Ijumaa, 17 Machi 2017

BWANA YESU ANAWATAFUTA WALIO WAKE Waihubiri INJILI

Bwana YESU anawatafuta watu walio waaminifu  ili waipeleke injili yake.
Anawatafute wateule wanaojua wajibu wao, majukumu yao na wito wao.
Ndugu, inakuaje unapenda kusifiwa na bosi wako kazini lakini hutaki kusifiwa na Bwana YESU aliyekupa injili yake ili uipeleke kwa watu wote?
Wewe hutaki kuipeleka injili, uko busy tu na kazi yako yenye malipo duniani tu na sio mbinguni.
Ndugu peleka injili ya KRISTO mbele, peleka injili kwa kuhubiri watu. Kama huna muda wa kuhubiri basi ipeleke injili kwa pesa yako kwa kuwasapoti wanaoipeleka injili. Peleka injili hata kwa kusambaza vipeperushi vya Neno la MUNGU, peleka injili hata kwa kuwaalika watu kwenda kwenye mikutano ya injili na ibadani kanisani, ni jukumu lako kuipeleka injili, ndugu timiza jukumu lako.
Kuna faida katika kumwamini YESU KRISTO na kulitii Neno la MUNGU.

Faida baadhi za kumwamini YESU na kulitii neno lake ni:

1.  Kuwa pamoja na KRISTO.
Mathayo 28:19-20 " Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la BABA, na MWANA, na ROHO MTAKATIFU ; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari."

2.  Kutenda mema.
2 Timotheo 3:16-17 " Kila andiko, lenye pumzi ya MUNGU, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;  ili mtu wa MUNGU awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema."

3.  Kushiriki pendo la MUNGU baada ya kumaliza kazi duniani.
Yohana 3:16 " Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele."

Ndugu yangu nakuomba sana ihubiri injili ya KRISTO siku zote, huku ukiishi maisha matakatifu katika yeye na huku ukimtii ROHO MTAKATIFU.
MUNGU akubariki sana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni