Jumatatu, 6 Machi 2017

HALI YA KIROHO YA ARDHI INAYOHUSIKA NA KUFUNGWA AU KUFUNGULIWA KWA MAFANIKIO YAKO sehemu 1.

✨1⃣ *SEMINA YA NENO LA MUNGU DAR ES SALAAM TANGANYIKA PACKERS*

*HALI YA KIROHO YA ARDHI  INAVYOHUSIKA NANKUFUNGWA AU KUFUNGULIWA KWA MAFANIKIO YAKO*

*MWL MWAKASEGE*

*DAY 1: 5 MARCH 2017*

Semina hii italenga maeneo  ya ardhi maalumu ya muhimu  yanayohusika kufunga watu  namna ya kuwafungulia.

*LENGO: KUHAKIKISHA MAFANIKIO YAKO YALIYOFUNGWA KATIKA ARDHI YANAFUNGULIWA*.

*1* *KUFUNGUA MAFANIKIO  YAKO YALIYOFUNGWA NA HALI YA KIROHO YA ARDHI INAYOFANYA HALI YA MAHALI UNAPOSIHI PAWE NYUMBA YA UTUMWA*.

_Kumbukumbu la Torati 6 : 12 ndipo ujitunze, usije ukamsahau Bwana aliyekutoa nchi ya Misri, nyumba ya utumwa._ Kufuatana na 2 Nyakati 7:14 ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, *na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao*. Nchi maana yake ni ardhi yenye mipaka halali ya kiumiliki

>>Hapa anazungumzia nchi na sio taifa.. maana taifa linahusisha mkusanyiko wa watu walio katika uongozi wa waliokubaliana.Taifa nalo lina mlololongo wake. Katika biblia  kuna taifa.. jamaa kabisa.. jamaa na lugha. Taifa linaweza kuwepo lakini halipo katika nchi yake.. biblia inasema  _Au Mungu amekwenda wakati gani akajitwalia taifa toka kati ya taifa lingine, kwa majaribu, na kwa ishara, na kwa maajabu, na kwa vita, na kwa mkono hodari, na kwa mkono ulionyoshwa, na kwa maogofya makuu, kama vile Bwana, Mungu wenu, alivyowatendea ninyi katika Misri, mbele ya macho yenu? Kumbu 4:34_  . Israel walikuwa taifa lakini walikuwa katika nchi ya Misri.

Wakati unasoma jua namna ya kutofautisha kati ya nchi na taifa, na nilipoanza kulitazama hili suala la ardhi lilinipa kujua  mambo mengi sana. Nilipoanza kufundisha hali ya ardhi katika  mkoa mmoja.. watu walianza kuzunguka na kusema Mwakasege  kapata wapi hiki kitu.. watu wa kule waliniambia na niliwaambia muwe na amani.. maana hili neno ni la Mungu.  Maana si wengi wanajua kuwa haya mambo ninayoongea yapo kwenye biblia.

Huwa nafundisha waalimu kuwa kabla ya kufundisha hilo neno liweke kwenye matendo kwanza wewe mwenyewe maana yake fundisha kwa shuhuda na hapa tutafanya maombi hapa ili mpate kuona. Ukiona nakufundisha masomo haya ujue mimi mwenyewe nimeyaweka kwenye matendo na ndio nimeona matokeo yake na ndipo nakuja kukufundisha kitu halisi ninanchokijua.

*2.UKILINGANISHA 2 NYAKATI 7:14 NA KUMB 6.12 UTAONA  YA KUWA HALI YA KIROHO YA ARDHI INAWEZA GEUZA ENEO KUWA NYUMBA  YA UTUMWA.*

Kumbukumbu la Torati 6 :12 ndipo ujitunze, usije ukamsahau Bwana aliyekutoa nchi ya Misri, *nyumba ya utumwa*

Nchi ni ardhi yenye mipaka halali na nchi hapa kwa mujibu wa kumbu 6:12.. *nchi ya misri nyumba ya utumwa* kwa hiyo ardhi  ya Misri imefanyika nyumba ya utumwa.Ardhi ina uwezo wa kufanya eneo kuwa nyumba ya utumwa.. tunaenda  sawa sawa?Ukitazama kiroho utaona kiupana ardhi maana hamna nchi iliyojengwa kama nyumba lakini Mungu  anaita nchi ya Misri nyumba ya utumwa.

*3.UTUMWA WA WANA WA ISREAEL ULIKUWA WA KIROHO LAKINO ULIJITOKEZA KATIKA MAISHA YAO YA KILA  SIKU*

Hapa kuna sababu 3

*I) Shida haikuwa kazi.. bali mazingira ya kiroho ya kazi waliyokuwa wanafanya hiyo  kazi*

_Kutoka 1 :11-14  Basi wakaweka wasimamizi juu yao wawatese kwa mizigo yao. Nao wakamjengea Farao miji ya kuwekea akiba, Pithomu na Ramesesi. 12 Lakini kwa kadiri ya walivyowatesa ndivyo walivyoongezeka na kuzidi kuenea. Nao walichukiwa kwa sababu ya wana wa Israeli. 13 Wamisri wakawatumikisha wana wa Israeli kwa ukali; 14 wakafanya maisha yao kuwa uchungu kwa kazi ngumu; kazi ya chokaa na ya matofali, na kila namna ya kazi ya mashamba; kwa kazi zao zote walizowatumikisha kwa ukali._

Tuangalie kazi walizokuwa wanafanya maana kazi zile walizofanya wakiwa Misri ndizo  hata Kanani walifanya maana walikuwa wanajenga miji ya akiba na majumba. Biblia inasema  wakifanya kazi ngumu, sasa hapa nataka uelewe  si kila kazi ngumu ni utumwa. Maana maeneo yote kama ni kushughukika na chokaa na ujenzi kote walifanya (Kanani na Misiri)  sasa tatizo lilkuwa ni mazingira ya kiroho.

Hata walipomlilia Mungu kwa sababu ya Utumwa. _Kutoka 2 :23 Hata baada ya siku zile nyingi mfalme wa Misri akafa; wana wa Israeli wakaugua kwa sababu ya ule utumwa, wakalia; kilio chao kikafika juu kwa Mungu kwa sababu ya ule utumwa._

Utumwa si kazi bali ni mazingira ya kiroho  yanayitengeneza hali  ya kimaisha, na  yanabana fikra na kuweka mipaka namna Ya kufanya  kazi. Na si wengi  wanajua hili. Utasema kwanini  kwa sababu

*2. WALISHINDWA KUJITOA*.

Maana ingekuwa ni kazi wangeacha.. ni sawa na mtu analalamika kuwa kazi ngumu  na bado yuko kazini nalalamika weeee lakini kazi haachi .. sasa si utoke utafute nyepesi, kuna maana gani kulalamika na kuendelea kubaki mazingira yale yale.

Unaweza ukawa mtumwa katika mazingira ya nyumbani na ni tofauti  na mazingira ya gereza maana mazingira ya nyumbani yanadanganya lakini  bado utumwa ni utumwa haijalishi uko gerezani au nyumbani.

Katika mazingira ya kawaida hawakujua kama wako utumwani.. kama Mungu asingewatangazia kuwa watumwa wasingejua. Maana walipoanza kulia Mungu  aliwaondolea utumwa na hakushughulika na uchungu bali  alishughulika na utumwa..Mzee Yakobo alikufa walimzika Kanani na hamna mtu alibaki kule waliacha kaburi tu. Na wote walirudi Misri, hawakujua kwanini wanarudi Misri, sababu ilikuwa ni ya kiroho zaidi.

*3.ILIBIDI  MUNGU  AWATOE KWA NGUVU*

Kumbukumbu la Torati 7 :8 bali kwa sababu Bwana anawapenda, na kwa sababu alitaka kuutimiza kiapo chake alichowaapia baba zenu, ndiyo sababu Bwana akawatoa kwa mkono wa nguvu, akawakomboa katika nyumba ya utumwa, katika mkono wa Farao, mfalme wa Misri.  Sio swala la kazi bali yalikuwa ni mazingira ya kiroho. Na ilikuwa  kazi ya kulima, au kutengeneza  matofali lakini ilikuwa ni kazi ya utumwa..

Japo walikuwa wanalima lakini  walikuwa wanaona uchungu.. na hawakujua nini kimewabana.. maana kama kazi ingekuwa utumwa basi kila mtu asingetafuta kazi. Maana kuna baadhi ya wapendwa hawataki kufanya kazi na wanaaza kuhalalisha kwa kutumia mistari ya biblia na kusema kuwa utaishi kwa imani  lakini Biblia inasema asitefanya kazi na asile

*4. WAISHIO NDANI YA NYUMBA WANATAMBULIWA KIROHO KWA KUANGALIA JINA LA MMILIKI WA NYUMBA HIYO.*

_Esta 8 :1-2 1 Siku ile mfalme Ahasuero alimpa malkia Esta nyumba yake Hamani, yule adui ya Wayahudi. Mordekai naye akahudhuria mbele ya mfalme; kwa maana Esta alikuwa amedhihirisha alivyomhusu. 2 Basi mfalme akaivua pete yake, aliyompokonya Hamani, akampa Mordekai. Naye Esta akamweka Mordekai kuwa juu ya mlango wake Hamani._

>>Ukisoma ile sura _Esta 7 :10 Basi wakamtundika Hamani juu ya mti aliomwekea tayari Mordekai. Ghadhabu ya mfalme ikatulia._

Sasa ubganisha na Esta 8:1.. Ester alipewa nyumba ya hamani.. Nyumba katika ngazi ya kiroho  inatazamwa tofauti sana.

Naanza kueleza Kumb 6:12 ndipo ujitunze, usije ukamsahau Bwana aliyekutoa nchi ya Misri, *nyumba ya utumwa* Ondoa misri weka utumwa..  hajailishi uko wapi kama  wewe ni Mmsiri watakujua kuwa wewe ni mtumwa  hata kama uko usa au china.

Na walipokuwa wanabishana  juu ya kuteliwa  kwa  Haruni  kuwa Kuhani wa Mungu, Mungu alisema  walete fimbo kwa ajili ya nyumba moja.. maana kila familia  wana ID (Utambulisho) . Haruni hakuhitaji kuleta fimbo ya watoto  wake, maana fimbo moja tu ilitosha kutambulisha familia yake.

Nyumba ya Yakobo   wana kitambulisho kinacho fanana. Kwa hiyo ukisema nyumba ya Yakobo haijalishi wako wapi ila wanatambulika kama ni watoto wa Yakobo. HAMANI alipokufa alikuwa na alama na alipokufa Hamani Ester ndiye alipewa  mamlaka (yaani adui ndio alipewa madaraka) .. haijalishi wanajipanga kiasi gani kurithi lakini Ester ndiye msimamizi mkuu wa nyumba yao yaani ndiye mwenye sauti. .

Ile Pete  ya Hamani alipewa modekai na alipewa na mamlaka kwenye lango.. na nyumba ile ya Hamani waliobaki wote  waliuwa. Haijalishi  hawako nyumbani  lakini  wako marked kiroho kuwa ni wa nyumba ya Hamani .. haijalishi wayahudi  wako wapi.. walikuwa marked..

Nyumba ya baba yako  kama wamepewa adui zako utapa shida  sana.. maana biblia inasema uzao wako utamiliki malango ya adui

_Mathayo 12 :29 Ama awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? Ndipo atakapoiteka nyumba yake._

Maana yake nani anayemiliki nyumba na uzao wako.. huwezi wafungua waliofungwa kama hauna nguvu ya kumshika yule aliyewashika au wafungwa

*5.MUNGU ALIWATOA WANA WA ISRAEL  KUTOkA KATIKA  NYUMBA YA UTUMWA KWA KUPITIA  KWENYE MALANGO WA NYUMBA YA UTUMWA*

_Mathayo 12 :29 Ama awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? Ndipo atakapoiteka nyumba yake._

Alitumia damu ya agano na nchi ya misri kipindi kile ilikuwa ina mazingira ya kitumwa na Mungu  alifuata uzao wa Ibarahim na alienda kuwatoa kwa sababu ya agano.. walikuwa na alama za kiagano, japo walikaa maiaka 400 na utumwani na walikuwa hawasogei kimaisha  lakini Mungu aliwatoa.

Je Mafanikio yako hayasogei  kwa kuwa uko  nyumba ya Misri   ya utumwa nayo imekufunga?

Hata kama ni kwenu ardhi  yenu imekuwa nyumba ya utumwa utapata  shida sana. Ndio maana utaona Kijana  ana akili  lakini  yuko  nyumbani, muda wote anazubaa tu nyumbani, na hatafuti hata kazi yupo yupo tu , na  unashangaa watoto  wa jirani wanasogea ila wako wamekwama kabisa..

Wewe unafikiri ni sawasawa hapa kumbe katika ukoo mna alama ya kuwa ni watumwa, yaani mmefungwa na ndio maana hamsogei  na kama mna agano na Mungu na shetani hata waaachia kirahisi rahisi

Maana unalima kama watu wengine, lakini  wako utumwani  Wana wa Israel  hawakujua na ndio maana waliona uchungu wakati wanafanya kazi, kumbe  sababu  ya mazingira  ya kiroho..

Hata wale wasimamizi walikuwa wanasimamia kwa sababu ya mazingira ya kiroho na waliwatesa sana wana wa Isarel,  ndio maana utaona Mtu anahama nyumba kutoka  nyumba  ya kupanga  kwenda kwenye nyumba yake unakuta hata kazi anachaaaza na anakuwa mvivu

Watu wengi hawajui kwanini Mungu aliwapitiasha wana wa Israel langoni katika  nyimba na hawajui kwanini.  Na alitumia malango na alitunia damu ya Pasaka waliyopaka katika malango.  Watu wako hapa wafungwa asipate  kazi.. na hata nyumbani kwake hatoki  na kakwama hapo yaani kafungwa kabisa

Wengine  wamefungwa kwa kitu cha imani na wapo wapo na asilimia kubwa sana ni vijana wa kiume hawafanyi kazi  na wanafika muda wa kuona lakini ukiwauliza kazi hawana majib u wanasema  katika  mlima wa Bwana inapatikana, msichana anakuuliza hivyo anajua kuwa huyu kijana hajajioanga bado. Sasa ili kukuheshimu anatesema ngoja  nikaliombeee kumbe kakuheshimu tuu na hataki kukuabisha.

Kuna  kitu cha imani kimepita mahali na kina shida.  Ukiwaukiza wako wapi watakueleza jina la nyumba  ya baba yao. Yesu anasema  kanisa ni nyumba  alama ya kiroho kanisa inategemea jina la kanisa.. na wengine   ukiwauliza unasali wapi watakupa jina la Mtumishi  na badala jina la kanisa..

Na ina maana ni alama.. ukisema mimi ni mlutheri ina maana una alama au mpetekoste inaonesha alama yao . Lakini akikuambia jina la mtumishi ina maana alama aliyoweka mtumishi ni kubwa (sina shida au ni vibaya ila nakufundisha tu namna ya kutafsiri haya mambo kiroho kwanza. Pia mwingine ukimuuliza jina la mchungaji wako ni nani unakuta hata hajui, ina maana kuan shida mahali mpaka umesahau jina la mchungaji wako. Kwa sababu umeshindwa kukaa chini ya mchungaji na ndio maana unasahau na jina lake .

Ardhi ni kama computer kubwa, nikakanyaga hapa ardhi inajua huyu mtu ni nani.. Ardhi  ya kule nilikozaliwa inaleta ripoti na ile ya kule ninakoishi nayo inaleta report kwa maana ardhi inatunza kumbukumbu na ndio maana Ukikataliwa mjini utakataliwa na mashambani..

Yesu anapitisha kondoo langoni.. na sio dirishani.. , na ndio maana na wewe uli utoke inabidi upite mlangoni maana wanaopita dirishani ni wezi , sasa naenda kufanya maombi hapa naunganisha ardhi ya hapa na ya huko kwako popote ulipo unapotufuatilia. Weka mikono yako katika magoti yako .

Akani alipokorofisha ardhi ilimeza wote  wa nyumbani mwake, sasa chukulia mmoja hayupo na kawaida ardhi inaambiana ina maana nae kule kule alikokuwa nae alimezwa . ndio maana utakuta ardhi ya kwenu umewafunga na wewe uko mbali na kwenu lakini utaona   pale wenzio wanapochanua wewe unachakae.

Jumapili, 5 Machi 2017

SABABU ZA KULITAJA NENO LA MUNGU (KULIHUBIRI)

SABABU ZA KULIHITAJI NENO LA MUNGU.

Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu yangu.

Karibu tujifunze Neno la MUNGU.

Leo tunajifunza sababu au umuhimu wa kila mtu kulihitaji Neno la MUNGU.

Sababu mojawapo ya kulihitaji Neno la MUNGU ni kwamba Tunalihitaji Neno la MUNGU ili likafanye mabadiliko ndani yetu, Hivyo ni muhimu sana kila mtu kulihitaji sana Neno la MUNGU.

''Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.-Mathayo 4:4''

Litokalo katika kinywa cha MUNGU ni Neno la MUNGU.

MUNGU ameshazungumza kupitia Biblia na amezungumza sana kupitia watumishi wake ndani ya Biblia ili kutusaidia sisi wanadamu.

MUNGU ametupa Neno lake Biblia ili;

1.  Tujue mpango wa MUNGU wa Wokovu kwetu.

Yohana 3:16-18  Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU.''

2.   Ili tumwabudu katika kweli na kumtumikia.

Yohana 4:24 ''MUNGU ni ROHO, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.''

3. Ili tujue jinsi ya kuwa watakatifu na tuwe watakatifu kwa kulitii.

Yohana 15:3 ''Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia.''

4.   Ili tusitende dhambi.
Zaburi 119:11 ''Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.''

5.   Tujue ahadi za MUNGU na kulitumia Neno hilo la MUNGU kwa halali.
2 Timotheo 2:15 ''Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na MUNGU, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli.''

6.   Ili lituondolee ujinga na kutupa nuru ya MUNGU.
Zaburi 119:130 ''Kufafanusha maneno yako kwatia nuru, Na kumfahamisha mjinga.''

7.   Ili tuliishi Neno hilo na kuukulia Wokovu.
1 Petro 2:2 ''Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu;''

8.   Ili litujulishe yaliyopita, yaliyopo na yanayokuja mbele yetu wanadamu.

Mwandishi mmoja wa Biblia aliambiwa ''Basi, uyaandike mambo hayo uliyoyaona, nayo yaliyopo, na yale yatakayokuwa baada ya hayo.-Ufunuo 1:19''

9.  Ili Litupe akili nzuri na  maarifa ya MUNGU.

Mithali 1:7 '' Kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu.''

10.  Ili litufanye kuwa viumbe wapya waliotengeneza na MUNGU kwa njia ya Neno lake.
2 Kor 5:17 "Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya KRISTO amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya. "

Ni muhimu sana kulizingatia Neno la MUNGU.

Usiposikia na kuzingatia Maneno ya MUNGU utayasikia maneno ya watu, ukiendelea zaidi kuyasikia maneno ya watu unaweza kujikuta unasikia maneno ya shetani, kisha kwa hayo maneno ya shetani unaweza ukajikuta unapata cheti cha dhambi.
Ni ni muhimu kukumbuka kwamba wenye vyeti vya dhambi wasipopata neema ya KRISTO inayowataka kutubu, hakika wanaweza kujikuta jehanamu.
Ndugu, Penda kusikia Neno la MUNGU halisi na fanyia kazi Neno la MUNGU.

Neno la MUNGU ni muhimu sana, na Biblia inasema

''Maana Neno la MUNGU li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.-Waebrania 4:12''

Kiini cha Neno la MUNGU ni ukombozi kwa mwanadamu ambao ukombozi huo huja kwa njia ya KRISTO, Kumpokea na kuishi maisha matakatifu kwa kulifuata Neno la MUNGU.

Warumi 10:17 ''Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la KRISTO.''

Ni muhimu sana kujua pia kwa wewe ambaye tayari umeshalipokea Neno la MUNGU, Usikubali kuitwa tu mlokole Bali okoka kwelikweli.

Neno la MUNGU ukilitii litakusaidia kumpendeza MUNGU.

Kama umemkosea MUNGU kwa mwaka uliopita basi jitahidi sana kumpendeza MUNGU mwaka huu, mtii MUNGU sasa na litii Neno lake. Kumbuka Neno la MUNGU halitapita kamwe, hivyo ni heri tu kulitii hilo.

''Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.-Mathayo 24:35''

Inawezekana kabisa umepewa kuishi mwaka huu kwa kusudi la wewe kutengeneza njia zao.
Ndugu jitahidi sana kumtii MUNGU na tii neno lake.

Ndugu usipokee neno ilimradi neno Bali pokea Neno la KRISTO maana hilo lina uzima wako.

Kama huna uzima hata hizo pesa zako nyingi zitakusaidia nini?

YESU analo neno la uzima, mtii yeye utapata uzima wake.
Mtu asiye na Neno la MUNGU Siku zote ni mtu wa kulalamika tu maana kukosekana kwa Neno la MUNGU ndani ya mtu kunaweza kukatoa nafasi ya neno la shetani kumtumia mtu huyo.

Ndugu, Ahadi za MUNGU kwako ni kweli na amina.

Tatizo la watu wengi ni kutokukaa katika kusudi la MUNGU na kuanza kujichafua kwa dhambi.

Ndugu kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa na mafanikio. songa mbele na BWANA YESU wala usikubali kurudi nyuma.

Litii Neno la MUNGU na liishi hilo.

Lakini pia kama wateule wa KRISTO inatupasa kuwa

VIUMBE VIPYA WENYE AFYA.

Yohana 4:10 "YESU akajibu, akamwambia, Kama ungaliijua karama ya MUNGU, naye ni nani akuambiaye, Nipe maji ninywe, ungalimwomba yeye, naye angalikupa maji yaliyo hai."

YESU ana chakula cha uzima ambacho ni Neno lake.
YESU ana maji ya uzima yaliyo hai, kumpokea yeye na kuishi maisha matakatifu katika yeye huko ni kunywa maji yaliyo hai ambayo hutupa uzima wa milele.
YESU ana maji ya uzima.
YESU ana uzima na uzima huo wa milele ametuandalia wateule wake.
Matokeo ya sisi kula chakula cha uzima na kunywa maji yaliyo hai ni kutufanya tuwe viumbe vipya.
Ukidumu katika neno la KRISTO na kuishi maisha matakatifu katika yeye hakika unakuwa kiumbe kipya.

2 Kor 5:17 "Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya KRISTO amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya. "

Wateule wa MUNGU ni viumbe Vipya.
Neno la MUNGU hutufanya tuwe wapya kama tukilitii.
Ndugu yangu hakikisha unakuwa kiumbe kipya.
Kiumbe kipya hakiendi kwa waganga.
Kiumbe kipya sio mzinzi wala mwasherati.
Kiumbe kipya sio muongo wala mwizi.
Kiumbe kipya huchukia dhambi na hukaa mbali na dhambi.
Viumbe vipya ni watakatifu waliokubali kubadilishwa na neno la MUNGU na kuwa wapya.
Ndugu hakikisha unakuwa Kiumbe kipya kilichookolewa na Bwana YESU.

Jambo jingine ni muhimu  kulizingatia kwa watoto wa MUNGU wote ni kwamba

WATOTO WA MUNGU NI LAZIMA TUKUE.

Wote tuliompokea YESU tumefanyika watoto wa MUNGU.
Watu wote ni watu wa MUNGU lakini sisi ni zaidi ya watu wa MUNGU, sisi tuliookoka ni watoto wa MUNGU.
Sio watoto wa kimwili Bali ni watoto wa kiroho.
Roho zetu zimezaliwa upya na MUNGU.
Ndani yetu kunatakiwa kuwepo utakatifu ambao ndio tabia ya uungu, tunatakiwa tuwe na tabia ya uungu.
Kwa njia ya kumwamini na kumpokea YESU KRISTO tumekuwa watoto wa MUNGU.
Wote tuliomwamini YESU tumefanyika watoto wa MUNGU.

Yohana 1:12-13 ".Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa MUNGU.''

Wokovu wa KRISTO ndio hutufanya kuwa karibu na MUNGU wetu.
Wokovu wa KRISTO ndio uliotufanya tuwe wana wa MUNGU.
Ni kitu kikubwa sana hiki na kwa jinsi hiyo tunatakiwa tuishi kama watoto wa MUNGU, na si watoto wa dunia.
Sasa kama watoto wateule na wapendwao tunatakiwa sana tukue kiroho.
Kila mtoto wa MUNGU anatakiwa kukua kiroho.
Na ili tukue kiroho ni lazima tuyatamani na kuyanywa maziwa ya akili yasiyoghoshiwa ambayo ni Neno la MUNGU.
Mtoto mchanga kiroho bila kunywa maziwa haya ya haki hawezi kujua kiroho na hawezi kuishi kiroho muda mrefu.
Biblia inatushauri sana kuhakikisha tunakuwa kiroho.
Ili tukue kiroho ni lazima sana tunywe maziwa ya ufahamu ambayo ni neno la MUNGU.

"1 Petro 2:2-3 "Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu; ikiwa mmeonja ya kwamba BWANA ni mwenye fadhili."

Ili tukue kiroho tunahitaji kula chakula kizuri ambacho ni neno la MUNGU.
Tunahitaji chakula ambacho hakijaharibiwa .
Tunahitaji neno la MUNGU ambalo li hai siku zote.
Kwanini ni muhimu sana kuokoka na kuukulia wokovu?
Kwanini sana ni muhimu sana kuishi maisha matakatifu ya wokovu?
Ndugu zangu kuna hukumu kwa waovu wote.
Kuna adhabu ya milele kwa wanaomkataa YESU na wokovu wake.
Biblia inajulisha kwamba kuna siku ya mwisho na ni hatari sana kwa wanaomkataa YESU na wanashindwa kuishi maisha matakatifu.
Mathayo 16:27 "Kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa BABA yake pamoja na malaika zake; ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. "

Ili tuishi vyema tunatakiwa tuwe safi na sio wachafu.
Safari ya mbinguni inahitaji watakatifu tu.
Neno la MUNGU ni chakula cha uzima na hilo tunatakiwa tulitii sana.
Kwa Neema ya MUNGU ya kutuokoa tunatakiwa sana tuishi maisha ya kumpendeza MUNGU wetu aliyetuokoa.

" MUNGU na atufadhili na kutubariki, Na kutuangazia uso wake. Njia yake ijulike duniani, Wokovu wake katikati ya mataifa yote. Watu na wakushukuru, Ee MUNGU, Watu wote na wakushukuru. -Zaburi 67:1-3

YESU alikufa kisha akafufuka, kisha akaenda mbinguni na kisha atarudi tena.
Ndugu yangu naomba ujue kwamba YESU atarudi tena na Siku hiyo atawahukumu wanadamu wote wakiwemo unaowajua wewe hivyo unatakiwa sana wewe uishi maisha matakatifu na saidia wengine kuishi maisha matakatifu ya wokovu wa YESU KRISTO.

Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.

MUNGU AKUBARIKI SANA

Ijumaa, 3 Machi 2017

JE UFALME WA MUNGU NI WA WATOTO TU NA SI WATU WAZIMA?

Karibu ndugu msomaji UNG'AMUE kitu.

UFALME WA MUNGU NI WA WATOTO WACHANGA  SI WATU WAZIMA!!!!!!!

BWAN ASIFIWE

Nakusalimu mtu wa MUNGU usishangae hicho kichwa cha somo nataka nikueleze jambo hili kidogo utanielewa namaanisha nn napokuambia ufalme wa MUNGU ni watoto wadogo si watu wazima ninamaanisha kweli unazijua sifa za mtoto Mdogo?

Sifa za mtoto Mdogo
=> mpole,mnyenyekevu,Hana makuu,si muongeaji,mtii,mkimya,ni mjinga katika ulimwengu huu,hajui dhambi,hana kiburi,dharau,majivuno,anaishi kutokana na maagizo ya wazazi wake.

Hizo ni baadhi tuu ya sifa za mtoto Mdogo je Ndugu yangu we ni mtoto mdogo?

Luka 18:15-17
15 Wakamletea na watoto wachanga ili awaguse; lakini wanafunzi walipoona waliwakemea.
16 Bali Yesu akawaita waje kwake, akasema, Waacheni watoto wadogo waje kwangu, wala msiwazuie, kwa kuwa watu kama hao ufalme wa Mungu ni wao.
17 Amin, nawaambia, Mtu ye yote asiyeupokea ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hauingii kamwe.

Watu wenye mfano wa mtoto Mdogo ndio pekee wataiyona mbingu Ndugu yangu watu wengi hawana tabia za watoto wadogo ufalme wa MUNGU upookee kama mtoto Mdogo kwa sifa hizo hapo juu nilizoziolodhesha MUNGU wetu hupenda sna watu wenye tabia za watoto wadogo MUNGU alipendezwa na daudi hata alivyokuwa mkubwa japo kwa makosa yote aliyofanya bado Tabia ya utoto mbele za MUNGU haikutoka kwake

Mathayo 18:1-4
1 Saa ile wanafunzi wakamwendea Yesu wakisema,
2 Ni nani basi aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni? Akaita mtoto mmoja, akamweka katikati yao,
3 akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.
4 Basi, ye yote ajinyenyekeshaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni.

Unaona aliyemkuu katika ufalme wa MUNGU?ni mtoto Mdogo na unatakiwa uongoke uwe kama mtoto Mdogo bila hivyo Mbinguni utapasikia unatakiwa kujinyenyekeshaye mbele za MUNGU ukiwa na sifa za mtoto huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni MUNGU hawafunulii watu wazima waliojawa kiburi dharau majivuno mashindano Bali watoto wachanga

Luka 10;21
21 Saa ile ile alishangilia kwa Roho Mtakatifu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya umewaficha wenye hekima na akili; umewafunulia watoto wachanga; Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyokupendeza.

MUNGU amewaficha wenye hekima na akili (watu wazima) Bali amewafunulia watoto wachanga maana ndivyo MUNGU wetu apendavyo watu watu wanaomba MUNGU awafunulie mambo wanataka wazijue siri za MUNGU katika dunia hii wengine wanaomba MUNGU afunue macho yao waone sikiliza mtu wa MUNGU je ww unakifua cha kuhifadhi siri zake? We sio mtu wa lopo lopo muongeajei? Je wewe sio mpole na mtulivu?je ww ni mkimya kama mtoto mchanga mpaka akufunulie siri zake uwone?

Sikiliza MUNGU hashei siri zake wapumbavu watu wazima ung'ang'ania MUNGU nionesha nataka nione je unatabia za mtoto mchanga? Maana MUNGU hupenda kuwafunulia watoto wachanga ndivyo apendavyo yeye MUNGU hashei siri zake na watu wazima wapumbavu sikuambii uwe mtoto katika akili zako sivyo

1korinto 14:20
20 Ndugu zangu, msiwe watoto katika akili zenu; lakini katika uovu mgeuzwe watoto wachanga, bali katika akili zenu mkawe watu wazima.

Ndio usiwe mtoto katika akili zako lakini katika uovu mgeuzwe watoto wachanga Bali katika akili zenu mkawe watu wazima ndivyo unavyotakiwa katika uovu wa namna yoyote kuwa mtoto usiwe muongeji usiwe na kiburi dharau majivuno mzinzi muasherati muongo msengenyaji maovu yoyote yale kwako uwe kama mtoto mchanga maana haya hayajui yeye mtoto mchanga Hapo ndipo MUNGU atakufunulia mengi na ufalme wa MUNGU utakaa ndani yako

Na MUNGU akubariki .

DHAMBI YA KUMKOSOA MWENYEZI MUNGU

<(") HII DHAMBI YA KUMKOSOA MUNGU NA UUMBAJI WAKE, JE NANI ATAPONA???
_________________________________
Ilikua  imezoeleka kuona  ni wasichana  na wanawake kujichubua ngozi zao,  ingawa  sio sahihi na wala si mpango wa Mungu  lakini  roho  hiyo  ya  mwanamke  Yezebeli  imepamba moto ktk nyakati hz  za  kumalizia,
na  sasa  imekuwa  kama  mchezo tu,  si wanawake, si wanaume tena  siku  hz  mpaka  na WACHUNGAJI nao wameingia ktk mtego huu wa Ibilisi,  nao  wamekua wakosoaji wakubwa wa Mungu na uumbaji wake.
_________________________________
Katika kusumbuka kuutafuta uzuri,  watu wengi leo  wanamtenda Mungu  dhambi  kwa  kumsahihisha,  kana kwamba  Mungu aliwaumbia viungo vyao kimakosa (kwamba  alikosea kuwaumba walivyo na badala yake angewaumba kama jinsi wanavyotaka wao),
*************************-***-****
Hii  si  sawa  hata  kidogo,  na ingawa  Mungu amenyamaza  lkn  ipo  siku ambayo  watu watajuta wakitafuta njia ya kutubu na wasiipate,
*********************************
Mungu anasema  kila alichokiumba na tazama kilikua chema (kikiwa kama kilivyo ktk asili yake) MWANZO 1:31.
_________________________________
Suala  la  kuvaa  nywele  za wafu (mawigi), kuweka  kucha  bandia,  kope, nyusi, meno na  hata kubadili asili ya ngozi kwa  kujichubua,  nakuambia  ipo  siku  inakuja ambayo watu  watajuta  kuvifanya,  na  siku  hiyo  haitawaonea  huruma  wachungaji wala  mama wachungaji wanaomtukana  Mungu  kwa  kumwona  hajui  kuumba  ila wao ndo  waumbaji wazuri  kuliko yeye,  maandiko yanasema,  Mtu  akimuheshimu  Mungu, Mungu pia atamuheshimu mtu huyo,  la   hakumuheshimu  basi  atahesabiwa kuwa ni mkosa, (1SAMWELI 2:30)
_______________________________
MAANDIKO  YAFUATAYO  YAKUSAIDIE KUELEWA VIZURI  UJUMBE HUU:
WARUMI 9:19-21,
ISAYA 29:16,
YEREMIA 13:23,
____ MWENYE MASIKIO NA ASIKIE______.


Ni kosa kubwa sana kumkosoa MWENYEZI MUNGU.

ALIPOUMBA VITU VYO VILIKUWA KAMILIFU VISIVYO NA KOSORO, je wewe ndio mjuzi kuliko YEYE?

TAFAKARI CHUKUA HATUA

KWA NINI NINAITEGEMEA DAMU NA JINA LA YESU?

Kinacho sababisha niitegemee DAMU NA JINA LA YESU NI KWA SABABU NILINUNULIWA NA YESU MWENYEWE KWA DAMU YAKE. NA NINAPATA MSAMAHA WA DHAMBI KWA JINA LAKE na ninasafishwa kwa DAMU YA YESU.

UFUNUO 5

9 Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,
10 ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.
11 Nikaona nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi, na za wale wenye uhai, na za wale wazee, na hesabu yao ilikuwa elfu kumi mara elfu kumi na elfu mara elfu,
12 wakisema kwa sauti kuu, Astahili Mwana-Kondoo aliyechinjwa, kuupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na baraka.
13 Na kila kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi na chini ya nchi ya juu ya bahari, na vitu vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia, vikisema, Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na yeye Mwana-Kondoo, hata milele na milele.
14 Na wale wenye uhai wanne wakasema, Amina. Na wale wazee wakaanguka, wakasujudu.

BARAKA ZOTE, ZINAPATIKANA KWA JINA LA YESU,
MSAMAHA KWA JINA NA DAMU YA YESU.
TUNASAFISHWA KWA DAMU YA YESU NA KWA JINA LA YESU MWENYEWE.

NAJIVUNIA HILO katika Kumwamini.

Usiufanye moyo wako kuwa mgumu, jinyenyekeze KWA YESU NA utasamehewa na kuwa safi kwa DAMU NA JINA LAKE.

MUNGU AKUBARIKI .

Alhamisi, 2 Machi 2017

KUNA FAIDA KUBWA KATIKA KUTOA KULIKO KUPOKEA

KUNA FAIDA KUBWA ZAIDI KATIKA KUTOA KULIKO KATIKA KUPOKEA.

Shalom mteule wa KRISTO upendwaye sana na MUNGU BABA.

Karibu tujifunze Neno la MUNGU.

Matendo 20:35 ''Katika mambo yote nimewaonyesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge, na kuyakumbuka maneno ya Bwana YESU, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni heri kutoa kuliko kupokea.''

Ukitoa utasababisha aliyepokea amshukuru MUNGU na jambo hilo kukuongezea kitu wewe mtoaji maana wewe ndio chanzo cha shukrani hiyo.

Utoaji wako utakupa sifa na heshima.

Lakini pia ukitaka kuwa mtoaji anayetoa katika mpango wa MUNGU basi Fanyika kwanza wewe kuwa sadaka ndipo utoe sadaka.
Ukifanya hivyo utabarikiwa sana rohoni na mwilini.

''Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake MUNGU , itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza MUNGU , ndiyo ibada yenu yenye maana. Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya MUNGU yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu. ''

Jambo muhimu pia la kukumbuka ni kwamba MUNGU hataki matoleo ya ubatili.
Matoleo ya ubatili ni sadaka isiyo sahihi mfano huwezi kuiba pesa harafu ukasema ''ngoja niipeleke kanisani ili MUNGU anibariki zaidi''. Hapo utakuwa unajidanganya wewe mwenyewe na huo ni ubatili mkubwa. Matoleo ya ubatili ni pamoja na kupeleka sadaka isiyo sahihi mfano una laki 1 mfukoni lakini unamtoleaMUNGU Tsh. 100. hii sio haki na kumbuka kwamba hata hiyo laki moja uliyonayo ni MUNGU kakupa na MUNGU hapa anaangalia tu utii wetu sio kwamba ana shida na pesa.

Lakini utoaji wa sadaka safi ni zaka kamili ni muhimu sana na ni agizo la MUNGU kwetu lenye matokeo mazuri sana kwetu watoaji.

Biblia inasema kwamba ni heri kutoa kuliko kupokea.
Maana yake nini?

Kuna faida kubwa zaidi katika kutoa kuliko katika kupokea.

FAIDA NNE(4) ZA KUTOA MATOLEO SAHIHI KWA MUNGU.

1. Ukitoa utakuwa unaweka hazina mbinguni ambapo hakuna atakayeiondoa.

Mathayo 6:19-21 '' Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba; bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi; kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.''

-Kutoa matoleo sahihi ni kuweka hazina mbinguni.

Hazina ni nini?

Hazina ni ni mali au vitu vya thamani  vinavyohifadhiwa eneo zuri kwa ajili ya matumizi ya baadae.

Kwa serikali, hazina ni mahali ambapo shughuli za serikali zinazohusu fedha zinaendeshwa.

Kiroho tunaweza kusema kwamba hazina ya wateule wa MUNGU ni mahali mbinguni ambapo matokeo ya utoaji wa mteule huonekana na kufanyiwa kazi yenye manufaa sasa kwa mteule huyo na baadae kwenye uzima wa milele.

Wako Malaika wa MUNGU walio katika kitengo cha uhazini mbinguni kiasi kwamba hakuna hazina ya mteule inayoweza kupotea wala kuibiwa wala kuondolewa.

Mhazini ni mtunza fedha au mali katika eneo zuri na salama, mbinguni wako Malaika katika eneo hilo hivyo Mteule unapotoa kwa moyo na kwa upendo kwa MUNGU hakika hazina yako mbinguni inaongezeka, ndio maana Biblia imesema kwamba ni heri kutoa kuliko kupokea.

Kuna faida kubwa katika kutoa kuliko katika kupokea.

Roho yako itakapokuwapo katika ufalme Wa MUNGU ndipo na hazina yako ya utoaji wako itakapokuwa.

2. Kitendo cha wewe kutoa maana yake unamjaribu MUNGU ili akukuze zaidi.

Malaki 3:10-12 ''Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema BWANA wa majeshi. Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema BWANA wa majeshi.''

Kuna watu shetani huwapangia magonjwa mara kwa mara lakini hawaumwi kwa sababu MUNGU anamkemea mharibifu wa afya zao kwa sababu tu ya utoaji wao sahihi na kwa uaminifu na upendo wa fungu la kumi na sadaka.

MUNGU anataka tumjaribu kwa matoleo.

MUNGU ameahidi madirisha ya mbinguni kufunguka. Madirisha ya mbinguni yakifunguka kwako kwa sababu ya utoaji wako sahihi na wa kudumu hakika huko mbinguni zitatoka baraka nyingi na upendeleo katika kazi, uchumba, ndoa na chochote kinachokuhusu.

MUNGU anaposema atakubariki kwa sababu ya uaminifu wako sio kwamba atakubariki pesa tu bali ni mambo mengi ya kukubariki.

Mwanzoni mwa maisha yangu ya wokovu nilikuwa na ugumu wa kutoa fungu la kumi lakini katika miezi ambayo sikuzingatia kutoa fungu la kumi nilikutana na matatizo ambayo nilitumia pesa mara tatu hadi saba zaidi ya fungu la kumi ambalo nilitakiwa kutoa.

MUNGU anaposema kwamba atamkemea yeye alaye uchumi wako hakika atamkemea.

Hata kama ni magonjwa ya mlipuko kitaifa lakini wewe mtoaji mwaminifu utashangaa tu uko salama, hapo MUNGU amemkemea anayetaka kukuharibia.

Mama mmoja alienda kwa mganga wa kienyeji na kupewa dawa ili kumpata baba mmoja aliyeokoka ambaye alikuwa mwaminifu kwa MUNGU, Yule dada alipewa nyoka ili nyoka yule amtume kwa yule kaka ili yule kaka amchukuie mkewe na kwa njia hiyo ampende yule dada wa nje. Yule dada akiwa na nyoka wake aliikaribia nyumba ya yule kaka na akamtuma yule nyoka ili akafanye mambo kwenye nyumba ile. Yule nyoka alienda na kurudi haraka akiwa amejeruhiwa na alipofika alimwuma yule aliyemtuma kisha akatokomea kusiko julikana. Wale watu wa MUNGU wala hawakumuona yule nyoka katika familia yao lakini yule dada aliteseka sana na hadi akaenda kwa mganga na mganga akaanza kumwambia hana dawa ya kumtibu huku akimtukana. Hakika MUNGU humkemea mharibifu katika mazingira ambayo sisi hatujui, ila uaminifu wetu kwa MUNGU katika utoaji wa zaka na saka hakika MUNGU hutuzingira.

Ukweli ni kwamba hakuna aliye mwaminifu hata mmoja ambaye akimtolea MUNGU habarikiwi, bali wote hubarikiwa katika maeneo mbalimbali katika maisha yao.

Hakika kuna faida nyingi sana katika utoaji.

3. Utoaji wako utakuwa sababisho la wewe kupata kitu fulani kutoka kwa MUNGU.

Mwanzo 8:16-22 '' Toka katika safina, wewe, na mkeo, na wanao, na wake za wanao pamoja nawe. Utoe pamoja nawe kila kilicho hai kilichomo pamoja nawe, chenye mwili, ndege, na mnyama, na kila kitambaacho, chenye kutambaa juu ya nchi; wajae katika nchi, wawe na uzazi, wakaongezeke katika nchi. Basi Nuhu akatoka, yeye, na wanawe, na mkewe, na wake za wanawe pamoja naye; kila mnyama, na kila kitambaacho, na kila ndege, kila kinachokwenda juu ya nchi kwa kabila zao, wakatoka katika safina. Nuhu akamjengea BWANA madhabahu; akatwaa katika kila mnyama aliye safi, na katika kila ndege aliye safi, akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu. BWANA akasikia harufu ya kumridhisha; BWANA akasema moyoni, Sitailaani nchi tena baada ya hayo kwa sababu ya wanadamu, maana mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu ujana wake; wala sitapiga tena baada ya hayo kila kilicho hai kama nilivyofanya. Muda nchi idumupo, majira ya kupanda, na mavuno, wakati wa baridi na wakati wa hari, wakati wa kaskazi na wakati wa kusi, mchana na usiku, havitakoma. ''

Baada tu ya Nuhu kutoka ndani ya safina alimjengea MUNGU Madhabahu kisha akatoa sadaka nzuri kwa MUNGU.

MUNGU baada tu ya kuikubali sadaka ya Nuhu alitoa baraka.

MUNGU alisema  Hatailaani nchi  wala kuipiga kwa gharika dunia yote, Hiyo ni baraka ya MUNGU inayodumu hata leo kwa sababu ya sadaka za Nuhu. Hata iweje leo haiwezekani dunia nzima kuzama kwenye maji kama ilivyotokea wakati wa Nuhu, hiyo ni baraka kwa Nuhu na uzao wake wote ambao ni mimi na wewe.

  MUNGU akiikubali sadaka yako hakika tarajia Muujiza wa MUNGU maishani mwako.

Kuna njia nyingi za MUNGU kukubariki kama utazingatia utoaji wa sadaka safi na zaka sahihi.

Sadaka inaweza ikafufua yale yaliyo kufa maishani mwako.

Dorkasi alikufa lakini sadaka zake zikawa muujiza wa kumfufua.

Hata leo yako mambo yaliyokufa maishani mwako lakini sadaka yako inaweza kuyafufua.

Utoaji wako unaweza kuzifufua baraka zako zilizokuwa zimekufa.

Hebu jifunze katika maandiko haya.

Matendo 9:36-41 '' Na mwanafunzi mmoja alikuwako Yafa, jina lake Tabitha, tafsiri yake ni Dorkasi (yaani paa); mwanamke huyu alikuwa amejaa matendo mema na sadaka alizozitoa. Ikawa siku zile akaugua, akafa; hata walipokwisha kumwosha, wakamweka orofani.  Na kwa kuwa mji wa Lida ulikuwa karibu na Yafa, nao wanafunzi wamesikia ya kwamba Petro yuko huko, wakatuma watu wawili kwake, kumsihi na kusema, Usikawie kuja kwetu. Petro akaondoka akafuatana nao. Alipofika, wakampeleka juu orofani wajane wote wakasimama karibu naye, wakilia na kumwonyesha zile kanzu na nguo alizozishona Dorkasi wakati ule alipokuwa pamoja nao. Petro akawatoa nje wote, akapiga magoti, akaomba, kisha akaelekea yule maiti, akanena, Tabitha, ondoka. Naye akafumbua macho yake, na alipomwona Petro akajiinua, akaketi.  Akampa mkono, akamwinua; hata akiisha kuwaita wale watakatifu na wajane akamweka mbele yao, hali yu hai. ''

4. Sadaka yako itakuwa ukumbusho mbele MUNGU.

Matendo  10:1-8 '' Palikuwa na mtu Kaisaria, jina lake Kornelio, akida wa kikosi kilichoitwa Kiitalia,  mtu mtauwa, mchaji wa MUNGU, yeye na nyumba yake yote, naye alikuwa akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba MUNGU daima. Akaona katika maono waziwazi, kama saa tisa ya mchana, malaika wa MUNGU, akimjia na kumwambia, Kornelio! Akamtazama sana, akaogopa akasema, Kuna nini, Bwana? Akamwambia, Sala zako na sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za MUNGU. Sasa basi, peleka watu Yafa, ukamwite Simoni, aitwaye Petro. Yeye ni mgeni wa mtu mmoja, jina lake Simoni, mtengenezaji wa ngozi, ambaye nyumba yake iko pwani, atakuambia yakupasayo kutenda.  Na yule malaika aliyesema naye akiisha kuondoka, Kornelio akawaita wawili katika watumishi wake wa nyumbani, na askari mmoja, mtu mtauwa katika wale waliomhudumia daima; na alipokwisha kuwaeleza mambo yote akawatuma kwenda Yafa.''

Sadaka ya Kornelio ikawa ukumbusho kwa MUNGU.

Kuwa ukumbusho sio jambo dogo, Malaika alishuka kwa Kornelio kwa sababu ya utoaji wake sahihi wa matoleo kwa MUNGU.

Ni neema ya MUNGU malaika aje kwako ametumwa na MUNGU.

sadaka sahihi inaweza kumfanya MUNGU amtume Malaika.

Malaika wa MUNGU akishuka kwako ni kwa kusudi la MUNGU.

Sadaka kuwa ukumbusho kwa MUNGU ni jambo la muhimu sana.

Naamini kuanzia sasa utakuwa mwaminifu kwa MUNGU katika kutoa zaka kamili na sadaka halisi ili MUNGU akutendea Mema aliyoyakusudia maishani mwako.

Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.

MUNGU AKUBARIKI SANA.

UVIVU WA KUSOMA NENO LA MUNGU NDIO UMELETA MAJANGA HAYA!!!!

UVIVU WA KUSOMA NENO LA MUNGU NDIO UMELETA MAJIBU HAYA YA WAKRISTO WA SASA KATIKA HOJA ZIFUATAZO..* 👇👇

1⃣ *KUVAA NGUO ZA NUSU UCHI. (1 Timotheo 2 :9).*

_Mungu anaangalia Roho na si Nje._

2⃣ *KUIMBA NYIMBO ZA BONGOFLEVA (1 Petro 4 :2-4, Yakobo 4: 4)*

_Mi nasikiliza Ujumbe Tu, acha Ushamba nani amekuambia kuwa ni dhambi._

3⃣ *WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI KUSHINDANISHWA (Efeso 4:11-12, 1 Wakorintho sura ya 12)*

_Kuna ubaya gani? Tunawatia Moyo._

4⃣ *WANA NDOA KUACHANA (Mathayo 19 :9)*

_Ruksa..! Ndoa imenishinda. Raha JIPE mwenyewe._

5⃣ *KUZINI (1 Wakorintho 6 :18)*

_Tutatubu._

6⃣ *WACHUNGAJI KUTAKA PESA NDIO WATOE HUDUMA (Mathayo 10 :9)*

_Unataka nile wapi? Mtenda Kazi ana stahili Ujira wake au umeshau mtendakazi wa madhabahuni hula vya madhabahuni._

7⃣ *KUFUNGA NA KUOMBA (Mathayo 26 :41,I Petro 4 :7).*

_Kuna haja gani ya kufunga wakati Nabii yupo? Vitambaa, Sabuni, mafuta ya UPAKO yapo?_

8⃣ *KUSOMA NENO (Kolosai 3:16)*.

_Yaan nakosa muda jamani, mmh basi TU Mungu mwenyewe anajua._

Wakat muda wote yupo online kwenye mitandao ya kijamii akichat na kupost picha.

9⃣ *KUHUDHURIA IBADANI (Waebarania 10 :25)*

_Nipo Busy sana, hizi Kazi nazo zinabana kweli_

🔟 *KUKEMEA DHAMBI (1 Timotheo 5 :20)*

_Hizo ni injili za zamani. Wewe TUTABIRIE tu na utufanyie Maombezi._

🔹🔹🔹🔹🔹🔹🔹

*JE, TUTAPATAJE KUPONA TUSIPOUJARI WOKOVU MKUU NAMNA HII* ❓

👉 *_lakini mwenye kuvumilia mpaka MWISHO ndio atakayeokoka_* .

  _Mathayo 24 :13_

*MPENDWA KUWA MACHO*