Jumanne, 14 Machi 2017

ALIYEMJUA YESU HAWEZI KUMWACHA KIRAHISI

UKIPATA NEEMA YA KUSOMA BIBLIA NA KUELEWA KILICHOANDIKWA HUMO, Hakika wewe ni mheri.

Mengi yamesemwa kuhusu waliokuwa wakristo hatimaye kuamua kumwacha YESU kwa visingizio visivyokuwa na maana yoyote, hivyo basi wamekuwa mashuhuri wa kupotosha maandiko kama ilivyoandikwa ya kuwa HUYAPOTOSHA MAANDIKO KWA HASARA YA NAFSI ZAO na ni hatari kwa mpotoshaji maana haina maana yoyo ili anaiangamiza nafsi yake.

Soma hapa 👇👇

2PETRO 3

14 Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia mambo hayo, fanyeni bidii ili mwonekane katika amani kuwa hamna mawaa wala aibu mbele yake.
15 Nanyi uhesabuni uvumilivu wa Bwana wetu kuwa ni wokovu, kama vile na ndugu yetu mpenzi Paulo alivyowaandikia kwa hekima aliyopewa;
16 vile vile kama katika nyaraka zake zote pia, akitoa humo habari za mambo hayo; katika nyaraka hizo yamo mambo ambayo ni vigumu kuelewa nayo; na mambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara, huyapotoa, kama vile wayapotoavyo na maandiko mengine, kwa uvunjifu wao wenyewe.

Wao hujifanya waalimu wa neno wakati hawana maarifa, elimu wala uelewa juu ya madai yao.

Nakupa faida ya kulijua Neno la MUNGU, na kwa nini huwezi kumwacha YESU kama unalinua  na umeliewa Neno lake.

Ni ujumbe mrefu ila jitahita kusoma aya na fafanuzi zake kama niatakavyo elezea katika Mathayo 5-7 ni sura 3 ambazo najaribu kukupa mwanga kwazo.

Mathayo 5

8 Heri wenye moyo safi;Maana hao watamwona Mungu.

1. Huwezi kumwacha Mungu eti kisa una Moyo safi.

Yesu amesema wewe una heri. Je waweza kumwacha Yesu kisa hilo?
Jibu ni hapana kwa kuwa unajua kuwa YESU alisema kweli hivyo huwezi kumwacha.

9 Heri wapatanishi;Maana hao wataitwa wana wa Mungu.

2. Ukijua kuwa Yesu ndiye Aliyesema neno hili Huwezi kumwacha.
Upatanishi wako hukuunganisha na Mungu.

10 Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki;Maana ufalme wa mbinguni ni wao.

Unapoijua haki huwezi kumwacha Yesu kwa kuwa haki yote yapatikana kwa Yesu

11 Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu.
12 Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu.

Ukimjua YESU huwezi kumwacha eti kisa wanakusema vibaya kwa ajiri yake, maana jibu unalo kuwa Thawabu yako ni kubwa mbinguni. katika kuudhiwa kwa ajili ya YESU Kuna malipo mazuri sana kule mbinguni kwa ajili yako.

13 Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu.
14 Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima.
15 Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani.
16 Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.

Unapomjua Yesu unapata nibu kuwa kakufanya kuwa nuru na chumvi ya Ulimwengu.

Sote tunajua kuwa nuru ni njema, pia chumvi ni njema pindi iwapo katika ubora wake. Ubora wako ni katika Yesu kristo na si vinginevyo.

Unapotembea katika neno lake huitwa chumvi safi/ nuru. Ukimwacha huitwa giza / chumvi iliyo haribiki.
Ukimjua Yesu ipasavyo huwezi kukubari kuitwa giza au chumvi iliyoharibika.

Kitendo cha kumwacha maana Yake wewe na mbingu ni kama maji na mafuta. Huna nafasi yoyote mbinguni, maana yake unajivua nguo na kubaki uchi!!! Hii ni hatari.
Ukilijua hilo huwezi kumwacha YESU.

17 Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.
18 Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie.
19 Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.
20 Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.

Huwezi kumwacha Yesu kwa kuwa tayari ashakwambia Torati ni kamili haijachakachuliwa (amri na sheria) hivyo yakupasa kutenda haki kuliko mafarisayo na waandishi.
YAKUPASA
Kuzitii amri na sheria kwa ajili ya UFALME WA MUNGU. Ukimwacha Yesu huwezi kuzitenda maana ukiwa na Yesu anakukumbusha ipasavyo kutenda ili uende mbinguni.

Je uko tayari kumwacha baada ya kumjua kuwa Yeye anataka uzitii ili uwe nae mbinguni?

21 Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu.
22 Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto.
23 Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako,
24 iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako.
25 Patana na mshitaki wako upesi, wakati uwapo pamoja naye njiani; yule mshitaki asije akakupeleka kwa kadhi, na kadhi akakupeleka kwa askari, ukatupwa gerezani.
26 Amin, nakuambia, Hutoki humo kamwe hata uishe kulipa senti ya mwisho.

Uko tayari kumwacha Yesu kisa unakosna najirani yako?
Njia nyepesi amekupa ili uendelee kuwa nae moyoni ya kuwa Ni kwenda kumuomba msamaha mshtaki wako ili uwe huru.
Je unaweza kukataa kutubu ? Jibu ni hapana, hicho sicho kiwezacho kukutenga na na Yesu baada ya kumjua.

