Jumamosi, 11 Machi 2017

NAMNA YA KUJUA KUWA UMEITWA NA MUNGU KUWA MWALIMU WA NENO LAKE

✍📖📚 *NAMNA YA KUJUA KAMA UMEITWA NA MUNGU KUWA MWALIMU WA NENO LAKE*

*NA MWL MWAKASEGE*

*JANUARY 2017  (ARUSHA UWANJA WA RELI)*

>>Ni muhimu sana kujua kama umeitwa mapema hata kabla ya kuanza huduma ya ualimu. Jambo hili limetokana na ushuhuda wangu mwenyewe wa namna nilivyohangaika sana kujua nimeitwa kuwa Mwalimu wa neno la Mungu.

>>Wakati ule wito ulipokuwa unawaka ndani yangu nilifikiria kazi moja ya kuwa inatakiwa niwe *mchungaji*. Sasa kwa wakati ule huduma ya ualimu ilikuwa haijulikani sana labda mwalimu wa kufundisha tu darasa la waliokoka hivi karibuni au ufundishe Sunday school. Lengo la mimi kwenda kusomea uchungaji ilikuwa ni ili niwe na watu wangu wa kuwafundisha. Kwa wakati ule kupata nafasi ya kuhubiri mahali kama wewe sio mwinjilisti au mchungaji  ilikuwa ni ngumu sana.

>>Na wakati nimeandaa mazingira tayari yakwenda kusomea uchungaji, siku moja  nimekaa kwangu ghafla Roho Mtakatifu anisema na mimi wazi wazi *Kuwa kule kusomea uchungaji kakutuma nani?*  na aliniambia *nitakufundisha mwenyewe*.

Niliwaza sana namna wale watu humo katikati walivyonisaidia hadi kupata nafasi ya kusomea uchungaji, basi niliwatafuta wale watu na nikawaomba msamaha kuwa sikusikia vizuri kwa Mungu. Lakini ilikuwa ni gharama sana.

Sasa fikiria wangenisaidia kusomea uchungaji lakini ni nje ya mapenzi ya Mungu, na ningekuwa mchungaji  lakini nje ya mapenzi ya Mungu, unafikiri gharama yake ingekuaje.

>>Niliomba Mungu anisaidie kujua namna ya kusikia sauti yake.  Na kwa wito wa kipindi kile wa kumtumikia Mungu ilikuwa ni kuimba Kwaya au kuwa mwinjilisti. Basi nilienda kuimba kwaya sasa nako ilikuwa ngumu kweli kweli. Maana nilimwambia yule mwalimu wa kwaya kuwa nahitaji kumuimbia Mungu. Aliniuliza unaimba sauti ya ngapi sasa na mimi nilikuwa sijui kuwa naimba sauti ya ngapi?. Akasema sawa akanipanga sauti ya kwanza. Sasa nako nikawa naimba sauti mara inapanda na kushukua, basi akanihamishia base. Nako nilijua kuwa sifit maana niliona kuna watu wanabase nzuri kuliko ya kwangu. Nikahamia kwa wapiga vyombo niliona namna watu walivyowatalaam kupiga gitaa basi nako kulinishinda. Nilijaribu drums nazo zilinishinda kuchanganya. Sasa nikajaribu tumba nazo ikawa tabu. Sasa niliona kuna mabati yale yamekaa kama mifuniko ya sufuria(crush) basi ndio nikawa napiga maana sikuona mtu anapiga kwa hiyo nikayawahi mimi. Ndio nikawa mpigaji wa hayo mabati.

>>Baadae nikaacha nikaanza kuhubiri kama mwinjilisti lakini naiga. Si unajua unaweza ukawa unacopy kila kitu kutoka kwa mwinjilisti Fulani. Siku moja nilikuwa nahubiri Kijenge kwenye mkutano wa nje. Mzee Moses Kulola alikuja nae kusikiilza akasema _*Yoooooh huyu ni Mwalimu sio mwinjilisti.*_

>>Usipofahamu  kuwa umeitiwa wapi inakuwa ni tabu sana. Maana kwa wakati ule hata kupata vitabu vya kukuelezea ualimu kama huduma moja wapo ambayo Mungu kaitoa , vitabu havielezi sana juu ya ualimu.  Na nilisoma ushuhuda wa  mtumishi mmoja huko Marekani  kuwa yeye alikuwa mchungaji kwa miaka kama 12 ivi na alipoacha kuwa mchungaji na kuwa Mwl wa neno la Mungu ndipo Mungu akasema kuanzia hapa sasa ndio umeanza kunitumika. Yule mtu alisema ngoja kwanza,  yaani miaka yote niliyokutumikia ilikuaje na mbona ulikuwa unanibariki. Mungu alimwambia yule mtu kuwa sikukuita ili  uwe mchungaji na nilikuwa nabariki neno langu. Nilikuwa sikubariki wewe.

>> Pia wakati Fulani nilipigiwa simu na askofu Fulani wa Califonia Marekani, aliniambia Bwana Mwakasege tumesikia huduma yako ila tunahitaji uje kanisani kwetu uwe askofu, na ukikubali tu umasikini bye bye.  Ila nilikataa, akasema basi ngoja tundelee kuomba wazee wake wa kanisa wakawa wanaomba kwa Mungu na kukemea ili nikubali, ila nilikataa maana nilijua ule sio wito nilioitiwa mimi. Kanisani kwake huyo askofu nimewahi hubiri ila nafasi waliyotaka kunipa ndio nilikataa maana ilikuwa nje ya mapenzi ya Mungu.

>>Siku moja nilikuwa Nairobi, na kulikuwa na semina ya wainjilist ilikuwa inaandaliwa Uholanzi, na kulikuwa na shirika moja linaandikisha watu kwa ajili ya kwenda hiyo semina. Basi kulikuwa na rafiki yangu aliniuliza vp umejaza? Nikamwambia hapana sijajaza akasema kwanini,, nilisema naona uzito yule ndugu aliniambia wewe jaza tu. Basi akanijazia na akaituma. Baada ya muda kidogo nikiwa Tanzania nilipata ujumbe Toka Marekani kwa ile huduma ya Bilgram iliyokuwa inaandaa ile semina kuwa ndugu tumekaa kwenye maombi na fomu yako ila tumeona kuwa Mungu hajakuita kuwa mwinjilisti kwa hiyo tunaona bora tuwape nafasi watu wengine wenye huduma hii.

                                                                        *HATUA ZA KUJUA KAMA WEWE NI MWALIMU*

*1 Ualimu ni kundi mojawapo katika utumishi wa neno la Mungu*

_Waefeso 4:11 Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na *waalimu;*_

*2 Nisababu zipi zilimfanya Mungu aweke makundi ya aina tofauti tofauti za watumishi wake*

>>Biblia iko wazi kabisa kuwa kila kitu ambacho Mungu amekiumba kinatenda kazi kwa namna yake, Pia kwa hata shetani nae huwa anaomba kumtumikia Mungu. Nenda kwenye biblia utaona wapi shetani alipoomba kumtumikia Mungu.

>>Kama Mungu anakuita na kukuweka  sehemu Fulani anakupa na sababu. Kwa hiyo nauliza swali *maana yako kama Mwalimu ni nini*

*Ualimu unakusaidia kufikia mahali  ndio maana* 

_Waefeso 4:11-16 Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, *hata* kazi ya huduma itendeke, *hata* mwili wa Kristo ujengwe; *hata* na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, *hata* kuwa mtu mkamilifu, *hata* kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu_. _Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo. Katika yeye mwili wote ukiungamanishwa na kushikanishwa kwa msaada wa kila kiungo, kwa kadiri ya utendaji wa kila sehemu moja moja, huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika upendo._

>>Katika Mistari hii tunaona sababu zifuatazo.

*a). KUWAKAMILISHA WATAKATIFU*

Neno *WATAKATIFU*  ni Zaidi ya kutokuwa na dhambi,  maana mtakatifu ni mtu aliyetengwa kwa kusudi la Mungu.

Sasa hapo nataka uone neno *hata* ziko tano.  Kumbuka maana ya hata ni mpaka au hadi, angalia tena hapo juu.

>>Ualimu ni miongoni mwa makundi matano ya kiutumishi ambayo Mungu kayaweka kwalengo *Kuwakamilisha watakatifu*

>>Sasa ukifuatiliakutoka kwenye zile hata au utaona

*a) Kazi ya huduma itendeke*

*b) Mwili wa Kristo ujengwe*

Kwa hiyo kuwa mwalimu ni ili uwasaidie wengine (wainjilisti, wachungaji.n.k) ili wasimame kwenye nafasi zao ili kwa pamoja msaidiane kujenga kazi ya Mungu.

*c) Umoja wa imani* 

Na kuna tofauti ya umoja wa Roho maana umoja wa Roho unakuja kwa kuokoka na kuna sababu zingine kwenye biblia.

>>Umoja wa Imani, tunajua kuwa imani huja kwa neno la Kristo, baada ya watu kupata ufahamu wa imani na msingi wa kuelewa maandiko yanayotuunganisha ili kuhakikisha neno haliwagawi watu bali linawaweka pamoja.

>> Tunafahamu kwa sehemu mambo ya Mungu na mwana wa Mungu, ile sehemu ninayomfahamu Mungu  inatakiwa itumie kutii neno na Mungu na kuwaunganisha wengine kwa pamoja.

*d) Hata kuwa wakamilifu*

*e) Kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; ili tusiwe tena watoto wachanga ili tufike  kwa yeye aliye kwa Kristo*.

>>Vitu hivyo vyote vimekaa kwa ajili ya makundi matano.
Mwalimu afanye kwa njia ya kufundisha

Mwinjilisti afanye kwa njia ya kuhubiri

Mchungaji afanye kwa njia ya kuchunga

Nabii nae hivyo kwa kutoa unabii

Mtume nae afanye kwa njia yake.

*3 Kuna vitu ambavyo Mungu anaweka ndani ya mtu vinavyoweka alama ya kujulisha ili kujua anamuweka katika kundi lipi la kiutumishi wake*.

_Kutoka 35: 30-34 Kisha Musa akawaambia wana wa Israeli, Angalieni, Bwana amemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila ya Yuda; naye amemjaza roho ya Mungu, katika hekima, na akili, na ujuzi, na kazi ya ustadi kila aina; na kuvumbua kazi za werevu, na kufanya kazi ya dhahabu, na fedha, na shaba, na kukata vito vya kutilia, na kuchora miti, atumike katika kazi za werevu kila aina. Naye amemtilia moyoni mwake ili *apate kufundisha*, yeye, na Oholiabu mwana wa Ahisamaki, wa kabila ya Dani._

>>Ina maana kuna vitu Mungu alimuwekea ndani ya moyo wake ili aweze kufundisha. Hivi ni vitu vilivyoko ndani ya mtu na sio vya kuiga. Maana kuna wengine hawajui kama kuiga ni kilema.  Hujawahi ona mtu anajifanya kilema na anakaa hadi kwenye wheelchair na unaona kuna hatari inakuja unaona ananyanyuka na kuanza kukimbia. Ndipo unaanza kushangaa kuwa huyu hakuwa kilema, bali unakuja gundua kuwa alikuwa anaiga.  Kuna wengine wanajipachika huduma na unajua huyu ni mwalimu kumbe sio yaani kaiga na amekuwa kilema, wacha kitokeze ndani chenyewe maana kama Mungu kakiweka ndani yako utakiona tu. Haijalishi uko wapi kitatoea tu maaana ni cha Mungu.

>>Utatambuaje kuwa wewe ni mwalimu, kuna vitu vimewekwa ndani yako ili kusukuma na kukupa kupenda kile kitu ambacho Mungu kakupa.  Kama Mungu kaweka kuwa nabii basi ujue atafanya kudhihirisha ndani yako kitu cha unabii, vivyo hivyo na kwa huduma zingine.

*NAMNA   VITU HIVI VINAVYOWEKWA NDANI YA MTU*

>>Kila mtu kuna vitu Mungu kamuwekea ndani yake,   ngoja nikuoneshe kidogo.

*1 Kufundisha ni Kipawa*

_Waefeso 4:7,11 Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha *kipawa* chake Kristo, Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu;_

*2 Ni neema*

_Waefeso 4:7 akini kila mmoja wetu alipewa *neema* kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo_
Kumbuka kuwa ukipewa kipawa ni lazima na neema iwe juu yako.  Kwa hiyo kufundisha ni neema

*3 Kufundisha ni karama*

_Warumi 12:4-6 Kwa kuwa kama vile katika mwili mmoja tuna viungo vingi, wala viungo vyote havitendi kazi moja; Vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake. Basi kwa kuwa tuna *karama zilizo mbalimbali*, *kwa kadiri ya neema mliyopewa*; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani;_

*4 Kufundisha ni Upako* (Mafuta ya Roho Mtakatifu)
_1 Yohana 2:27 *Nanyi, mafuta yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha*; lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha habari za mambo yote, tena ni kweli wala si uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani yake._

*5 Ualimu ni hazina*
_Mathayo 13:52 Akawaambia, Kwa sababu hiyo, kila mwandishi mwenye elimu ya ufalme wa mbinguni amefanana na mtu mwenye nyumba atoaye katika *hazina yake vitu vipya na vya kale*._

*6 Ualimu ni wito*

_Waefeso 4:1 Kwa hiyo nawasihi, mimi niliye mfungwa katika Bwana, mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa;_

>>Kwa hiyo katika yale makundi matano ya huduma, na katika ile Kutoka 35:34 tumeona namna Mungu alivyoweka vitu ndani ya Ohaliba ili aweze kufundisha.  Kwa hiyo hivyo vitu sita vilivyotajwa hapo juu ndivyo Mungu anavitumia katika kuweka vitu vyake ndani ya Mtu.

>>Kwa hiyo ni lazima ujue tofauti yake ni nini , kwenye tafsiri ya kawaida ina maana Mungu aligawa vipawa, kwa hiyo *Ualimu ni kipawa ndani ya kipawa*

>>Kwa kiingereza tungesema ni *gift* sasa kwenye Kiswahili ni *zawadi*, ualimu ni kipawa na imebeba kipawa, na. tambua kuwa kipawa ni ofisi. Kipawa cha ualimu kinakupa authority yaani mamlaka ya kufundisha

>> *Neema* Ukienda kuangalia katika maandiko Paulo anasema  _tena walipokwisha kuijua ile *neema niliyopewa*; Yakobo, na Kefa, na Yohana, wenye sifa kuwa ni nguzo, walinipa mimi na Barnaba mkono wa kuume wa shirika; ili sisi tuende kwa Mataifa, na wao waende kwa watu wa tohara;_*Wagalatia 2:9*

>>Kwa hiyo neema inakupa nafasi. Kwenye ualimu hatufanani kila mtu ana neema ya kwake na ni tofauti kati ya mwalimu wa kufundisha masomo ya awali na yule anayefundisha ya ngazi ya juu. Haina maana ya kuwa kuna kufundisha masomo ya chuo kikuu au kufundisha darasa la kwanza au kindergarten  wewe sio mwalimu hapana. Ili mwalimu wa chuo kikuu aweze kumfundisha mwanafunzi vizuri chuo inategemea msingi aliouweka mwalimu wa shule ya awali au darasa la kwanza. kwa hiyo wote ni wa muhimu mnoo.

>>Mama yangu alisomea ualimu na alikuwa anafundisha darasa la kwanza na la pili. Miaka yote alifundisha hapo na hadi alikuja kuwa mwalimu mkuu bado aliendelea kufundisha darasa la kwanza na la pili. Na watu waliopita mikononi mwake wanamkumbuka mpake leo maana kuna alama aliweka katika maisha yao na haiwezi futika. Haijalishi wewe katika neno la Mungu unafundisha katika ngazi ipi wewe ifanye kwa uaminifu na hakika alama utakayoiweka haitafutika.

>>ile wote mmejifunza physics na chemistry na wewe ukawa unafundisha form one na mwingine anafundisha chuo kikuu, haimanishi kuwa yule wa chuo kikuu ni bora sana kuliko yule mwalimu wa form one. Ila jua kuwa katika hii nafasi ya ualimu wote tunatenda kazi ya kuujenga mwili wa Kristo. Tunakwenda sawa sawa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

*4) Karama maana yake vitendea kazi ndani ya ofisi*

>>Kwa hiyo katika kufundisha pia kuna teaching aids, yaani kinachorahisisha kufundisha. Hata kwenye neno la Mungu kuna teaching aids(zana za kufundishia). Sasa kwa wale waliopita ile shule kama tuliyosoma sisi tulikuwa tuanenda *ndude*, ehehe mnazifahamu *ndude* yaani vile vizibo vya soda kule kwetu tunaita ndude. Sasa zile tulikuwa tunatumia kuhesabu ili kujua kuongeza na kutoa. Na ilikuwa inafanyika kwa vitendo ili tuweze kuelewa namna ya kuhesabu.  *Hata kwa Mungu kuna teaching aids yaani mfano na shuhuda* kazi yake ni kusaidia kuelewa.

>> sasa sio kila mtu atakuwa nacho hiki kitu cha kufundisha,ndio maana kuna mahali napenda sana kweye biblia inasema hawata ambizana kuwe mjue Bwana kwa maan watanijua wao. Jifunze na wewe watoto wako kumjua Bwana. Sasa upako alio nao Bonnke ni tofauti na Upako wa wewe mwinjilisti wa kijiji. Bonnke ni mwinjilisti wa Africa sasa upako ulio juu yake ni tofauti na ule utakao kuwa juu yako ewe ambaye ni mwinjilisti wa kijiji. Sasa unakuta uomba Mungu akupe upako kama wa Bonnke wakati wewe ni mwinjilisti wa kijiji. Na usiige omba Mungu akupe kwa kadri yako wewe na ile nafasi aliyokupangia.

>>Sasa niulize mimi ukitaka kuiga, unasimama kwa siku nane kila baada ya muda mchache kwa mwaka mzima, na unatakiwa kila siku ufundishe kitu kipya, upate na muda wa kuomba, kusoma na kuandika vitabu na kazi zingine. Sasa ndio maana nasema usiige maana huwezi jua mzigo aliobeba mtu. Na ukiwa na karama kama hii *haitakiwi ujivune maana hii ni neema Mungu kakupa*

*5) Mwalimu ni mtu ambaye ndani yake kuna elimu ya ufalme.*

>>Elimu inayooanisha mahitaji yaliyoko katika ufalme huu na ujao na sio mfumo huu wa elimu ya kawaida ya huku duniani bali ni elimu ya ufalme.  Hii elimu ya ufalme ya Mungu ina mfumo wa syllabus yake, sasa chukulia mtu anatumia mfumo wa duniani huku anatoa elimu ya mfumo wa kanisa lake badaya ile ya ufalme wa Mungu, ujue tu kuna mahali tutakanyagana kwa maana hatuendani sawa.

>>Ndio maana Yesu alikuwa anabishana na Mafarisayo juu ya elimu waliyokuwa wanaitoa ilikuwa tofauti na ile ya ufalme wa Mungu. Japo wote walisoma torati ile ile ila walikuwa wanazitazama kwa macho tofauti, Mafarisayo waliitazama kidini wakati Yesu aliitazama kwa mfumo wa ufalme wa mbinguni.

*6) Ualimu ni tabia*

Tabia hujidhihirisha katika mwenendo wako, ndio maana ualimu sio kipawa tu bali inageuka kuwa tabia, ndio maana utaona kwa mwalimu kuwa na tabia ya kuuliza maswali ni suala la kawaida kwa maana anataka kuelewa. Na ukiona hata mtoto nyumbani ni mdadisi na anakuwa na maswali mengi basi jua kuwa kuna kipawa cha ualimu ndani yake maana waalimu huwa wanahitaji uelewa.

*7 Cheki ndani yako je moyo wako unakupa kufundisha?*
>>Kufundisha ni kutoa maelekezo

>>Kufundisha ni kufahamisha (kutoa ufahamu)

>>Kufundisha ni kusahihisha, ndio maana mwalimu mzuri hutoa usahihi mahali watu wamekosea au hawajaelwa.

>>Kufundisha ni kujenga madaraja kitu Mungu anataka uweke.
Ndio maana kabla ya kula chakula kigumu unaanza kwanza kunywa maziwa ndipo unakuja kuanza kula chakula kigumu ukisha komaa.

.. Ndio maana kama kuna mahali mwalimu haelewi anataka kuuliza swali, kwa hiyo kama unafundisha usisikie vibaya watu wakikuuliza maswali na wewe unaanza kukemea kuwa sihitahi injili za maswali, ila jua kuwa maswali yanasaidia kuelewa.

>>Kufundisha ni kuadibisha (kumtolea Shetani mtu huyo, ili mwili uadhibiwe, ili na roho iokolewe katika siku ya Bwana Yesu.) 1 Wakorintho 5;5

Kwa hiyo kama wewe unamheshimu Mungu  lazima utahitaji sana Mungu apate heshima anayostahili kuliko mapokeo ya dini yako, na endapo utaona kuna kitu kinaenda tofauti ni lazima tu utasikia vibaya.

>>Katika kulea huduma yako ya ualimu, cheki kwanza nae kulea ana huduma gani, chukulia wewe ni mwalimu unalelewa na mwinjilist si unajua lazima atakuwa anakuonesha vitu vya kuinjilisti Zaidi unakuta na wewe unaanza kuwa mwinjilist lakini huduma hiyo siyo ambayo Mungu alikupangia. Sasa hapo unakuwa unaoa huduma yako. Omba Roho Mtakatifu akusaidie ili upate watu sahihi wa kulea huduma yako. 

>>Pia ukiwa mwalimu lazima *usome sana vitabu mbali mbali kwa msaada wa Roho Mtakatifu ili uweze kuelewa vitu mbali mbali. Hivyo ni muhimu ulewe na kanuni ya kuwa mwalimu bora ni lazima uhakikishe kile kitu unachokifundisha na wewe unakiapply na ndio maana biblia inasema*

*_Jitunze nafsi yako, na mafundisho yako. Dumu katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo utajiokoa nafsi yako na wale wakusikiao pia._1 Timotheo 4:16*

>>Siku nyingine kutakuwa na sehemu ya Maswali, darasa hili litakuwa ni endelevu na tutalifanya si kila mkoa ila pale Mungu atakapotupa nafasi. Zidi kuliweka katika maombi.

*Naamini sasa umeanza kujitambua kuwe wewe ni mwalimu au sio mwalimu. Baada ya hapo jiweke wakfu kwa Bwana ili akusaidie katika huduma hii. Ubarikiwe mnoo*.

✍✍✍✍✍✍✍✍✍
🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏.

Maoni 13 :

  1. Najua kuwa mwalimu Ni lazima uwe na kina Cha neno na nitakuoaje Kama mimi Ni mwalimu wa watu wa nje au wamataifa au wa ndani yaani waliookoka tu

    JibuFuta
  2. Ni SoMo zuri Sana Sana, ubarikiwe Sana mtu wa mungu,

    JibuFuta
  3. Asante mwalimu umenisaidia. Na pia ningeomba pawe na group la watumishi ili kuweza kupata kwa urahisi mafundisho kama aya

    JibuFuta
  4. Na kama kuna ilo group basi number yangu ni +255672721193

    JibuFuta
  5. Asante mwalimu kuna kitu nimepokea.

    JibuFuta
  6. Asante Mungu akuzidishie upako.

    JibuFuta
  7. Uniweke Nami kwenye groupe nipokee mafundisho Siku kwa Siku. De

    JibuFuta
  8. Bamba yangu +243995449372

    JibuFuta
  9. Bwana Yesu asifiwe. Naomba uniambie ili na mimi nijue kipawa changu. Napenda kufundisha lakini sielewi nianzie wapi?

    JibuFuta
    Majibu
    1. Bwana wetu Yesu kristo Asifiwe. Nashukuru Mungu Kwa somo nzuri nililolipata kweny ukurasa huu. Ninaomba kujua Kam kuna group la whatsap/ Telegram.

      Futa