na utakatifu na hakikisha ushindi wako unambatana na utakatifu.
Ukiwaza ushindi katika MUNGU hakikisha unadumu katika utakatifu ndani ya Wokovu wa YESU KRISTO utafanikiwa.
Lakini katika yote usikubali kuwa kwazo kwa kanisa au jamii.

Vyanzo vya mtu kuwa kwazo ni.

1. Roho ya kiburi.

  1 Petro 5:5 inasema ''...MUNGU huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.''

Kiburi ndio maana wa dhambi zote.

Kwa kiburi kunaweza kutokea makwazo mengi sana.

2. Dhambi.

1 Yohana 3:4 '' Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi.''

Dhambi hutengeneza mambo mengi na hata kuna makwazo huja baada ya dhambi.

Fikria mwanakwaya anafanya uzinzi na kwaya nzima inaonekana ni wazinzi, na hata nyimbo zao wakiimba kanisani watu huona kama wanapoteza tu muda maana wanajulikana ni wazinzi wakati mzinzi ni mmoja tu na huyo amegeuka kwazo kwa kikundi kizima.

3. Kujihesabia haki.

Mathayo 7:1 ''Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi.''

Anayejihesabia haki siku zote huwaona wengine ni wabaya hata kama yeye ndiye mbaya.

Anaweza akawahukumu wengine hata kama yeye ndiye anapaswa kuhukumiwa.

4. Kujiona bora kuliko wengine.

Wafilipi 2:3 ''Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake.''

Ukijiona wewe ni bora kuliko wengine unakuwa unapishana Neno la MUNGU linalokutaka uwahesabu wengine ni bora kuliko wewe.

Ukijiona bora kuliko wengine hakika hutakuwa na unyenyekevu na kwa njia hiyo utageuka tu kwazo katika sehemu sehemu.

Kuna watu hata hawawezi kuwatii wachungaji wao kwenye kweli ya MUNGU na kwa njia hiyo hugeuka makwazo.

Kuna watu hata huwafuata baadhi ya washirika ili kuwarubuni ili wasifanye jambo fulani jema la kikanisa lililopagwa, kwa sababu tu wao hawakupewa kusimamia, huko ni kujiinua na kujiona bora na kwa njia hiyo mtu kama huyo lazima awe makwazo tu.

5. Tamaa.

Yakobo 1:14-16 ''Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa. Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti. Ndugu zangu wapenzi, msidanganyike.''

Ndugu tamaa zako mbaya zinaweza kuleta makwazo kwa jamii au kanisa au familia au majirani.

Usikubali kuwa kwazo lolote kwa sababu tu ya tamaa zako za kipepo.

Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.

MUNGU AKUBARIKI