27 Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini;
28 lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.

Kuzini kunaepukika ili uendelee kuwa na Yesu.
Je, hicho ndo cha kukutenga Yesu?
Ukitenganishwa na hicho wewe hukumjua Yesu. Aliyemjua Yesu huikimbia dunia na tamaa zake.

31 Imenenwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe hati ya talaka;
32 lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.

Uko tayari kuongeza kimada? Ukiongeza hukumjua Yesu na hiyo siyo sababu ya KUMWACHA YESU. ukimwacha Yesu kwa tatizo ni dhahiri kuwa hukumjua hata usidanganye watu.

33 Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana nyapo zako;
34 lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu;
35 wala kwa nchi, kwa maana ndiyo pa kuwekea miguu yake; wala kwa Yerusalemu, kwa maana ndio mji wa Mfalme mkuu.
36 Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi.
37 Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu.

Ukimjua YESU huwezi kuwa na viapo vya ajabu ajabu, maana jibu liko hapo juu kwenye aya hizo.

38 Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino;
39 Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili.
40 Na mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia.
41 Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye mbili.
42 Akuombaye, mpe; naye atakaye kukopa kwako, usimpe kisogo.

Aliyemjua Yesu hana mda wa visasi, ukiona umehadaliwa kwa hilo ujue wewe hukumjua Yesu.

Aliyemjua Yesu hana mkono wa birika hata kwa adui yake.


43 Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;
44 lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,
45 ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.
46 Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo?
47 Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo?
48 Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.

Aliyemjua Yesu ni mtu wa uprndo. Ukiona mtu asiye na upendo huyo hakumjua Yesu.
Alikuwa msanii wa maneno ya ajabu ajabu hatimae akaanguka katika dunia. Hilo si la kukufanya umwache Yesu.

Ukimwacha kwa hilo ni bayana na hakika kuwa hukumjua YESU .

Mathayo 6

1 Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni.
2 Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu.
3 Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume;
4 sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.

Unakuta mtu analalamika eti hasifiwi atendapo mema, anaanza kugoma hata kwenda kanisani.
Nani kasema umeumbwa usifiwe?

Faida ya kusifiwa ni nini hata umwachr Yesu. Amwachaye Yesu kwa sababu hiyo ujue huyo hakumjua Yesu.

9 Basi ninyi salini hivi;Baba yetu uliye mbinguni,Jina lako litukuzwe,Ufalme wako uje,
10 Mapenzi yako yatimizwe,hapa duniani kama huko mbinguni.
11 Utupe leo riziki yetu.
12 Utusamehe deni zetu,kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.
13 Na usitutie majaribuni,lakini utuokoe na yule mwovu.[Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele.Amina.]
14 Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi.
15 Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.

Aliyemjua YESU anasamehe aliyemkosea
hicho ndicho cha kukufanya umwache Yesu?

ukiamwacha kisa tu hutaki kumsamehe aliyekukosea, hiyo inathibitisha kuwa hukumjua YESU.

19 Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba;
20 bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi;
21 kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.

Aliye mjua YESU hazina Yake iko mbinguni, unaweza kumwacha Yesu eti kisa unataka maghorofa duniani?

Aliyemjua Yesu hafanyi hivyo. Afanyaye hivyo hakumjua hata asidanganye watu.


24 Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.

25 Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi?
26 Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao?
27 Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja?
28 Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti
29 nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo.
30 Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?
31 Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?
32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.
33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
34 Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.

Aliyemjua Yesu anamtukia Mungu na si mali. Ukiona mtu anakwambia mi hata kanisani siendi, natafuta mali,
Ujue huyo hakumjua Yesu.

Ndio maana YESU anakwambia mapema usiisumbukie dunia.

Mathayo 7
13 Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo.
14 Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.

Aliyemjua Yesu hatishwi na wingi wa walio kinyume nae, maana anajua kabisa kuwa Yesu ndiye kielelezo na si wingi wa wale wajisifiao kuwa wsko wsko kihaki kuliko wingine.

24 Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;
25 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba.
26 Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga;
27 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa.
28 Ikawa, Yesu alipoyamaliza maneno hayo, makutano walishangaa mno kwa mafundisho yake;
29 kwa maana alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye amri, wala si kama waandishi wao.

Aliye mjua YESU hawezi kuwa na tumaini kwa mwingine, ila tumaini liko kwa YESU, ukiona anayemwacha YESU na kuweka tumaini kwa mwingine huyo hakumjua YESU.

NDIO MAANA NINASEMA ALIYEMJUA YESU HAWEZI KUWACHA KIRAHISI.   YESU NI NJIA KWELI NA UZIMA.

UKISHAJUA KUWA YESU NDIYE NJIA, KWELI NA UZIMA je tumaini lako utakuwa umelielekeza kwa nani?

ALIYE MJUA YESU HAWEZI KUMWACHA NA Kumfuata asiye na tumaini la maisha yake.

YESU NI YOTE NDANI YA YOTE.

NDIO MAANA IMEANDIKWA KUWA ATARUDI KUWACHUKUA WALIO WAKE. Je ukimwacha utakuwa mgeni wa nani?

TAFAKARI CHUKUA HATUA.
.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni